Muhambwe wampa 5 Rais Samia mradi wa maji wa milioni 650, mbunge atoa kompyuta na mashine ya photocopy

Muhambwe wampa 5 Rais Samia mradi wa maji wa milioni 650, mbunge atoa kompyuta na mashine ya photocopy

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Dkt Florence George Samizi ameendelea na ziara yake ya kufanya mikutano ya hadhara kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo leo alikuwa Kata ya Misezero Kijiji cha Kumkugwa.

Wananchi wa Kumkugwa wameonyesha kufurahia mno na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mradi wa maji wa milioni 650 pamoja na upelekaji wa umeme kwenye vitongoji viwili vya kata hiyo.

Katika hatua nyingine ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia kuboresha sekta ya elimu, Mbunge Dkt. Samizi ametoa kompyuta moja na mashine ya kutoa nakala (photocopy machine) moja kwa shule ya sekondari Misezero.

Pia, Mbunge Samizi akahudhuria michezo Kata ya Bunyambo kufunga michezo kati ya timu ya Nyarubongo na Kumhama ambapo timu ya Kumhama ilibuka kidedea.

Mbunge Samizi ameendelea kuunga mkono michezo Jimboni ambapo ametoa Seti moja ya Jezi kwa timu iliyoshinda pamoja na fedha taslimu Laki mbili kwa timu ya Kumhama iliyoshinda, huku mshindi wa pili timu ya Nyarubongo ikipata kiasi cha fedha Elfu 50 pamoja na marefa wakipata Elfu 50 pia.

IMG-20230723-WA0029.jpg
IMG-20230723-WA0030.jpg
IMG-20230723-WA0031.jpg

 
Back
Top Bottom