Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 22,719
- 40,739
Mshambuliaji wa Kimataifa na kutegemewa wa Mabingwa wa Soka Nchini Simba,Chris Mugwalu ameuzwa kwenye Club ya Wadi Degla ya Nchini Misri. Kwa mujibu wa taarifa za Mwandishi wetu aliepo Nchini Misri Mwaliute Mwambumbumbu amesema kuwa Mshambuliaji huyo Raia wa Zambia ameonekana kwenye jukwaa la VIP la timu hiyo inayoshika nafasi ya 16 kwenye Ligi Kuu Nchini humo iliyokuwa ikicheza match ya ligi zidi ya club ya Ismaily iliyomalizika usiku huu ambapo Wadi Degla wakiwa ugenini wameweza kushinda goals mbili bila na kuweza kufikisha point 28.
Duru za ndani kutoka Jijini Dar es Salaam na Nchini Morocco ilipo kambi ya Simba zinasema kuwa Mchezaji huyo Mzambia ameuzwa kwa shilingi za kitanzania 120ml na atalipwa mshahara mara mbili ya aliokuwa anaupata alipokuwa klabuni hapo. Alipopigiwa simu afisa habari wa timu hiyo Ezekiel Kamwaga alisema kuwa habari kamili atazitoa CEO wa timu hiyo hapo kesho.
Chanzo: Lembwe Blog