Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya

Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya

Ifike wakati wasitangaze thamani ya hayo madawa ya kulevya kama Serikali inapinga matumizi ya hii kitu hizi thamani wao wamezipata wapi wataje uzito na aina inatosha kutaja taja thamani kunachochea ongezeko la hiyo biashara haramu..
Kisheria thamani ya madawa lazima itangazwe ili kukazia HUKUMU. Huyo chonji alikua anatom.bah lishangazi flan amazing hivi daah. Sijui like lishangazi Lina Hali gani sasa hivi
 
Kwa hiyo kwa akili yako unaona hii serikali ya samia ndio ina umadhubuti wa kupambana na vita ya madawa ya kulevya??

Kwamba kukamata hao akina choji ambao hata sio main supplier ndio kunakufanya uwe excited namna hii kiasi cha kubwabwaja maneno ya mipasho kama kimama cha uswahilini chenye asili ya kizanzibari?

Wewe nakuona umevimbiwa asali na haujui kinachoendelea, na kwa taarifa yako tu ni kwamba hakuna kipindi ambacho biashara haramu zinafanyika sana tena kwa uwazi kama awamu hii... weka hilo akilini.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Tetesi huyo aliefungwa US amesha achiwa... Kule walimpeleka kupumzika tu.. Waka freeze assets zake bhas... A very humble and family man... Ila kwa matukio sasa.....
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mbona kama anaonekana siyo humble[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] alivyokamatwa aliwaambia polisi kuwa wanajisumbua tu yeye at
Atachiwa tu
 
Magomeni siku hizi imepoa sana...! Vijana wa enzi hizo wa magomeni walikuwa na ndoto kubwa...na wengi walienda nje bila kuwa na passport [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Walitumia njia ngumu sana kwakweli wanahitaji pongezi...! Vijana mlio Baki wa magomeni mmeingiwa na uoga...!​
Kweli hata Kuna brother mmoja South Africa and hela kinoma..ni mtoto was magomeni ...na yule Rasta tiko wa magomeni naye ana bonge la mjengo magomeni
 
Beka rangers Alifungwa miaka saba Mauritius ila kamaliza,, huyu anamuongelea tiko rasta wa makanya naye alikuja kuchukuliwa na interpool bongo akafungwa marekani nafikiri ni miaka mitatu nae kamwaga
Naamini kwa vifungo hivyo vigupi itakuwa wanacooperate na mamlaka, hivi hivi hauwezi fungwa muda mfupi hivyo.
 

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa watano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya aina za heroini gramu 5,309.57 na kokeni zenye uzito wa gramu 894.28.

Hukumu imetolewa Julai 11, 2024 na Jaji Awamu Mbagwa, aliyesikiliza kesi hiyo ya jinai namba 58/2023.

Waliohukumiwa ni Muharami Abdallah, maarufu Chonji, Abdul Chumbi, Rehan Umande, Tanaka Mwakasafule na Maliki Maunda.

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, Jaji Mbagwa aliwahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa wote watano akieleza upande wa mashitaka umethibitisha makosa hayo bila kuacha shaka yoyote.

Washtakiwa walidaiwa kusafirisha dawa za kulevya kinyume cha kifungu cha 16 (1) (b) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.

Katika shitaka la kwanza, walidaiwa Oktoba 21, 2014 eneo la Magomeni Makanya, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroini ambazo iwapo zingeuzwa zingekusanya Sh265.47 milioni.

Shtaka la pili, walidaiwa siku hiyohiyo na katika eneo hilo, walisafirisha dawa za kulevya aina ya kokeni za Sh62.59 milioni.

Katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliwakilishwa na mawakili watano wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Saraji Iboru, huku washtakiwa wakitetewa na mawakili wanane wakiongozwa na Juma Nassoro.

Upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi 10 na vielelezo 12, ikiwamo mizani tatu za kupimia, bastola aina ya Browing iliyokuwa na risasi nane, ripoti ya mkemia, simu, cheti cha kukamata na ripoti ya kitaalamu ya taarifa ya uchunguzi na uthibitisho wa picha mjongeo (video).
Asee
 
Miaka hiyo, vijana wa Dar wanawaza kwenda Ulaya, vijana wa vijijini wanatamani kuja Dar! Huu mtazamo unaenda katika nyanja mbalimbali za kimaisha!

Watoto wa Magomeni, Ilala, Kinondoni na Kariakoo miaka hiyo ndiyo walikuwa DSM! Sinza walikuja baadaye sana! Weka pembeni wale wa kishua from Masaki, Osterbay na Upanga wale walikuwa next level!
Babkubwa...
Mji umejaa washamba huu wa vijijini...
Mtu anatoka kwenye tembe za tope huko maporini , ila akifika Dar anaanza kuwaponda watu wa Mbagala,.....
Wakati mzunguko wa hela Mbagala ni zadi ya Iringa au Mbeya mjini....
 
Back
Top Bottom