Kuna wakati viongozi wa simba nao wanajichanganya. Tatizo la wachezaji wa Safu ya ushambuliaji lilionekana hata kwa mtu asiyejua mpira.
Mugalu ligi inaisha hana goli hata Moja halafu majeruhi kila siku. Bado unamkumbatia unaenda naye pre- season kwa gharama kubwa.
Kagere tatizo ni umri. Moyo unataka mwili unagoma.
Lwanga tatizo lake ni majeruhi.
Kigezo cha kocha kusajili ni sawa , lakini wakati mwingine napo ni patapotea kama utakutana na kocha mpiga madili. Mfano , Nabi kamsajili chiko ushindi . Leo hii chiko Yuko wapi?
Kuna kocha fulani wa Yanga jina nalihifadhi alipewa Kazi ya kusajili lakini kilichotokea kila mtu ni shaihidi. Alienda kuwazoa hakina Kindoki (kipa), PAPAA moringa (toto ya ndama) , Surpong (Mwili jumba) , Maybin karengo na Yipe Yanga kikawa kichekesho.
Itoshe tu kusema wakati mwingine usajili ni kama kamali.kuna kupata au kuliwa.
Sent from my Infinix X612 using
JamiiForums mobile app