Muhimbili: Familia yaomba Serikali iisamehe deni la Tsh 10m ili wapate mwili wa ndugu yao mochwari. Profesa Janabi atoa utaratibu wa kuchukua mwili

Muhimbili: Familia yaomba Serikali iisamehe deni la Tsh 10m ili wapate mwili wa ndugu yao mochwari. Profesa Janabi atoa utaratibu wa kuchukua mwili

Hiyo tuliambiwa ni oxygen tu ile hapo bado madawa na ndo mana unaona bili zinakuja kubwa milions of money

Inabidi kuhoji haya mambo. Ipo hatari kubwa ya kuuziana mbuzi kwenye magunia.

Hospitali nyingi za umma zina mitambo ya umma ya kuzalisha hizi oxygen.

IMG_20230215_122840.jpg

Bei hIzi kwenye hospitali za umma hazikubaliki. Labda kama ni mpango tu wa kuwafilisi watu na mifuko ya bima.
 
GHARAMA ZA MATIBABU ZINAZODI KUPAA NI KUBWA MNO.

NCHI HII INAUMIZA SANA

Masikini Tanzania Yangu.
 
Inabidi kuhoji haya mambo. Ipo hatari kubwa ya kuuziana mbuzi kwenye magunia.

Hospitali nyingi za umma zina mitambo ya umma ya kuzalisha hizi oxygen.

View attachment 2518291

Bei hIzi kwenye hospitali za umma hazikubaliki. Labda kama ni mpango tu wa kuwafilisi watu na mifuko ya bima.
Hapo sasa wahusika ndo waingilie kati sie tubaki wapenzi watazamaji
Ila ujue tu siku ukizidiwa ikibidi uingie ICU gharama ndo hizo kama huna nduguzo watauza hata nyumba yako walipe deni ukitoka hospital unaanza upya mana huo.msamaha hauwahusu below 65
 
Ujinga wetu ndiyo unaoyaruhusu haya kuota mizizi. Haupo mfuko wa bima ambao hautafilisika na hakuna watu watakaoweza kulipia gharama hewa hizi.

Haya mambo si ya kuchukulia poa. Mpango mzima ni kuhakikisha watu wanafilisika kwa namna yoyote Ile.
 
Hospitali acheni kuchonganisha Serikali na raia. Amri ilishatolewa maiti isizuiliwe kisa deni

Familia ya Marehemu Swalehe Mshale (74) wa Mbagala Majimatitu, imeiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa Mpendwa wao mochwari toka alipofariki February 10 mwaka huu.

---
Familia ya Marehemu Swalehe Mshale (74) wa Mbagala Majimatitu A Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam, imeiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa mpendwa wao mochwari.

Mzee Swalehe alifariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Februari 10 2023 wakati akipatiwa matibabu kutokana na utumbo wake kutoboka na hadi sasa ni siku ya tano wameshindwa kuuchukua mwili wake kwa ajili ya mazishi kutokana na deni wanalodaiwa la milioni Kumi ambapo wanasema wameambiwa watoe asilimia 75 ya deni ndipo wapewe mwili wa Mpendwa wao.

"Tulikuwa na Mgonjwa Muhimbili Hospitali alilazwa Kibasila wodi namba 11 akahamishiwa Mwaisela ICU namba 2 kwa ajili ya matibabu zaidi kwa sababu hali yake haikuwa nzuri hadi Februari 10, akafariki ambapo nikaambiwa nikafunge bili, nikakuta nadaiwa milioni kumi na laki sita lakini kutokana na hali yangu ngumu ya kiuchumi nikaambiwa nifate process ili tupate msamahama ambapo tuliandikiwa barua na Serikali ya Mtaa tukaenda hadi Muhimbili Ustawi wa Jamii ndipo tukaambiwa tulipe asilimia 75 ya pesa sawa na milioni nane".

"Uwezo wetu ni mdogo sana, kama Serikali inaweza kutupa mwili wetu tutashukuru sana lakini kama haiwezekani basi itabidi sisi tuache tuangalie taratibu nyingine maana hadi sasa tumefanikiwa kukusanya shilingi milioni moja tu," Tunaendelea kuutafuta Uongozi wa Hospitali ya Muhimbili ili kusikia kutoka upande wao.

----

Profesa Janabi atoa mwongozo wa kufuata ili kuchua mwili

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohammed Janabi ameitaka familia ya marehemu Swalehe Mshale (74) kufika katika uongozi wa hospitali hiyo ili kukamilisha taratibu za kupatiwa mwili wa mpendwa wao.

Tamko hilo ni kufuatia familia ya marehemu kuiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na hospitali ya Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa mpendwa wao toka alipofariki Februari 10, mwaka huu.

“Utaratibu upo very clear ni kurudi hapo kwa watu wa social (Ustawi) kuna barua ambayo wanatakiwa kuandika ya ‘commitment’ wataacha ID (kitambulisho) wataruhusiwa kuchukua mwili halafu baada ya hapo watakuwa na makubaliano kama ni miezi sita, kama ni mwaka kila mtu anaji-commit kivyake kwamba atakuwa analipa kidogokidogo, hivyo wakamuone Mkurugenzi wa Uuguzi,” amesema Prof. Janabi.

Ameongeza, “tatizo ni kwamba watu wa namna hii hawafuati taratibu wanazotakiwa kuzifuata, badala yake wanakimbilia kwenye jamii wakitarajia tutapata pressure, ‘we don’t get pressure’, hizi hela ni za Serikali.”
 
Huyo Samia amepeleka fedha za uendeshaji pale muhimbili?Wakiwa jukwaani wanasema nyeusi kwenye utendaji 0
 
Huyo Samia amepeleka fedha za uendeshaji pale muhimbili?Wakiwa jukwaani wanasema nyeusi kwenye utendaji 0
Sisi tunajuaje? Kama kinachesemwa hakiwezekani si waieleze serikali kwamba hilo agizo halitekelezeki
 
Familia ya Marehemu Swalehe Mshale (74) wa Mbagala Majimatitu, imeiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa Mpendwa wao mochwari toka alipofariki February 10 mwaka huu

Pole kwa familia,ila dawa ya deni ni kulipa,taasisi zinahitaji fedha kujiendesha cha bure salamu tu.
 
Nchi inaendeshwa kisheria na sio matamko ya kisiasa. Tamko la waziri sio sheria.
 
Unapewa bili kubwa ukichungulia dirishani hauoni mgonjwa wako akipata huduma inavyotakiwa, yaani yupoyupo tu kitandani na limtungi limemsimamia likingoja azime lihamie kwa mwingine liendeleze maokoto.
 
Inabidi kuhoji haya mambo. Ipo hatari kubwa ya kuuziana mbuzi kwenye magunia.

Hospitali nyingi za umma zina mitambo ya umma ya kuzalisha hizi oxygen.

View attachment 2518291

Bei hIzi kwenye hospitali za umma hazikubaliki. Labda kama ni mpango tu wa kuwafilisi watu na mifuko ya bima.
Tatizo unaweza zani kua ni hospital za umma,kumbe nyuma ya pazia zinamilikiwa na watu binafsi, ndiyo maana malipo ni lazima! Kumbuka kuna mikataba mingi ya sirini!!
 
Tatizo unaweza zani kua ni hospital za umma,kumbe nyuma ya pazia zinamilikiwa na watu binafsi, ndiyo maana malipo ni lazima! Kumbuka kuna mikataba mingi ya sirini!!

Hii nchi inahitaji total overhaul:

IMG_20231208_100714.jpg
 
Back
Top Bottom