MUHAS na CUHAS ndio vyuo bora pekee vya Afya Tanzania

Wenye taaluma have to market themselves period!
Setting ichange for them, instead of waiting for things to change for them
 
Nahisi tatizo lilianzishwa na wanansiasa kulinda ugali wao. Kumbuka MAT ilikuwa na nguvu huko nyuma hasa kudai stahiki zao, waliweza hata kuitisha migomo na ikafanikiwa.

Wanasiasa wakadhani madaktari wanaringa kwa sababu ya uchache wao, wakaona ili kuondoa maringo wakaamua kufanya mass production ya kozi zote, sasa Medical Field ndio wakasajiri kile chuo cha IMTU wakaanza kufyatua Madakitari, Pharmacist na kozi zingine kama maabara nadhani. Baada ya miaka kadhaa wakafungiwa. Kairuki akapewa kijiti, wakaja Kairuki, CUHAS, KCMC sasa UDOM.

Cha kushangaza sababu zilizowafanya wakawafungia IMTU hazikuangaliwa walipo toa usajili KAIRUKI, UDOM, KCMC na CUHAS. Lecturers wote walitoka MUHAS wakati huo MUCHS.

kama unavyosema course ya mwaka mzima wanapigwa semester moja. Nilikuwa naona lecturers wana safiri kama mchezo, ratiba zao MUCHS zikawa zinapungua ili kukidhi mahitaji ya mifuko yao.

Wakafanya mass production, taaluma ziko saturated sasa, maana wanansiasa walitaka number siyo quality, kwa sababu wao wanatibiwa nje ya nchi, huo ndio mtizamo wangu.

Na hakuna wa kuregulate tena, unaona waki fail mitihani ya board wanalia zinaundwa tume wanatafuta namna ya kuchakachua. Hata sijui tunaenda wapi?
 

Dah inaumiza sana . Na hapo wakiumwa never kutibiwa TZ . I was surprised kuona JK anatibiwa surgery ya enlarged prostate nje ya nje , a very simple surgery ambayo ilikuwa ni simple kufanyikia TZ . Ila mauti yakiwa mlangoni sana ndio utaona wanaenda HOSP zao.

Wanasiasa wameharibu taalamu ya Afya, sajili za chuo zimekuwa ni kama unasajili nyumba. Unakutana na MD unajiulizA wewe umesoma kweli au ulifaulu. It is not about huyu hana experience or not , mtu mwenye akili na aliyefaulu proper way unamuona first day the way anavyopresent cases , sio hawa wa sasa. Halaf wanapelekwa mikoani kutibu , kwenda kumaliza watu zaidi.

A medical Doctor hata ujamsikiliza mgonjwa unaanza kuandika dawa,mgojwa ana flu una towa dawa tano, makosa kama haya yanatakiwa kuboreshwa na famasia, famasia mwenyewe ni wa IMTU, UDOM , KAMPALA kazi yake kubwa ni mbili mara tatu.

Koz za Afya miaka ya ile tunachuo cha MUHIMBILI chini ya UDSM zilikuwa na heshima na ukiona mtu anasoma hizo course amefaulu vema .

Now days tunapigania eti Doctor , famasia na nurse , mtu mwenye F ya hesabu aweze kusoma hizo . Yaani nimestuka sana tunapoelekea na hii ni failure system ya nchi nzima

Dhambi kubwa Wizara Sensitive kama ya Afya anaenda kupewa mtu wa Socialogy ambae kila kitu kinaenda kisiasa.

Hatuna Nurses anaeweza kuwa Waziri wa Afya ? Hatuna Famasia anaeweza kuwa Waziri wa Afya , Hatuna MD Anaeweza kuwa Waziri wa Afya ? Hatuna Lab scientists anaeweza kuwa Waziri wa Afya ? ili tuweze kuongea lugha moja tukiwa tuna present mada kama hizi.

Sio kutuwekea mtu wa sociology kuongoza Wizara ya Afya . Ukiuliza unaambiwa pale hafanyi Afya , …… but no! It matters a lot kuwa na mtu wa Afya yoyote yule awe lab au nurse Dr au Pharm .

Tunaona kazi nzuri ya Dorothy , kama kawaida waliona Ngosha alikosea kumpa uwaziri, but she was the best kuliko hiki kinachoendelea Wizara ya Afya , ujanja ujanja na upigaji, Universe Coverage imewashinda, KITITA cha NHIF ni siasa. Muhasibu ndio anaenda kuwa CEO wa NHIF

.Hosp ya MNH inafanya vema sababu ipo chini ya Doctor , JKCI inafanya vema sababu ipo chini ya Doctor , TMDA inafanya vema sababu ipo chini ya Famasia na CEO ni famasia, BOHARI KUU YA DAWA inafanya vema sababu ipo chini ya Famasia na hili libohari lilifanya vibaya sana baada ya kuwapa wanajeshi na watu wa sociology, NHIF inatakiwa kuwa chini ya Mtaalam mostly Famasia ndio wanaelewa mifumo ya dawa , tukikosa hata sis mtupe.

Taasisi zote za Afya ziwe chini ya wataalam , Mpaka wizara ya Afya, kama ni ishu ya management, wapelekwe kujifunza management , shida nini ?

Huku vyuoni Nacte, TCU kote, course za Afya zitolewe maamuzi na watu wa Afya , sio kushauri watu wa F D wakasomee hizo course
Shame Sociology na tunaenda kuangamiza nchi
 
Bad news is elimu imejaa siasa.... mawazo mazuri kama haya huwa hawawezi kuyakubali....
Sababu hata watunga sheria ni KKK unategemea wataona umuhimu wa elimu bora????
 
Nchi ishaangamia buda... tunaenda kumalizia malizia kuangamiza
 
Kweli asee kuna mwana tulinaliza nae advance yeye akwenda chuo aliajiriwa na CRDB 2005 na advance alipata CES ,sasa wakati na fundisha chuo cha IAA darasani mwamba huyu hapa ,tukacheka sana baada ya pindi ,chakushangaza anawakimbiza madogo fresh from school na wana div one nzuri kabisa .
 
Bad news is elimu imejaa siasa.... mawazo mazuri kama haya huwa hawawezi kuyakubali....
Sababu hata watunga sheria ni KKK unategemea wataona umuhimu wa elimu bora????

Huzuni sana
 
Siasa, siasa yani inatumaliza..
 

Chuo gani?
 

Naomba kujua hapo Ocean road ulikaa miaka mingapi
na kila mwaka mlikuwa mnapokea wanafunzi wangapi wa Intern kwa kila kozi au hata kwa ujumla?
Na kwa namna gani wewe uliweza kuhusika/kuwafundisha wanafunzi wa kozi zote za fani tofauti tofauti za Afya

Nahitaji tu kujua kama utafiti wako unatosha kuujengea hoja au ni zile mada za blaa blaa ambazo hazifuati taaluma (research ethics)
Inaonekana umekuja hapa kupiga propaganda za chuo flani kiana kwa kutumia data zako FEKI!
 
nilitaka nipite tu lakini kuhusisha topic hii na CCM kwa maelezo kana kwamba imefeli sikweli, wewe ni mtoto mdogo sana hujui tulikotoka tulikuwa tunapewa aspirin kutibu magonjwa yote tulikotoka Nchi hii ni mbali sana mpaka tumefikia utalii wa tiba yaani watu wanatoka Nchi zao wanakuja kutibiwa Tanzania na wanaondoka wamepona, wewe una matatizo. ni wazi Muhas ni chuo kikongwe kwa hapa Nchini kikianzia kama kitivo cha udsm lakini huwezi kubeza mchango mkubwa wa vyuo vingine.
 
Unaongelea pass marks? Hawawezi kuweka vigezo vya juu kwa vile kazi hizo hazina pesa kwa bongo.
 
Wapo wengi
Mfumo wa Afya unatuangusha

Kuna yule docta anauliza tell me your family has the history of falling from the tree?

Mambo ya hovyo sana

Kwanza Tanzania hatutumii kiingereza
Hivyo kitendo cha kuamini huo utani na kuufanya kuwa ni kweli, inaonesha kabisa kuna kitu hakipo sawa!!!
 

[emoji1787]nijue kwanza ulisoma chuo gani, upo subjective sana
 

[emoji1787]
 
Wrwe
Bugando hakuna kitu wanaweza kuwa wanazidiwa hata na IMTU. Hao ni km wale wanaosoma Ukrain

Ulipotaja CUHAS tu nikajua hujui unachokiongea. Miongoni mwa vyuo vina products zenye ubora mdogo ni CUHAS . At least KCMC inapokuja kwenye kazi za mikono na practical wanatoa Madaktari wazuri sio CUHAS
Wewe utakuwa ni product ya KCMC sio bure, mimi sio MD ila ni Lab Scientist nadeclare hili kwa namna ninavyokutana na Intern wa baadhi ya Vyuo na wale wanaokuja mazoezi kwa Vyuo baadhi hasa hivi vifuatavyo MUHAS, CUHAS& KCMC wengi hasa KCMC mtu third year hajui kabisa kuoperate microscope tu, Mtu Urine hajui anachukua wapi apime!!

Japo nakiri wapo wachache wanajua!!
 
muhas najua ni muhimbili na cuhas ni chuo kipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…