NgerukeAbra
JF-Expert Member
- Sep 5, 2022
- 1,336
- 2,008
Naikumbuka vizuri siku hiyo kabla ya kukamatwa chonji alirushiana risasi na askari.HIi kesi ya zamani kweli, haki imetendeka.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naikumbuka vizuri siku hiyo kabla ya kukamatwa chonji alirushiana risasi na askari.HIi kesi ya zamani kweli, haki imetendeka.
Ni kweli. Ila wakitaka kujua huwa hawasubiri polisi itangaze. Mtu kama anataka kufanya hii shughuli anaulizia ''mazingira'' kwa washikaji wa vijiweni huko, na siyo polisi.Wapo ambao hawajui thamani.
Chonji ni maarufu kwenye hiyo biashara ya ngada,kituo cha polisi magomeni alikuwa mfadhili wao.Wamekamatwa wa 5 ila Chonji ndio yupo kwenye headline itakuwa ni maarufu huyu
Ila maisha jela kisa kuuza hiyo kitu haija kaa sawa ukizingatia watumiaji hawashikiwi bundukiChonji ni maarufu kwenye hiyo biashara ya ngada,kituo cha polisi magomeni alikuwa mfadhili wao.
Duh! Sasa kwa nini polisi wasitengeneze mazimgira ya kumuua tuu kama walivyofanya kwa yule don wa colombiaNaikumbuka vizuri siku hiyo kabla ya kukamatwa chonji alirushiana risasi na askari.
Kuna jamaa anadai jamaa wanaishi kama wako uraiani! Wanapata kila kitu! Simu, misosi ya maana, mpaka mademu!Wa Adiddas naona ana chekea tumboni akifikiria msala ulio wakuta 😄
Si unaona walivyo na vitambi kwenye picha hapo wanang'aaKuna jamaa anadai jamaa wanaishi kama wako uraiani! Wanapata kila kitu! Simu, misosi ya maana, mpaka mademu!
Kama kina Escobar!
Hatari sana hawa watu!
Huyo Chonji anakaa magomeni Kagera nyuma ya kituo cha mafuta cha oil com,mtaa wa magomeni kondoa kama sijakosea hapo ana miliki ghorofa na hapo ndipo alipotupiana risasi na askari.Duh! Sasa kwa nini polisi wasitengeneze mazimgira ya kumuua tuu kama walivyofanya kwa yule don wa colombia
Mie ningekuwa mkuu wa hiyo idara yaani ningesema kabis ahapa sitaki kesi nataka a dead body tena especially mtu ambaye tunajua kabisa anatembea na bunduki
Au wao wana soko na hayo madawa ndio wanatoa thamani huko...huwa nawashangaa sana kutoa taarifa kwa kuiga Nchi zingine bila wao kufanya tafiti..Wajinga sana, thamani ya Nini?
Nenda maeneo ya magomeni Kagera nyuma ya kituo cha mafuta cha oil com kaulize habari zake wakazi wa hapo watakupa historia yake yote.Lakini, Je, ni KWELI kwamba Watu hao wamekamatwa na hayo madawa ya kulevya au wamebambikiwa tu hayo madawa ya kulevya???
Endapo Kama ni kweli kiuhalisia Watu hao wanahusika na hayo madawa ya kulevya basi haki imetendeka, lakini kama wamebambikiwa na 'Watesi wao' basi Mungu awaongoze vyema ili waangalie namna ya kuweza kujinasua na dhahama hiyo, ikiwezekana wakate Rufaa na Mungu asaidie ili Rufaa yao ishinde.
Aliekamatwa na wamarekani Beka Rangers,tena walienda kumkamatia Mauritius kama sijasahau akapelekwa Marekan nahisi kesi yake iliishaChonji si ndo yule aliyekamatwa na wa marekani? Akapelekwa mtwara akatoroka wakamkamata tena au ni yupi? Kama ni yeye umrinwake ni mkubwa sana na hiyo miaka sijui kama atakaa mingi atajifia zake gerezani tu.
Yule wa underground ya hapo magomeni yeye alitoka au vipi?
Halafu Wagalatia wanakuambia samia anacheka na drugs dealer, haya hao wamekula kifungo cha maisha
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa watano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya aina za heroini gramu 5,309.57 na kokeni zenye uzito wa gramu 894.28.
Hukumu imetolewa Julai 11, 2024 na Jaji Awamu Mbagwa, aliyesikiliza kesi hiyo ya jinai namba 58/2023.
Waliohukumiwa ni Muharami Abdallah, maarufu Chonji, Abdul Chumbi, Rehan Umande, Tanaka Mwakasafule na Maliki Maunda.
Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, Jaji Mbagwa aliwahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa wote watano akieleza upande wa mashitaka umethibitisha makosa hayo bila kuacha shaka yoyote.
Washtakiwa walidaiwa kusafirisha dawa za kulevya kinyume cha kifungu cha 16 (1) (b) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
Katika shitaka la kwanza, walidaiwa Oktoba 21, 2014 eneo la Magomeni Makanya, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroini ambazo iwapo zingeuzwa zingekusanya Sh265.47 milioni.
Shtaka la pili, walidaiwa siku hiyohiyo na katika eneo hilo, walisafirisha dawa za kulevya aina ya kokeni za Sh62.59 milioni.
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliwakilishwa na mawakili watano wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Saraji Iboru, huku washtakiwa wakitetewa na mawakili wanane wakiongozwa na Juma Nassoro.
Upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi 10 na vielelezo 12, ikiwamo mizani tatu za kupimia, bastola aina ya Browing iliyokuwa na risasi nane, ripoti ya mkemia, simu, cheti cha kukamata na ripoti ya kitaalamu ya taarifa ya uchunguzi na uthibitisho wa picha mjongeo (video).
Chonji huyo mrefu zaidi, ana 55yrsmrangi njoo mkuu, Chonji ndio huyo nyuma kabla ya askari?
M niltaka wanyongwe kabisaaa wametesa vijana wengi sana ba madawa yaoioi