ProcrastinatorInChief
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 13,027
- 29,556
ok sawa lets Go deeper zaidi ili unielewe...Wewe kilaza acha kupotosha na vi tafsiri vya kipumbavu
Men are the caretakers of women, as men have been provisioned by Allah over women and tasked with supporting them financially. And righteous women are devoutly obedient and, when alone, protective of what Allah has entrusted them with.1 And if you sense ill-conduct from your women, advise them ˹first˺, ˹if they persist,˺ do not share their beds, ˹but if they still persist,˺ then discipline them ˹gently˺.2 But if they change their ways, do not be unjust to them. Surely Allah is Most High, All-Great.
na natamani twende bila kutupiana matusi au kejeli uwe mjadala wa wazi kabisa..
sasa kwakuwa umetaka nionyeshe ukilaza wangu twende kwenye lingustic tuone hasa maana...
Aya tunayozungumzia ni hii.. Sura 4 aya ya 34
الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّهُ ۚ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي
الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا
kwa matamshi tungetamka hivi..
"Ar-rijālu qawwāmūna ‘alā an-nisā’i bimā faḍḍala Allāhu ba‘ḍahum ‘alā ba‘ḍin wabimā anfaqū min amwālihim. Fa-ṣ-ṣāliḥātu qānitātun ḥāfiẓātun lil-ghaybi bimā ḥafiẓa Allāh. Wa-llātī takhāfūna nushūzahunna fa-‘iẓūhunna wahjurūhunna fī al-maḍāji‘i wa-ḍribūhunna. Fa-in aṭa‘nakum falā tabghū ‘alayhinna sabīlan. Inna Allāha kāna ‘Aliyyan Kabīrā."
kwanini nimezungushia au nimeweka neno Wadribuhunna (وَاضْرِبُوهُنَّ)
kwenye maandishi mekundu? kwa sababu hapa ndo kumeleta mjadala kati yangun na wewe mpaka ukaniita kilaza haya sasa twende...
kwanza Neno "Wadribuhunna" (وَاضْرِبُوهُنَّ) linatokana na mzizi wa neno la Kiarabu "Da-Ra-Ba" (ضرب).
ukisoma kamusi ya Lughat-ul-arabiya inayoitwa Lisan al-Arab,
maana ya kwanza ni..
Mzizi (Root) D-R-B (ض ر ب)
Katika linguistics ya lugha za KiSemitic zote iwe ni kiarabu iweni kiaramu kiebrania au kibabylon mzizi unajulikana kama neno la "Multi-action".sasa Maana ya Daraba ya msingi kabisa (primary sense) ni "kukutanisha vitu viwili kwa nguvu au kwa haraka".
Japokuwa linguistics ya Kiarabu ya baadae kutokana na developments za mawazo hasi ya matumizi ya mzizi huu kwenye quranu ikaanzishwa kitu kinaitwa "Ishtiqaq" (Derivation). Maana ya neno inategemea kabisa "Harf al-Jarr" (Prepositions) zinazofuata baada ya neno hilo au muktadha wa sentensi.
sijui kama unanielewa?
sasa twende kwenye Maana za Kilinguistics (Bila Dini) maana ya Halisi ya awali au Primary meaning maana yake ni Action of Impact (Kugongana au Kugonga kwa nguvu) Hii ndiyo maana ya kwanza. Kupiga ngoma, kupiga muhuri, au kupiga sarafu (Daraba al-‘umla). Hapa linguistics inatazama kitendo cha "impact" kati ya vitu viwili.
tuache hapa ngoja nikufundishe kitu..
Katika elimu ya lugha arabic linguistics, kuna kitu kinaitwa Haqiqah (maana ya asili) na Majaz (maana ya mfano/fumbo).
Maana ya kwanza kabisa inayokuja akilini mwa mzungumzaji wa Kiarabu anaposikia mzizi wa neno D-R-B (ضرب) ni Physical Impact. Kama vile neno "Piga" la Kiswahili; ingawa linaweza kumaanisha "piga simu" au "piga pasi," maana yake ya msingi (default meaning) ni kutoa kipigo.
Ikiwa msemaji angetaka kumaanisha "kupiga kusikoumiza" angetumia maneno ya wazi zaidi kama Wadharban Ghayra Mubarrih yaani Kupiga kusikoumia, kusikoacha alama, na kusikovunja mfupa. Kutumia Daraba ni ushahidi kuwa kuna kitendo cha nguvu kinacholengwa....
ngoja nikufundishe kitu kidogo na ningependa kuiweka kwa maandishi makubwa na bold ili uielewe..
kama umesoma uongozi kuna kitu kinaitwa Punishment escalation au Force escalation..
sijui kama unakijua? maana yake ni kwamba ni mfuatano wa adhabu kulingana na ukubwa wa tatizo na hii huwa naturalhaihitaji elimu kubwa..
Mfano..Mwanao kakosea mara ya kwanza utamwambia kwa mdomo karudia kosa mara ya pili utamwambia but this time utakuwa mkali kidogo ,karudia mara ya tatu lazima umuadhibu ili asirudie tena...
sasa in fact ukaingalia aya uliyotaja inafuata kanuni ya Punishment escalation au Force escalation..
kwa mwanamke kwa sababu imeanza kutaja kwanza kuwa mwanaume ndo kiongozi wa mwanamke then ikataja adhabu endapo atakosea tuaziangalie hizo adhabu...
- Waʿẓ (وعظ) yaani kuonya (kwa sheria ya escalation akiacha na akakusikia hapa unaacha huendelei kwenye hatua ya pili)
- Hajr fi al-madjaʿ yaani kuacha kulala kitanda kimoja) Yaani kama hajakuelewa kwenye hatua ya kwanza unafanya hii hatua ya pili ambayo hatua hii ni kali kuliko hatua ya kwanza
- “Daraba” yaani Kupiga hii ni hatua ya juu kabisa ya Punishment escalation hata mashuleni zilitumika hivi huko primary na shule ya msingi so kupigwa ni hatua ya juu huwezi niambia kuwa mtu ambaye hajaelewa kwa kumtenga kulala naye eti umpige na mswaki aje akuelewe..hiyo inakiuka kanuni huwezi kurudi adhabu yenye force ndogo kuliko ya nyuma..