Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

Naona kuwa wangetaka kudai labda kipindi cha Mkapa au wangetime muda mwingine au kwa kuwa na rais mkristo, but the way sidhani kwamba Jk ataweza kufanya suala hili ni kwamba anaogopa sana
 
Maswala ya dini ni magumu na very controversial, na mara nyingi hakuna mshindi kwani kila mmoja anajiona yuko right. Ni swala la imani, na kiumbe akiamini ujue ameamini sio rahisi kumbadili....kumbuka ya Kibwetere na watu walivyoteketea.

Kosa kubwa ni pale CCM ilipoweka katika ilani yake ya 2005 hilo swala la mahakama ya Kadhi, watalijutia kwani kila mmoja sasa anaruka, ni kama 'hot potato'
 
Hapa nina wasiwasi na shule ya mufuti. Nafikiri amekuwa mzembe wa kufikiri na ameongozwa na hisia. Ningeomba atushauri kuichukia ccm tu kwa sababu imetutia umaskini, lakini sio kwa sababu ya mahakama ya kadhi.
 

alikuwa anaandika kiprofesa zaidi ,sasa ameamuwa kulainisha lugha ndiyo unampata teh teh teh teh
 
Ibara ya 108(b) ya Ilani ya CCM ya 2005-2010 inatoa ahadi ifuatayo:
Kulipatia ufumbuzi suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara.
Kiini cha madai ya "tumeahidiwa CCM itaanzisha mahakama ya kadhi" ndiyo mstari huo. Mtu yeyote makini anaweza kuona pasipo shaka kuwa CCM haikuwaahidi Waislamu kuwa serikali itaanzisha mahakama ya kadhi. Kwa kadiri watu wanazungumza ni wazi hakuna aliyesoma hasa CCM imeahidi nini.

Lakini pia kitu ambacho sijaona watu wakilalamika na kukipigania ni ile ahadi ya (a) ya ibara hiyo ambayo inasema:

Kuzifanyia marekebisho sheria za mirathi na zile zinazoonekana kuwakandamiza wanawake.

Kimsingi utaona ahadi ya kufanyia marekebisho sheria na ile ya "kulipatia ufumbuzi suala" haziko katika uwanja mmoja. Moja inaeleza hatua za kuchukua nyingine inaongelea mpango wa kufikiria ni hatua gani zichukuliwe. Hivyo, wenye madai ya kuahidiwa kitu hapa ni Wanawake wa Tanzania zaidi kuliko kundi la Waislamu wote.

suala la (d) la ibara hiyo kwa mfano limeshaanza kufanyiwa kazi kwa kuundwa kwa Huduma ya Uendeshaji mashtaka nchini.
 
Hapa nina wasiwasi na shule ya mufuti. Nafikiri amekuwa mzembe wa kufikiri na ameongozwa na hisia. Ningeomba atushauri kuichukia ccm tu kwa sababu imetutia umaskini, lakini sio kwa sababu ya mahakama ya kadhi.
.
Mufti yuko sawa, kwa Muislam yoyote anajua umuhimu wa mahakama ya kadhi, kwa asiye kuwa
Muislamu haimuhusu, kubakia kama mtazamaji tu!
 
.
Mufti yuko sawa, kwa Muislam yoyote anajua umuhimu wa mahakama ya kadhi, kwa asiye kuwa
Muislamu haimuhusu, kubakia kama mtazamaji tu!

hii ni kweli. Sasa wanapoipeleka Bungeni wale wasio Waislamu watoke Bungeni?
 
.katika hili BAKWATA Imepata fursa muhimu sana ya kurejesha imani kwa WAISLAMU.
.
Waislamu wako pamoja juu jambo hili.
 
hii ni kweli. Sasa wanapoipeleka Bungeni wale wasio Waislamu watoke Bungeni?

Kwanza hii maana yake ni kuwa wakati wa kulijadili hili swala bungeni, wabunge wasio Waislamu wakae kimya - wafunge midomo yao kwa sababu hili swala haliwahusu. Jaribio la kuwanyamazisha watanzania wasio Waislamu kuongelea swala hili tunalishuhudia hadi humu ndani ya JF kwa kigezo kuwa ni mbumbumbu kwa maswala ya Kiislamu hasa yanayohusu Sharia na mahakama ya kadhi. Sasa kama ni hivyo kwa nini swala hili linalohitaji mabadiliko ya kikatiba lipelekwe bungeni ? Je, litaundwa kamati ya bunge ya Waislamu watupu kulijadili ?
 

kwa ufupi ni kuwa kama wanataka Watanzania wasio Waislamu wasilizungumzie wala kulitolea maoni, basi wasilihusishe na chama kimoja cha siasa, serikali, wala Bunge. Wakilizungumzia katika mikutano yao ya Bakwata na taasisi nyingine na kulisimamia wao wenyewe sisi wengine tutasema "more power to them" na wala hatutalitolea mawazo yoyote.
 
Kinachoshangaza ni kwamba ujerumani inafanya jitihada za kuwa karibu na waislam lakini nchi kama TZ second user wa dini wanapinga kutafuta njia muafaka wa kutoa maamuzi yatakayo onyesha hawaja sukumwa na upande fulani!!!!!!!!!. Naona tumefika pabaya kwani mimi huwa naamini Katika waafrika basi wa TZ ni wastaarabu, but on that issue wamechemsha and mbaya zaidi alie toa maamuzi amejenga tabaka ambalo litakua linahisi ni watu baki...Na laweza hatarisha usalama wa nchi. Kwani waislam la wakiristo hawana tabu ila viongozi jamaniii, hawajui jinsi yakupinga kitu au kutoa maamuzi yenye kuleta tija kwenye taifa letu.
Mimi naona mfumo waelimu zetu unapelekea watu kutokua waadilifu, kwani hata mtu akifanya tafiti anakua bias kwenye maamuzi, as results anatuletea matatizo tusiojua kinachoendeleaaaa, Jamani kudesa kubaya kwani siku zote utakua unatoa majibu ambayo ni msukumo wa mawazo yakoooooooooooo. Let science speek!!!! . Sirikali engeweza toa haja kua gharama za kuendesha chombo hicho si juu ya serikali na sirikali itahakikisha hamna kinachofanyika ndani ya chombo hicho kinyume na katiba ya nchi, from there you raise discussions............hope could work, lakini Maaskofu na heshima zao wakaanza nao kutoa amri na kuiweka sirikali pabaya na nchi kwa ujumla, tunaenda pabaya jamani tuaamke, kwani hawa viongozi wadini wasifikiri yatakapo tokea machafuko nchini wao watasalimika, itakula wote, kama si kiongozi wa dini au nchi basi ndugu yake ....

Jamani tudumishe umoja wetu na tuaache kusukumwa na matamanio ya nafsi zetu, natusilipeleke suala kama hili ki ushabiki wa ya yanga na simba... tutaishia pabayaaaaaaaaaaaaa.

Mungu ibariki Tanzania
 

Nani aiunde hii mahakama ya Kadhi, na iendeshwe kwa gharama ya nani?
 
Soma maelezo yangu vizuri . Kwangu mimi huo unatakiwa uwe mjadala ili kuona nani anatakiwa abebe gharama? Ama kuunda mahakama ya kadhi nafiri ni waislamu ndo wanatakiwa kufanya hivyo but wakisimamiwa na sirikali
 
Soma maelezo yangu vizuri . Kwangu mimi huo unatakiwa uwe mjadala ili kuona nani anatakiwa abebe gharama? Ama kuunda mahakama ya kadhi nafiri ni waislamu ndo wanatakiwa kufanya hivyo but wakisimamiwa na sirikali

Ninapata wasiwasi kuwa zaidi ya mufti kuwa na taaluma yenye mashaka mbele ya dunia ya leo (kiwango kidogo cha elimu), lakini pia waislamu wanaotetea hoja hii wameshindwa kuonyesha uelewa unaoweza kuheshimika mbele ya wachambuzi wa mambo wenye taaluma zao katika dunia ya sasa. Ni aibu kuitetea hoja ya mahakama ya kadhi itakayoundwa Dodoma kwa gharama za raia wa Tanzania wenye dini na madhehebu tofauti. MDEBWEDO wa aina hiyo HAUPO. Waunde mahakama zao za kadhi na wazigharamie. Kama uwezo wao wa kufikiri hautoshelezi, basi serikali iwasaidie. Na hapo katika kuwasaidia hakuna cha Juma wala John, hakuna cha muislamu wala mkristu. Ni kuwasaidia watu walioshindwa kufanya mambo yao ya "ibada" bila kuingiliwa "and without prejudice to or against the prevailing State laws".
 
Last edited:
Soma maelezo yangu vizuri . Kwangu mimi huo unatakiwa uwe mjadala ili kuona nani anatakiwa abebe gharama? Ama kuunda mahakama ya kadhi nafiri ni waislamu ndo wanatakiwa kufanya hivyo but wakisimamiwa na sirikali

Nani ajadili suala hilo? Wakristu washiriki kwenye mjadala huo au waislamu peke yao?
 
Kwani mahakama inatakiwa kuundwa bungeni? Mimi nafikiri kinachotakiwa ni waislamu waunde mahakama ya kadhi kama katiba inaruhusu, na kama katiba ya nchi inaruhusu ni haki yao kuwa na chombo kama hicho bila kuvunja sheria za nchi. Otherwise kusema kiwango cha elimu ni ndogo haisaidii sana , kwani hata aliekua hajasoma anatakiwa aeshimiwe , na mawazo yake kwakua kusoma nayo ni relative kwani Prof. wa mifupa hawezi kua mtoa hoja mzuri wa kutengeneza tekinolojia ya kusukuma dawa kwa kutumia electronic siringe lakini aweza toa wazo ambalo hata ambae hajaenda shule fundi mekanika wa kule sinza na likawa na maana likifanyiwa kazi na wataalamu wa fani husika(wahandisi).
Unapojadili suala hili jaribu tu kuonyesha constructive idea itakayo kua na manufaa kuliko kuonyesha umesoma na ni hodari wa kujenga hoja za kisomii.

Nakuunga mkono kwenye kipengele kua waislamu waunde chombo hicho wenyewe but tumia kauli nzuri kama kawaida ya mtanzania
 

Katiba ya nchi ni kanuni ambazo jamii imejiwekea ili zifuatwe katika maisha yao ya kila siku. Kama suala ni kuingizwa kwenye katiba sioni ubaya ili mradi iwekwe wazi kuwa halazimishi mtu kwenye hilo. Mbona Hiyo BAKWATA Ilipoanzishwa wakati wa Nyerere maaskaofu hawakupinga?.

Halafu kama issue ni kuingizwa kwenye katiba, huoni kuwa kwa sheria hizohizo kuingizwa kwenye mahakama za kawaida zinakuwa tayari zimeingizwa kwenye katiba ( Sheria mama?). hoja yako bado imeelemea upande mmoja. Ndoa imefungishwa na Sheikh kwa sheria za dini yao ya kiislamu wewe hakimu Brown Christian unatumia sheria za dini isiyokuhusu kuhukumu wapi na wapi?. Huku ndiyo mwanzo wa kutafuta patashika. Kwa hili serikali imekosea inabidi watu waache idiology zao na kufanya kazi ya nchi sio maaskofu.
 
Kwani mahakama inatakiwa kuundwa bungeni?

yeah! Vinginevyo kila mtu angejiundia mahakama yake.
Mimi nafikiri kinachotakiwa ni waislamu waunde mahakama ya kadhi kama katiba inaruhusu, na kama katiba ya nchi inaruhusu ni haki yao kuwa na chombo kama hicho bila kuvunja sheria za nchi.

Ok.
Otherwise kusema kiwango cha elimu ni ndogo haisaidii sana

Hapa najua hunizungumzii mimi.


hata hapa hayanihusu kwani sijasema lolote kuhusu elimu au usomi wa mtu.

Nakuunga mkono kwenye kipengele kua waislamu waunde chombo hicho wenyewe but tumia kauli nzuri kama kawaida ya mtanzania

Sijatumia kauli mbaya kwa mtu yeyote kwenye mada hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…