Nilijua tu utakuja na hoja mufilisi kama hizo, umeshindwa kuthibitisha ni wapi zilifanyiwa utafiti, badala yake umekuja na majibu ya "dawa zote hufanyiwa utafiti kabla ya kutumika" sasa nakuongeza maswali mawili, je chanjo ya korona itadumu kwa muda gani katika kukinga au kutibu korona? Je tutachanjwa mara mbili kwa mwaka au zaidi? Si unasema ulifanyika utafiti? Majibu yako yarejee utafiti uliofanyika kwanza. Pili, wakati wa utafiti wa hyo chanjo tatizo la kuganda kwa damu lilionekana? Kwanini nchi nyingi zinasitisha chanjo?
Sent from my Android using
JamiiForums mobile app
Mkuu, tusibishanie hili, kwa sababu ninaelewa ninachokizungumzia hapa kwa uhakika kabisa wala sibahatishi.
Ninaposema hakuna dawa au chanjo yoyote inayoweza kutumika kwa binaadam bila kufanyiwa uchunguzi/utafiti kuwa ni salama; na kuwa kweli inafanya kazi inayotakiwa kufanya, wewe niamini hivyo, vinginevyo si rahisi kuanza kukupa darasa kwenye kurasa hizi za JF.
Kukujibu utafiti umefanyiwa wapi, haikupi jibu la kujua utafiti umefanywa au haukufanywa. Siyo lazima uje ufanyiwe hapa Tanzania ndiyo ujue kwamba chanjo hizo zimefanyiwa utafiti kitaratibu zote kama inavyotakiwa kwa dawa yoyote ile kabla ya matumizi yake.
Maswali ya nyongeza uliyoweka, yanahusiana vipi na swali la msingi kuhusu chanjo kufanyiwa au kutofanyiwa utafiti?
Hata hivyo ngoja nikufahamishe. "Chanjo ya corona itadumu kwa muda gani katika kukinga (siyo kutibu)"; hilo ni swala la mwili utakuwa na uwezo wa kuendelea kuzalisha kinga kwa muda gani. Kumbuka, sio chanjo inayozalisha kinga, ni mwili wako uliyepata chanjo ndio unaozalisha kinga baada ya kupata changamoto ya chanjo. Hii inaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu. Lakini kumbuka, maana ya chanjo ni kukinga mwili, lakini hapo hapo pia inasaidia katika maenezi ya maambukizi kwa jumuia, hii nayo ni faida.
Je, tutachanjwa mara mbili kwa mwaka au zaidi? Ni dhahiri unatafuta kujifunza hapa, maana inaonekana wazi hata ile A,B,C ya jambo hili huna kabisa. Chanjo inafanywa mara mbili, lakini hiyo haikupi garantii kwamba huwezi kuambikzwa na kuugua corona. Kuna waliochanjwa, na bado wakaugua corona..., hakuna hakika ya asili mia kwa mia; si kwa corona peke yake na hata chanjo zingine, na dawa za aina nyingine zote.
Hata hivyo, nikukumbushe (hapana, nikufahamishe, kwa sababu mambo haya huyajui), corona ni virus. Virus wanao uwezo wa kujibadilisha kadri wanvyopita kwenye miili ya watu (utakuwa umesoma angalau strain mpya zinazojitokeza Africa Kusini na kwingineko); kwa hiyo huwezi kutegemea kwamba chanjo ya mwanzo itakuwa inafanya kazi kwenye 'strain' zingine zote zitakazokuwa zinajitokeza baadae, ni kama wale virusi wa influenza, nao hubadilikabadilika kwa msimu, na chanjo zinatengenezwa kufuatana na 'strain' ya msimu fulani inayotegemewa kuwepo.
"Wakati wa utafiti wa hiyo chanjo tatizo la kuganda damu lilionekana?"
Mkuu, hata haya unayosoma juu juu bado hayakusaidii, kwa sababu inaonyesha unachanganya mambo.
Kuna aina nyingi tu sasa za chanjo ya corona, siyo hiyo tu moja ya Astra Zeneca unayozungumzia wewe. Zipo nyingi zisizokuwa na tatizo la namna hiyo.
Hata hivyo, swali lako limekaa kishabiki - nani aliyekwambia kwamba kuna dawa yoyote hapa duniani isiyokuwa na madhara? Ulishaona dawa yoyote ambayo unaweza kutumia tu usitegemee kuwepo matatizo hata kama itafanya kazi vizuri?
Halafu eti unahitimisha: "kwa nini nchi nyingi zinasitisha chanjo"? Nchi gani zimesitisha chanjo? Na bado hutaelewa kwa nini nimekupa swali hilo. Sitegemei wewe kulijibu kwa usahihi, lakini nimekuuliza tu kukuonyesha ni kiasi gani usivyojua chochote, lakini upo hapa unajifanya kama wewe kweli ni mjuaji wa haya mambo.
Nchi yetu tumekuwa sana na utapeli wa namna hii, watu kujifanya wanajua, kumbe hawajui chochote. Hadi viongozi wa siasa sasa ndio wamekuwa wajuaji wakubwa wa sayansi kuliko wanasayansi wenyewe. Matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona sasa hivi.
Halafu ulivyo kilaza unasema:
"Ulijua nitakuja na hoja mfilisi..." Hoja zako ni zipi hapa?
Mtu ni wazi huna hata chembe ya unachoelewa!