Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya

Hv hayo madawa polisi wanayaharibu kweli?...au ndo yanarudishwa kwenye mzunguko!!
 
Uko sahihi Mkuu, hakuna kipindi ambacho Kitengo kimejitahidi kama Kwa miaka ya hivi karibuni...!
 
Hizo dawa ziko Wapi? Wakishahukumiwa mzigo wao unakua chini ya Nani? Au ndio unaozunguka mtaani?
 
Yule alishamaliza kifungo chake Marekani yupo huru, siyo huyu Chonji.

Yule Don anaitwa Skuba.
 
Duh huyu cambiasso hii ngoma ya sahvi ngumu ni kuicheza
Maana kesi nyingi alikutana nazo alizichezesha...anyway ngoja tuone

Ova
Toka maktaba :

2022 21 November
Kambi Zubery Seif, mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya kilogram 27 eneo la Kiluvya kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Dawa za Kulevya.


View: https://m.youtube.com/watch?v=JPTClkY3Ntk
SARAH MWENYE KESI ya DAWA ZA KULEVYA kilo 34.89 inayomkabili pamoja na Muharami Sultan, Cambiasso na wenzanke kadhaa AWATAJA WATOTO WAKE MAHAKAMANI - ''SIELEWI WANAISHIJE''...

View: https://m.youtube.com/watch?v=Dh02jQsSM_Y2023 16 February
SARAH MWENYE KESI ya DAWA ZA KULEVYA heroine zenye uzito wa kilo 34.89. AWATAJA WATOTO WAKE MAHAKAMANI - ''SIELEWI WANAISHIJE''...Kutoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ni kuhusu mshtakiwa Sarah Joseph anayekabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya, ameieleza Mahakama hiyo kuwa haelewi watoto wake wanaishi maisha gani huko walipo.Mshtakiwa huyo ametoa madai hayo leo baada ya Wakili wa Serikali Caroline Matemu kuieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio kuwa upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea, hivyo wanaomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mrio baada ya mahakama kuelezwa hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 2, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na kesi inayowakabili haina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Mbali ya Sarah pia katika kesi hiyo kuna washtakiwa wengine watano akiwemo aliyekuwa kocha wa Makipa wa Timu ya Simba, Muharami Sultan(40), ambapo kusafirisha dawa za Kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 34.89.
 
Atayajua wapi haya huyo boya..mtu akiishavaa shati la kijani anajiona eti Na yeye ni mtu wa systems😀😀😀😀
Sasa hivi ukienda huko visiwani wavuvi wanavua samaki kwa njia haramu na hatarishi sana, yaani ni mwendo wa mabaruti tu na hakuna anayejali wala kufuatilia.

Bangi na mirungi jamaa zangu wanavusha tu kwenda Kenya kupitia Sirali na hawana wasi wasi wowote.... bila kusahau wazee wa kupanga magogo barabarani kwenye mipaka ya burundi.

Halafu leo hii eti kuna mlamba asali mmoja akiwa na kilaki mbili chake mfukoni alichokipata kwa njia ya rushwa, anakuja kuanza kumsifia sifia Samia kwamba anadhibiti bishara za haramu huku akipondea awamu zilizopita...!?? Shenzy zake
 
K
Kwan samia ndiyo ametoa hukumu
Mpumbavu wewe
Hata ukinya utasema asante samia

Mijitu mijinga kama wewe unafikir raisi ndiyo anafanya kila kitu
 
Kazi ya kamishna wa kwanza Rogers Sianga.
 
K

Kwan samia ndiyo ametoa hukumu
Mpumbavu wewe
Hata ukinya utasema asante samia

Mijitu mijinga kama wewe unafikir raisi ndiyo anafanya kila kitu
Mkuu unanitukana bure tu. Kwa Tanzania hii hata leo Dr Samia akiamua Chonji atolewe anatoka na huna la kufanya na hakuna atakayekohoa.

Tuendelee kupambania katiba bora inayowajibisha watu bila Rais kulazimika kutia mkono wake.

Bado tuna shukuru utashi wa Dr Samia kuamua magwiji hao wakamatwe.
 
Kaka unanisakama bure tu mimi sina hata huo uchawa na wala asali ya ccm sijawahi na siitaki.
Jambo moja unalosahau kujua ni kwamba kwa Katiba Yetu Tanzania bila Rais kutaka hakuna kitu chochote kinawezekana.

Si umemsikia Nape Nauye? Je Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina nguvu yoyote juu ya kina Nape?
 
Haaa nimekuelewa sasa, ila comment yako ya awali ilikuwa imekaa kichawa zaidi na kilamba asali.... maana walamba asali wanachojua wao ni kutoa sifa za uongo kwa mama yao huku wakipondea awamu iliyopita...

Kuhusu akina Nape Nnauye kuwa na nguvu kuliko tume pamoja na Samia mwenyewe hilo liko wazi wala sio la kushangaza na ndio maana mimi nawachukia sana machawa sababu wanaowakingia kifua ndio wanufaika wakuu wao wanarushiwa mifupa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…