Mugwalu auzwa Wadi Degla ya Misri

Mugwalu auzwa Wadi Degla ya Misri

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Mshambuliaji wa Kimataifa na kutegemewa wa Mabingwa wa Soka Nchini Simba,Chris Mugwalu ameuzwa kwenye Club ya Wadi Degla ya Nchini Misri. Kwa mujibu wa taarifa za Mwandishi wetu aliepo Nchini Misri Mwaliute Mwambumbumbu amesema kuwa Mshambuliaji huyo Raia wa Zambia ameonekana kwenye jukwaa la VIP la timu hiyo inayoshika nafasi ya 16 kwenye Ligi Kuu Nchini humo iliyokuwa ikicheza match ya ligi zidi ya club ya Ismaily iliyomalizika usiku huu ambapo Wadi Degla wakiwa ugenini wameweza kushinda goals mbili bila na kuweza kufikisha point 28.

Duru za ndani kutoka Jijini Dar es Salaam na Nchini Morocco ilipo kambi ya Simba zinasema kuwa Mchezaji huyo Mzambia ameuzwa kwa shilingi za kitanzania 120ml na atalipwa mshahara mara mbili ya aliokuwa anaupata alipokuwa klabuni hapo. Alipopigiwa simu afisa habari wa timu hiyo Ezekiel Kamwaga alisema kuwa habari kamili atazitoa CEO wa timu hiyo hapo kesho.

Chanzo: Lembwe Blog
 
Nathibitisha habari hizi ni za kweli zimepenyezwa.na watu wa ndani kabisaaaa,utopoloo oyeeeee watotoooooo wadooogooo
 
Mugwalu wa Zambia kauzwa Misri na Mugalu wa Congo kauzwa utopolo!
 
Mshambuliaji wa Kimataifa na kutegemewa wa Mabingwa wa Soka Nchini Simba,Chris Mugwalu ameuzwa kwenye Club ya Wadi Degla ya Nchini Misri. Kwa mujibu wa taarifa za Mwandishi wetu aliepo Nchini Misri Mwaliute Mwambumbumbu amesema kuwa Mshambuliaji huyo Raia wa Zambia ameonekana kwenye jukwaa la VIP la timu hiyo inayoshika nafasi ya 16 kwenye Ligi Kuu Nchini humo iliyokuwa ikicheza match ya ligi zidi ya club ya Ismaily iliyomalizika usiku huu ambapo Wadi Degla wakiwa ugenini wameweza kushinda goals mbili bila na kuweza kufikisha point 28.

Duru za ndani kutoka Jijini Dar es Salaam na Nchini Morocco ilipo kambi ya Simba zinasema kuwa Mchezaji huyo Mzambia ameuzwa kwa shilingi za kitanzania 120ml na atalipwa mshahara mara mbili ya aliokuwa anaupata alipokuwa klabuni hapo. Alipopigiwa simu afisa habari wa timu hiyo Ezekiel Kamwaga alisema kuwa habari kamili atazitoa CEO wa timu hiyo hapo kesho.

Chanzo: Lembwe Blog
Kuch kuch hotae anataka kuuza wachezaji wote ili abakie na aliowasajili yeye ili aseme timu ni yake.
 
Huyo mugwalu wa zambia anavaa jezi namba ngapi pale simba?
 
Hizi blog hizi🤣 Simba hakuna mchezaji anayeitwa Mugwalu ndugu yetu Mwambumbumbu aliyepo ni Mugalu na uraia wake siyo Zambia ni Congo wewe Mwambumbumbu umesikia?
 
Kuch kuch hotae anataka kuuza wachezaji wote ili abakie na aliowasajili yeye ili aseme timu ni yake.
Kwani Hao walioondoka aliwasajili na kuwalipa mishahara nani?

Mo Dewji ndiyo kaichangamsha ligi ya bongo
 
Back
Top Bottom