MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES Best University in Tanzania, 1610th Worlwide

MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES Best University in Tanzania, 1610th Worlwide

analysti

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2009
Posts
731
Reaction score
614
Hizi ni Rankings za mwaka 2012, It is based on academic performance.

Tembelea: URAP - University Ranking by Academic Performance

Country Ranking: Tanzania World Rank
1. Muhimbili University of Health and Allied Sciences 1610
2. University of Dar Es Salaam 1618
3. Sokoine University of Agriculture 1749
cleardot.gif





Hongera sana Muhimbili! Hongereni wanafunzi wa Muhimbili!
 
hongera zao ila machifu wanaendelea kufa bila kurithisha vitengo kwa vijana!
 
hahahahahahahahahahah ukiwa wa kwanza kati ya wajinga wa mwisho sijui atakuwaje...hata mirembe kuna walio afadhali
 
hakuna kitu aisee hapa
kama hawafanyi machapisho,hawatoi madaktari quality tutaendelea kuwa wa mwisho mwisho
bora wangekuwa hata chini ya 200 tungesema wamejitahidi
maprof hawajishughulishi, wao wamekalia siasa, maabara hawaingii,nk kazi tunayo ndefu bado
 
Dar shule ya elfu na inapewa hongea? Ama kweli Tz na watanzania tuna vituko.
Ni kweli ya 1610 lakini Tz Ni ya 1. Jamani ulitaka chuo ulichosoma wewe ndiyo kiwe cha kwanza? Tuambiwe wewe umesoma wapi ili tujue chuo chako ni cha ngapi duniani.
 
hongera zao ila machifu wanaendelea kufa bila kurithisha vitengo kwa vijana!

Holo ndo tatizo!, Kama yule, wamekalia tu kusema, i am the only prof in so and so.......They think this contry will appreciate them kwa kusema hivyo, au they think kuwa tunafikiri they are the only people who are intelligent!!, Tunawaona kama ni wabinafsi na ni wahujumu wa elimu ya TZ na tasnia nzima ya Afya. Wanafunzi wanaenda kusoma postgraduate pale, wanawanyanyasa kama kitu gani, kitu ambacho lengo lake ni kuhakikisha tu vijana wale hawagraduate na kwenda kukamata vijiwe vyao huko mitaani. Huu ni ufisadi wa aina yake, wewe mzee kama umeshindwa kutengeneza maisha kwa kipindi cha miaka sitini, utaweza hivi sasa. Unakuta prof ana miaka 80, yupo hapo anafundisha kwa mkataba, Mara yupo Agakhan, mara Tumaini, Mara Regency, Mara.... mara ...., Huku anaendelea kuwakamata vijana wasigraduate. Inafika wakati kunakuwa na gap la wataalamu ambalo huchukua muda kuliziba!
 
Nimecheka sana hahahahaaaa chuo cha 1610 tanzania ndio cha kwanza alafu ulikonimaliza zaidi umecite from (URAP - University Ranking by
Academic Performance) hahahaaa alafu badala ya kuweka thread kwa masikitiko wewe unashangilia kama mwehu! "Ujinga nao ni kipaji" mwl Nyerere.. Mimi nimesikitika sana nchi yangu ilivyopotea, ukweli hautengenezwi hata siku moja.. Bora unatumia ID fake haujashusha reputation yako, haya mawazo yaache hapahapa usiende kwa watu wenye akili utachekwa sana na hizi cite za kwenye blog.
 
Inabidi mjue lakini kuwa hizi rankings hazitegemei akili za wanafunzi au walimu, zinategemea pesa ambazo chuo kinapewa kwa ajili ye research.
Muhimbili wamekuwa wa kwanza kwa sababu ya pesa zinazokuja kwenye tafiti za UKIMWI.
 
Kucheka na kulia zote ni kelele. Katika hili nashindwa kucheka nashindwa kulia.
 
Hizi ni Rankings za mwaka 2012, It is based on academic performance.

Tembelea: URAP - University Ranking by Academic Performance

Country Ranking: Tanzania World Rank
1. Muhimbili University of Health and Allied Sciences 1610
2. University of Dar Es Salaam 1618
3. Sokoine University of Agriculture 1749
cleardot.gif





Hongera sana Muhimbili! Hongereni wanafunzi wa Muhimbili!

Ila mbona kama UDSM wanaonewa ,wamefanya research za kutosha kuhusu kukubalika kwa Jk na chama chake cha CCM
 
3.university of Dodoma nafikiri hapo umesoma vizuri na nafikiri kadri muda unavyokwenda kitakuaja kuwa chuo cha kwanza kwa tanzania
 
Ufundishaji Bongo sio mbaya sana. Nimesoma Bachelor UDSM na Masters UK tena kwenye chuo bora, sijaona tofauti sana kwenye ufundishaji ila matatizo yako kwenye mambo yafuatayo ambayo yanaleta utofauti:


  • Kuchapisha/publication- Tanzania unaweza kukuta mtu eti ni Prof anakitabu kimoja na vi-article vichache wakati kwa wenzetu mtu ni PhD tu maandishi kibao. Wengine ndio baada ya PhD hata kuandika wamesahau. Mtu ni Lecturer hata kutayarisha notes hawezi kazi kupiga copy vitabu vya watu! Huwezi kuona Dr/Prof anagawa copy ya kitabu cha mtu kwa wenzetu.
  • Pesa za research zipo za kumwaga, ni jitihada yako kuziomba na kuzitumia.
  • Wataalamu/waalimu wanafanya consultations na si kufundisha tu. Hii inawafanya wawe na mambo mengi ya kufanyia tafiti, na baada ya hapo wanazichapa, publish.
  • Vipimo vya uelewa hasa kwa UK sio mitihani pekee. Nilishangaa sana hata kwa level ya Bachelor kuna baadhi ya programs mwanafunzi anapimwa kwenye maabala/ mfano computer au kuandika essay kwenye jambo fulani basi. Hivyo wao sio kila somo lazima ulifanyie mtihani wa kukaa kwenye meza masaa matatu mwisho wa semester bali unaweza kuingia library ukafanya kama ka-utafiti na ukaandika paper, basi. Jambo hili linawajenga sana katika uandishi.
  • Collaboration - ukiangalia moja ya vigezo vya vyuo bora ni collaboration. Vyuo vyetu vinapenda kujitenga sana, hasa UDSM. Nakumbuka wakati nasoma tuliwahi kuwaambia chuo pale Faculty of Commerce, (sasa UDBS) waangalie ku-incorporate sylllabus ya NBAA ili wahitimu wa BCom hasa Accounting na Finance wapate exemptions zaidi wakasema wao hawatoi degree ili baadae upate CPA. Kwamba CPA ni jambo lako binafsi hapo baadae. Wakaja na jeuri kwamba, by the way, CPA exams inakuwa moderated na walimu wa UDSM wakasahau kwamba NBAA ni independent institution hivyo inamaamuzi yake. Lakini baada ya mikwaruzano NBAA wakasalimu na kuendelea kutoa exemptions kwa BCom Accounting. Ila walifanya hivi kwa kuwapa uhuru UDSM wafundishe wanavyotaka wakati vyuo vingine vilipewa exemptions baada ya program zao kuwa scrutinized na NBAA.
  • Suala hili hili la ubabe wa kijinga wa UDSM unawafanya wanafunzi wa BAF Mzumbe wapate exemptions 7 kwenye ACCA,UK wakati BCom Accounting na BCom Finance ya UDSM wanapata 4 exemptions. Naongelea sehemu ninayoifahamu, yapo mengi naamini juu ya collaboration ambayo inabidi tubadilike kuendana na wakati na ulimwengu wa taaluma. Niongezee hapa kwa ACCA, Mzumbe kwa kweli kwa hili nawapongeza kwani wanapata exemptions kuliko hata baadhi ya vyuo vya UK. Ni kwamba they enjoy all exemptions, na masomo mawili ambayo hawapati exemptions kwenye ACCA ni Tax, kwa sababu Tax ni muhimu na wengi wanakuwa hawajaisoma, na pia kwa sababu ya different tax regime (Tanzania Vs UK Tax). La pili ni Financial Reporting ambalo katika vyuo haliwi covered vizuri. Baada ya hapo, wanafunzi wa Mzumbe wanaingia kwenye ACCA Professional Stage ambayo kila mtu lazima afanye. Nisiwachoshe na mambo ya BCom.
  • Citation - website hata za vyuo vyetu ziko poor. Ebu angalia website ya chuo chochote hapa nchini. Taarifa mpaka uzifuate ofisini hata mambo ya kawaida sana. Hakuna kazi za waalimu kwenye mitandao, unategemea nini? Website za vyuo vyetu hazipati HIT ( yaani watu hawazitembelei) kwa sababu hazivutiii, hazina taarifa, wakati kuna mengi ya kuweka kwenye mitandao yetu. Si jambo la kushangaza uka-click link fulani ukaambiwa ..under construction..au document unavailble..Usitegemee chuo kikapata rank nzuri.
  • Employability and graduate satisfaction..Wenzetu wanajali sana kuajiriwa kwa wanafunzi wao. Na hii ndio namba moja kwao. Vyuo vina-fight kutafuta waajiri kuja kuajiri hata chuoni kwa wanafunzi wanaomaliza. Kuna Career Centres zinawafundisha wanafunzi employment skills. Hizi centre kuna watu full time wameajiriwa kwa ajiri si ya kufundisha bali kutatua matatizo ya wanafunzi yanayohusiana na kuajiriwa.
Jamani mambo ni mengi..kuna mengi yakubadilisha.
 
Duuh! Enzi hizo za term system, MUHAS enzi hizo MUCHS, Sapu ilikuwa kawaida, Disco haikuwa ajabu, ukipata C, unashangilia na kwenda kunywa bia pale Mashine "BAR" kwa Mzee Njau. Anyway hongereni Ntogwi, Nyambo na marehemu wote mungu awalaze. Siku hizi MMED wanasoma wale waliotoka IMTU, HKMU na vyuo vingine vya magumashi.
 
Back
Top Bottom