Mugalu, Kagere na Thadeo Lwanga hawajam-impress kocha Zoran

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Tetesi zinasema mastraika wa kigeni wawili, Maddie Kagere na Chris Mugalu, pia kiungo Thadeo Lwanga hawajam-impress kocha zoran na kutanabaisha kabisa kuwa hawako kwenye mipango yake msimu huu na hivyo kuwaambia viongozi wao wamalizane nao haraka sana!

Pia taarifa zaidi zinasema , hata miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa, Kuna mmoja Hana viwango huku amenunuliwa kwa mpunga mrefu!

Viongozi wetu wa Simba sports club kama tutahitaji kufikia malengo, Basi msikilizen kocha anavyotaka, sio tung'ang'ane na mafikirio yetu , mwisho wa siku tumfukuze kimazoea.

My take: Ni muhimu kabla hatujaanza kusajili tumshirikishe kocha, kocha aweke majina ya watu ambao anauhakika na uwezo wao kulingana na mfumo wake.

Kumbe ni tetesi, basi ngoja tusubiri tuone.
 
Hii kitu haija kaa sawa unaenda na wachezaji preseason baadae una waacha as if walikua wachezaji wa majaribio kwani report ya coach aliepita si ingetumika kama reference
Shida Ni mifumo ya makocha, ndo maana tunashauri, kabla ya mchezaji tafuta kocha kwanza, then mwambie Nina moja mbili tatu, yeye atatoa majina ya wachezaji anaowahitaji kulingana na mfumo wake
 
Shida Ni mifumo ya makocha, ndo maana tunashauri, kabla ya mchezaji tafuta kocha kwanza, then mwambie Nina moja mbili tatu, yeye atatoa majina ya wachezaji anaowahitaji kulingana na mfumo wake
Hii ilishawahi tolewa ufafanuzi, kocha mwingne anachukua wachezaji wake km connection ya ulaji, kumbuka mchezaji ni mali ya team sio kocha.
 
Sasa nan Okrah? Mmmh hapanaa, labda kiyombo au Akpan.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tanzania tuna Cha kujifunza, tuwaige league za Europe itatusaidia,, itaokoa hasara
 
Hii ilishawahi tolewa ufafanuzi, kocha mwingne anachukua wachezaji wake km connection ya ulaji, kumbuka mchezaji ni mali ya team sio kocha.
Daah ngoja tuone, si unaona soko lilivyogumu kwa wakati huu? Na mwamba kawakomalia anataka straika mpya
 
Daah ngoja tuone, si unaona soko lilivyogumu kwa wakati huu? Na mwamba kawakomalia anataka straika mpya
Okwaa na Manzoki wakitua hapo basi case kwishaaa, tatizo simba inaona aibu kuwaacha wachezaji eti kisa walitusaidia, sio kuhusu pesa,

Mfano match tuliyofungwa 2, kocha akasema ni kukosekana kwa kiungo mkabaji box to box mildfrider, ndo wakaamua waanze kumrejesha Kanoute, ila wao walitaka wamuuze, wakamuweka kwan pending, naamini watajua Kanoute ana umuhimu wake, maana wana mu underate sana.
 
Kuna wakati viongozi wa simba nao wanajichanganya. Tatizo la wachezaji wa Safu ya ushambuliaji lilionekana hata kwa mtu asiyejua mpira.

Mugalu ligi inaisha hana goli hata Moja halafu majeruhi kila siku. Bado unamkumbatia unaenda naye pre- season kwa gharama kubwa.

Kagere tatizo ni umri. Moyo unataka mwili unagoma.

Lwanga tatizo lake ni majeruhi.

Kigezo cha kocha kusajili ni sawa , lakini wakati mwingine napo ni patapotea kama utakutana na kocha mpiga madili. Mfano , Nabi kamsajili chiko ushindi . Leo hii chiko Yuko wapi?

Kuna kocha fulani wa Yanga jina nalihifadhi alipewa Kazi ya kusajili lakini kilichotokea kila mtu ni shaihidi. Alienda kuwazoa hakina Kindoki (kipa), PAPAA moringa (toto ya ndama) , Surpong (Mwili jumba) , Maybin karengo na Yipe Yanga kikawa kichekesho.

Itoshe tu kusema wakati mwingine usajili ni kama kamali.kuna kupata au kuliwa.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Shida Ni mifumo ya makocha, ndo maana tunashauri, kabla ya mchezaji tafuta kocha kwanza, then mwambie Nina moja mbili tatu, yeye atatoa majina ya wachezaji anaowahitaji kulingana na mfumo wake
Muda wa kufanya hayo yote upo wapi kumbuka sasa hivi zimebaki week tatu ligi ianze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…