Muhimbili yakanusha taarifa za uzushi kuwa muuguzi wake amefariki kwa Corona

UFAFANUZI KUHUSU KIFO CHA MAREHEMU EVODIA KAPINGA ALIYEKUA MUUGUZI WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI*

Dar es Salaam, Jumapili Aprili 19,2020

Kuna taarifa inasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Marehemu Evodia Kapinga amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona na kwamba alikua akihudumia wagonjwa wa Corona. *Marehemu Kapinga hajawahi kuhudumia wagonjwa wa wanaougua ugonjwa wa Corona*

Marehemu alikua akitoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto.
Marehemu ni mgonjwa wa siku nyingi aliyekua akisumbuliwa na MARADHI AMBAYO HATUWEZI KUYATAJA KULINGANA NA MAADILI YA TIBA.

Jana jumamosi tarehe 18 Aprili, 2020 saa NNE USIKU marehemu akiwa nyumbani kwake Kimara, alizidiwa ambapo watoto wake walifanya jitihada ya kumkimbiza Muhimbili lakini wakiwa njiani hali yake ilibadilika ndipo walipompeleka Hospitali ya karibu ya Sinza, Palestina.

Madaktari na Wauguzi walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake bila mafanikio ambapo amefariki leo jumapili saa 09 alfajiri.

Hivyo, taarifa
zinazosambaa kuwa kifo chake kinatokana na ugonjwa wa Corona siyo za kweli, ZIPUUZWE.

Imetolewa na;

Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Amaniel, stop this nonsense! Wewe huna uwezo au courage ya kusema amekufa kwa corona, stop this rubbish! Amaniel stop this nonsense! Kwahiyo hakuna restriction kumzika, ndugu wake wote anayependa ataruhusiwa kwa kuchukua tahadhali wenyewe?
 
Hivi hawa wanaozusha wanapata faida gani?
 
RIP Mtaalamu, namfahamu sana, mazishi lini? Turuhusiwe kuhudhuria mazishi, na wasizike harakaharaka kama muathirika wa COVID-19
UFAFANUZI KUHUSU KIFO CHA MAREHEMU EVODIA KAPINGA ALIYEKUA MUUGUZI WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI*

Dar es Salaam, Jumapili Aprili 19,2020

Kuna taarifa inasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Marehemu Evodia Kapinga amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona na kwamba alikua akihudumia wagonjwa wa Corona. *Marehemu Kapinga hajawahi kuhudumia wagonjwa wa wanaougua ugonjwa wa Corona*

Marehemu alikua akitoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto.
Marehemu ni mgonjwa wa siku nyingi aliyekua akisumbuliwa na MARADHI AMBAYO HATUWEZI KUYATAJA KULINGANA NA MAADILI YA TIBA.

Jana jumamosi tarehe 18 Aprili, 2020 saa NNE USIKU marehemu akiwa nyumbani kwake Kimara, alizidiwa ambapo watoto wake walifanya jitihada ya kumkimbiza Muhimbili lakini wakiwa njiani hali yake ilibadilika ndipo walipompeleka Hospitali ya karibu ya Sinza, Palestina.

Madaktari na Wauguzi walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake bila mafanikio ambapo amefariki leo jumapili saa 09 alfajiri.

Hivyo, taarifa
zinazosambaa kuwa kifo chake kinatokana na ugonjwa wa Corona siyo za kweli, ZIPUUZWE.

Imetolewa na;

Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hao waliofariki walikuwa na magonjwa mengne, hivyo hilo kuwa alikuwa na ugonjwa muda mrefu liondoe kabisaa na ukitaja hivyo unapelekea hisia ya watu kuwa basi ameharakishwa na hiyo kitu Kama ilivyotokea kwa wengne

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe mama ni mbisha kama K! Hata mumeo kama umeolewa anakazi kweli kweli!!
 
Alikuwa akiugua muda mrefu sasa iweje ghafla tena? My friends hiyo ni Corona asilimia 100. Yani ukiona mtu ana maradhi ya muda mrefu kisha kwa kipindi hiki akaugua ghafla na kufa jua kuwa mzee wa kazi Corona kashatimiza wajibu wake.

Nasikia kazikwa tayari tena na serikali na ndugu wapo karantini.

Alale pema peponi kamanda kafia kazini. Dah ilikuwa sahihi kuitenga Muhimbili japo wamechelewa.
 
Analogia Malenga,
Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Ripoti ya Muhimbili Hospital na ufafanuzi ina mapungufu makubwa na ya msingi kabisa kuleta shaka ktk jamii na familia, sote tunajua wafanyakazi sekta ya afya wapo ktk hatari kubwa ya kuambukizwa.

Swali ambapo halijajibiwa ktk taarifa ya hospitali kuu ya taifa Muhimbili, Dar-es-Salaam je mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi autopsy https://www.mayoclinicproceedings.org/article/S0025-6196(12)64990-8/fulltext na swabs kuchukuliwa Effectiveness of Patient-Collected Swabs for Influenza Testing kujiridhisha pamoja ya kuwa marehemu alikuwa na matatizo mengine ya siku nyingi ya kiafya, majibu ya autopsy, vipimo vya swabs, damu n.k vilionyesha alikuwa Covid-19 negative ?

Back
Top Bottom