Muhimbili yakanusha taarifa za uzushi kuwa muuguzi wake amefariki kwa Corona

Muhimbili yakanusha taarifa za uzushi kuwa muuguzi wake amefariki kwa Corona

Kwani Ni ajabu kwa muuguzi kufa kwa Corona, waache hizo bwana.
 
UFAFANUZI KUHUSU KIFO CHA MAREHEMU EVODIA KAPINGA ALIYEKUA MUUGUZI WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI*

Dar es Salaam, Jumapili Aprili 19,2020

Kuna taarifa inasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Marehemu Evodia Kapinga amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona na kwamba alikua akihudumia wagonjwa wa Corona. *Marehemu Kapinga hajawahi kuhudumia wagonjwa wa wanaougua ugonjwa wa Corona*

Marehemu alikua akitoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto.
Marehemu ni mgonjwa wa siku nyingi aliyekua akisumbuliwa na MARADHI AMBAYO HATUWEZI KUYATAJA KULINGANA NA MAADILI YA TIBA.

Jana jumamosi tarehe 18 Aprili, 2020 saa NNE USIKU marehemu akiwa nyumbani kwake Kimara, alizidiwa ambapo watoto wake walifanya jitihada ya kumkimbiza Muhimbili lakini wakiwa njiani hali yake ilibadilika ndipo walipompeleka Hospitali ya karibu ya Sinza, Palestina.

Madaktari na Wauguzi walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake bila mafanikio ambapo amefariki leo jumapili saa 09 alfajiri.

Hivyo, taarifa
zinazosambaa kuwa kifo chake kinatokana na ugonjwa wa Corona siyo za kweli, ZIPUUZWE.

Imetolewa na;

Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Sawa tutazipuuza lakin,swali muuguzi huyo tayari ameshazikwa?na kama tayari je maiti yake wamepewa ndugu wazike na kama bado tutaona nani atawajibika kuzika huo mwili!!! tanzania hii huu ugonjwa unaweza ukatuathiri vibaya sana kama viongozi watakalia ukweli.badala ya kuweka wazi bayana hali halisi ya huko maosptalini.
 
Kwa hivyo angekuwa ndugu yako kama mama au dada ungependa taarifa za ugonjwa wake kuwekwa kwenye vyombo vya habari?
Mfano alikuwa anaugua magonjwa ambayo ktk jamii yanafanya watu waone aibu kujulikana?

Au ya kawaida lakini kwa sababu flani za kimikataba ya kisheria kama mambo ya bima usingependa yajulikane na mtu wa nje ya familia.
Wangekausha tu kama vipi mbona hao wengine wamesema presha wangekausha tungewaona wamaana sana
 
Back
Top Bottom