Mwanakijiji,
Mkuu nitaendelea kukujibu kwa sababu bado kabisa majibu yako ni ndani ya kabati hilo ulojifungia... hutaki wala husikii sauti nje ya kabati hilo..
Mkuu binafsi sikubaliani na swala la mahakama ya kadhi kwa sababu za msingi ambazo hazihusiani kabisa na dini zetu.. Ni mahakama yenyewe ya kadhi nikitazama WATU na MAZINGIRA tunayoishi ndipo nakuja na hoja zangu..lakini wewe umeshikilia Udini tuuuu kiasi kwamba maswali yako ni ya kidini tupu... ukiwaona wao ni waislaam na wewe Mkristu.. mambo ya CCM na Chadema..kwa ufinyu huo ndio maana Pinda kajibu ujenzi wa barabara Kigoma umefanywa na chama chake - CCM..
Mkandara, tatizo lako unachodai wengine wanfanya ndicho wewe unafanya. Hoja zako japo ni nzuri lakini haziwezi kusimama hadi umshambulie mtu. Mara kabati, mara droo, mara hili mara lile. Inafanya vigumu kweli kukusoma bila kukerwa na mashambulizi binafsi ya mtu. Uzuri wa hoja na nguvu ya hoja haiji kwa kulazimisha hivyo isipokuwa kwa kuitetea na kuonesha ukweli wake.
Hivi nikuulize mambo ya wanawake mathaln UWT mbona huulizi nani alaipia gharama zake.
Sina sababu ya kuuliza kwa sababu UWT ni jumuiya ya wanawake wa CCM. Mimi si mwana CCM na si mwanamke; lakini pia kwa sababu fedha za walipa kodi wa Tanzania kinadharia haziingii kule. Nikiwa mwana CCM nitahoji.
kwa nini usiwaambie wanawake wachukue dhamana ya matumizi ya chombo hicho badala ya taifa zima kulipa hali sisi sii wote wanawake..
Ungesema Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto hilo tutalizungumzia; lakini UWT haiendeshwi kwa fedha za serikali. Period.
Watoto Yatima, vilema, budget ya mikoa, wilaya kwa nini tunahusishwa sote wakati wengine haituhusu!.
sijui unazungumzia nini hapa. Kama UWT basi haituhusu; kama ni mambo ya serikali yanatuhusu.
.Haya ndio mawazo yako mkuu wangu unajaribu kutuvisha lakini huyo huyo Mwanakijiji inapofikia siasa huichambua CCM kama vile yeye sii mkristu anayepinga mambo mengine..
sijakuelewa.
Mkuu, unapofikiria tu kuwa waislaam ni WAO, wale, na kadhalika tayari wewe umeshaweka utengano, yaani hao wana mabaya fulani ambayo wewe hutaki kuhusishwa, hivyo hoja yako haiwezi kujenga Umoja unataka kuutangaza hapa.bali kujitenga kama unavyojitenga na Ufisadi.
wewe unaona "wakristu" na "waislamu" mimi naona Watanzania. Mambo ya Waislamu hayanihusu. Bahati mbaya wao wanayafanya ya Watanzania wote.
Wewe unajua fika kwamba Magistrate Court Act yetu ina restrict matumizi ya Islamic law ktk maswala yote ya personal matters ya waislaam ambao Kikatiba wanaruhusiwa kufanya ibada hizo.
.
sasa kama ni suala la ibada, kwani wamekatazwa na nani kuitekeleza? Hivi kuna Muislamu aliyeenda kwa Shehe na kutaka jambo lake liamuliwe kidni akakataliwa?
Sasa jiulize inakuwaje unamruhusu mtu kufanya ibada zake lakini inapofikia matatizo settlement ya dispute baina ya wahusika haifanyiki kufuata misingi ya dini..
sasa hilo ni swali la kidini siyo la serikali. Kwanini Waislamu kwa mambo ambayo yako katika dini yao hawafanyi kile dini yao inataka hususan masuala haya ya kisheria?
Toka wakoloni Tanzania tulikuwa na mahakama za kadhi, toka Mreno, Mjarumani, Muingereza na hata baada ya Uhuru sheria nyingi za kiisilaam ziliendelea kutumika ktk legal framework..
hili mbona halina utata. Lakini wakati wa Mkoloni tulikuwa na mambo mengi ambayo leo hatuendelei nayo. Sasa kama wakoloni walikuwa wanafanya basi na sisi tufanye? Hii hoja haina nguvu, kuna sheria ambazo tulizirithi toka kwa wakoloni na tumeeendelea kuzifuta kila inapobidi. Suala la Mahakama ya Kadhi liangaliwe kwa mwanga wa leo na mahitaji ya taifa zima.
ndiyo maana sina tatizo la mahakama za kadhikuwepo au sheria za Kiislamu ambazo zinatufaa Watanzania wote kuingizwa kwenye sheria zetu. Lakini sheria za kikundikimoja tu cha dini kuingizwa kwenye sheria zetu ili zifae kikundi hiko kimoja cha dini hilo nalikataa kwani zinafunza non-discrimination clause ya Katiba yetu.
Nitarudia kusema, kuwa mimi binafsi natazama nje ya box na nafanya hivyo sii kwa sababu ni Muislaam isipokuwa natazama wahusika na mustakabali wa nchi nzima kwa ujumla wake kwani binafsi sina mke zaidi ya mmoja, mirathi yangu ipo ktk will na kadhalika.
Sijui kama ni kweli unataza nje ya box. Kauli zako zimejaa mashambulizi ya kidini,kejeli za kidini na kudhalilishana kidini kwa sababu tu wewe si mtu wa dini hiyo.
Binafsi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuweka vitu vyangu kulingana na mazingira ya hapa, nchi ambayo haitambui Uislaam zaidi ya dini ya Waarabu (Axis of evil)..kwangu poa vile vile lakini sii nyumbani ambaklo tunadai ati sisi ni nchi isiyokuwa na dini wakati tunatoa maamuzi mengi kufuata mfumo wa dini moja..
nakusikia.
Kingine naelewa fika kwamba Tanzania ni Democratic secular State, imetoa ruksa kwetu sote yaani kila dini kuendesha shughuli zetu tofauti ktk maswala ndoa, Talaka, guardianship, Urithi na kadhalika lakini serikali hiyo hiyo inakataa (restrict)kutambua sheria za dini moja ktk maswala ambayo imeruhusu..Sasa jiulize kweli unawapa uhuru waislaam kuabudu au unawakaanga kwa mafuta yao wenyewe.
hili si kweli. Hivi ni muislamu gani aliyetaka mirathi yake iendeshwe kwa minajili ya dini ya kiislamu akakataliwa? Ni nani aliyetaka talaka au kutoa talaka kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu akakataliwa au talaka yake kutotambuliwa?
je, Muislamu akitoa talaka kama inavyosemwa katika Uislamu, talaka yake serikali yetu haiitambui? Kama inaitambua je siyo huko kutambua sharia za kiislamu?
.
Hii ndio point ya hao Masheikh kutaka mahakama ya kadhi na kama utatumia sabnbabu zako mkuu unazidi kujenga hoja zao vizuri kwani unaonekana wewe ni Mdini..
well inamhitaji mtu mmoja mdini kumjua mwingine.
Kinachotakiwa ni empirical and objective information.
sidhani kamahili linawezekana kwa mtindo huu wa kuongozwa na dini.