MUGABE: Mfungwa aliyekuwa Rais msomi kuliko marais wote duniani

MUGABE: Mfungwa aliyekuwa Rais msomi kuliko marais wote duniani

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Inaelezwa kuwa alikuwa ndiye Rais aliyekuwa na elimu kubwa kuwazidi Marais wote duniani alikuwa ni Rais wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe. Mugabe alizaliwa 21 February 1924 kule Kutama, Southern Rhodesia (Zimbabwe) miezi michache baada ya Southern Rhodesia kuwa koloni la Uingereza. Watu wake Kutama walikuwa wakikandamizwa na sheria mpya na hivyo hawakuwa na fursa ya kupata elimu na ajira pia.

Ingawa watu wengi kutoka Southern Rhodesia waliishia tu elimu ya msingi (grammar school), Mugabe alipata bahati ya kupata elimu nzuri. Alisoma katika shule ya Misheni ya Majesuiti (Jesuit Mission) chini ya Fr. O'Hea. Padri huyo aliweka ushawishi mkubwa katika maisha ya Mugabe mvulana mdogo.

Fr. O'Hea alimfundisha Mugabe kuwa watu wote wanatakiwa kutendewa haki katika usawa na kupata elimu ili kutimiza au kuufikia uwezo wao. Walimu wa Mugabe waliutambua uwezo wake tangu mapema na wakawa wanamuita kijana mwenye akili nyingi (a clever lad).

Mugabe alikuwa na degree 7 za kitaaluma za kutoka Fort Hare University (Afrika Kusini), University of South Africa, Unisa (Afrika Kusini) na University of London (Uingereza). Shahada sita za Mugabe alizisoma kwa njia ya posta (distance learning), kati ya shahada hizo sita, mbili alizisoma akiwa gerezani. Shahada hizo 7 ni za taaluma anuwai ikiwemo elimu, uchumi, utawala na sheria.

Katika kipindi cha miaka tisa (9), Rais Mugabe alikuwa akisoma shahada hizo wakati akiwa ni mwalimu katika shule mbalimbali za Misheni kule Southern Rhodesia. Mugabe aliendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu, University of Fort Hare nchini Afrika Kusini akahitimu katika shahada ya Historia na Kiingereza a Bachelor of Arts degree in History and English) mwaka 1951. Baada ya kuhitimu elimu hiyo, Mugabe alirejea nyumbani kufundisha. Mwaka 1953, Mugabe alihitimu Shahada ya Elimu (Bachelor of Education), aliyoisoma kwa njia ya posta.

Mwaka 1955, Mugabe alikwenda Northern Rhodesia (Zambia) na kufundisha kwa miaka minne (4) katika Chuo cha Chalimbana. Wakati huo huo akiwa anafundisha katika Chuo hicho cha Chalimbana, alikuwa akisoma kwa njia ya posta katika Chuo Kikuu, University of London shahada uchumi (Bachelor of Science degree in Economics, BSc. in Economics). Alimalizia shahada hiyo mwaka 1958 alipohamia Ghana.

SHAHADA ZA KITAALUMA ZA MUGABE:

1. Bachelor of Arts (History and English) (BA) degree ya University of Fort Hare (1951)

2. Bachelor of Administration (B.Admin) kutoka University of South Africa (Unisa)

3..Bachelor of Education (B.Ed) ya University of South Africa (Unisa)

4. Bachelor of Science (BSc.) in Economics ya University of London (External Programme)

5. Bachelor of Laws (LLB) kutoka University of London (External Programme)

6. Master of Laws (LL.M) ya University of London (External Programme)

7. Master of Science (MSc.) in Economics ya University of London (External Programme)

Shahada mbili za sheria alisoma wakati akiwa gerezani kati ya mwaka 1964 na 1975 wakati Shahada ya Uzamili katika Uchumi (MSc in Economics) alipata wakati akiwa Rais baada ya Uhuru wa Zimbabwe.

SHAHADA ZA HESHIMA ALIZONYANG'ANYWA (REVOKED HONORARY DEGREES):

1. Honorary LLD degree aliyopewa na Chuo Kikuu, University of Edinburgh (1994), ambayo alinyang'anywa mnamo Juni 2007.

2. Honorary LLD degree kutoka University of Massachusetts (1986), aliyonyang'anywa pia mnamo Juni 2008.

3. Honorary LLD degree kutoka Chuo Kikuu, Michigan State University (1990), ambayo pia alinyang'anywa tarehe 12 Septemba 2008.

SHAHADA ZA HESHIMA ALIZOBAKIA NAZO (HONORARY DEGREES):

1.Honorary LLD degree kutoka Ahmadou Bello University (Nigeria)

2. Honorary LLD degree ya Morehouse College (Atlanta, Georgia)

3. Honorary LLD degree kutoa Chuo Kikuu, University of Zimbabwe

4. Honorary LLD degree kutoka St. Augustine's University (Tanzania)

5. Honorary LLD degree ya kutoka Lomonosov Moscow State University (Russia)

6. Honorary LLD degree ya Solusi University (Zimbabwe)

7. Honorary D.Litt. degree ya Africa University (Zimbabwe)

8. Honorary D.Civil Laws degree ya University of Mauritius (Mauritius)

9. Honorary D.Com. degree ya kutoka For Hare University (Afrika Kusini)

10. Honorary D.Tech. degree ya kutoka National University of Science and Technology (Zimbabwe)

11. Honorary D.Phil (African Heritage and Philosophy) degree kutoka Great Zimbabwe University (Zimbabwe)

Kwa hiyo, hadi wakati anafariki dunia, Mugabe alikuwa na shahada 18 za Chuo Kikuu baada ya kupokwa au kunyang'anywa shahada tatu (3). Kama asingepokwa hizo tatu, basi angekuwa na shahada 21.

Andiko hili nimeandika baada ya kusoma pia kutafsiri andiko la Kazeem A. Badaru ambaye pia alirejea taarifa za FactsUniversity.com.

Credit: Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
1759992314587.jpg
 
Back
Top Bottom