Nahisi tatizo lilianzishwa na wanansiasa kulinda ugali wao. Kumbuka MAT ilikuwa na nguvu huko nyuma hasa kudai stahiki zao, waliweza hata kuitisha migomo na ikafanikiwa.
Wanasiasa wakadhani madaktari wanaringa kwa sababu ya uchache wao, wakaona ili kuondoa maringo wakaamua kufanya mass production ya kozi zote, sasa Medical Field ndio wakasajiri kile chuo cha IMTU wakaanza kufyatua Madakitari, Pharmacist na kozi zingine kama maabara nadhani. Baada ya miaka kadhaa wakafungiwa. Kairuki akapewa kijiti, wakaja Kairuki, CUHAS, KCMC sasa UDOM.
Cha kushangaza sababu zilizowafanya wakawafungia IMTU hazikuangaliwa walipo toa usajili KAIRUKI, UDOM, KCMC na CUHAS. Lecturers wote walitoka MUHAS wakati huo MUCHS.
kama unavyosema course ya mwaka mzima wanapigwa semester moja. Nilikuwa naona lecturers wana safiri kama mchezo, ratiba zao MUCHS zikawa zinapungua ili kukidhi mahitaji ya mifuko yao.
Wakafanya mass production, taaluma ziko saturated sasa, maana wanansiasa walitaka number siyo quality, kwa sababu wao wanatibiwa nje ya nchi, huo ndio mtizamo wangu.
Na hakuna wa kuregulate tena, unaona waki fail mitihani ya board wanalia zinaundwa tume wanatafuta namna ya kuchakachua. Hata sijui tunaenda wapi?
Dah inaumiza sana . Na hapo wakiumwa never kutibiwa TZ . I was surprised kuona JK anatibiwa surgery ya enlarged prostate nje ya nje , a very simple surgery ambayo ilikuwa ni simple kufanyikia TZ . Ila mauti yakiwa mlangoni sana ndio utaona wanaenda HOSP zao.
Wanasiasa wameharibu taalamu ya Afya, sajili za chuo zimekuwa ni kama unasajili nyumba. Unakutana na MD unajiulizA wewe umesoma kweli au ulifaulu. It is not about huyu hana experience or not , mtu mwenye akili na aliyefaulu proper way unamuona first day the way anavyopresent cases , sio hawa wa sasa. Halaf wanapelekwa mikoani kutibu , kwenda kumaliza watu zaidi.
A medical Doctor hata ujamsikiliza mgonjwa unaanza kuandika dawa,mgojwa ana flu una towa dawa tano, makosa kama haya yanatakiwa kuboreshwa na famasia, famasia mwenyewe ni wa IMTU, UDOM , KAMPALA kazi yake kubwa ni mbili mara tatu.
Koz za Afya miaka ya ile tunachuo cha MUHIMBILI chini ya UDSM zilikuwa na heshima na ukiona mtu anasoma hizo course amefaulu vema .
Now days tunapigania eti Doctor , famasia na nurse , mtu mwenye F ya hesabu aweze kusoma hizo . Yaani nimestuka sana tunapoelekea na hii ni failure system ya nchi nzima
Dhambi kubwa Wizara Sensitive kama ya Afya anaenda kupewa mtu wa Socialogy ambae kila kitu kinaenda kisiasa.
Hatuna Nurses anaeweza kuwa Waziri wa Afya ? Hatuna Famasia anaeweza kuwa Waziri wa Afya , Hatuna MD Anaeweza kuwa Waziri wa Afya ? Hatuna Lab scientists anaeweza kuwa Waziri wa Afya ? ili tuweze kuongea lugha moja tukiwa tuna present mada kama hizi.
Sio kutuwekea mtu wa sociology kuongoza Wizara ya Afya . Ukiuliza unaambiwa pale hafanyi Afya , …… but no! It matters a lot kuwa na mtu wa Afya yoyote yule awe lab au nurse Dr au Pharm .
Tunaona kazi nzuri ya Dorothy , kama kawaida waliona Ngosha alikosea kumpa uwaziri, but she was the best kuliko hiki kinachoendelea Wizara ya Afya , ujanja ujanja na upigaji, Universe Coverage imewashinda, KITITA cha NHIF ni siasa. Muhasibu ndio anaenda kuwa CEO wa NHIF
.Hosp ya MNH inafanya vema sababu ipo chini ya Doctor , JKCI inafanya vema sababu ipo chini ya Doctor , TMDA inafanya vema sababu ipo chini ya Famasia na CEO ni famasia, BOHARI KUU YA DAWA inafanya vema sababu ipo chini ya Famasia na hili libohari lilifanya vibaya sana baada ya kuwapa wanajeshi na watu wa sociology, NHIF inatakiwa kuwa chini ya Mtaalam mostly Famasia ndio wanaelewa mifumo ya dawa , tukikosa hata sis mtupe.
Taasisi zote za Afya ziwe chini ya wataalam , Mpaka wizara ya Afya, kama ni ishu ya management, wapelekwe kujifunza management , shida nini ?
Huku vyuoni Nacte, TCU kote, course za Afya zitolewe maamuzi na watu wa Afya , sio kushauri watu wa F D wakasomee hizo course
Shame Sociology na tunaenda kuangamiza nchi