Muhimbili yamtunuku Rais Samia Tuzo ya Udaktari Bingwa Bobezi wa mageuzi sekta ya Afya

Muhimbili yamtunuku Rais Samia Tuzo ya Udaktari Bingwa Bobezi wa mageuzi sekta ya Afya

Hospitali ya Taifa Muhimbili imemtunuku tuzo ya heshima ya udaktari bingwa bobezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa katika mageuzi ya huduma za Afya Nchini.

Tuzo hiyo imetolewa kwenye hafla iliyowakutanisha Madaktari na wauguzi Bingwa bobezi Machi 28, 2026 kwenye Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam.
 
Kuna muda nahisi chawa industry inakuwa kwa kasi sana,watu wasomi na ma PHD yao lakini akili anaweka kwenye tumbo lake.

Kujikomba komba tu,inakera sana hii tabia
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili imemtunuku tuzo ya heshima ya udaktari bingwa bobezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa katika mageuzi ya huduma za Afya Nchini.

Tuzo hiyo imetolewa kwenye hafla iliyowakutanisha Madaktari na wauguzi Bingwa bobezi Machi 28, 2026 kwenye Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam.

#fblifestyle
 
Hizo tuzo Hua zinachekesha sanaaa miezi kadhaa iliopita alipewa tuzo ya maji kufanaikisha maji kutoka masaa 24 Tanzania nzima ile anapewa tu tuzo na maji yakakatika maeneo mengi Tanzania mpaka Leo ninapokaa maji hayatoki walisema mito imekauka lakini kwa sasa mvua zinanyesha mpaka mafuriko na bado maji hayatoki

Hizi tuzo wanampa za nini mbona hatuelewi au ndio Uchawa wa kichoko

Kwanini mtu asifanye Kazi zinazoonekana hata kwa watanzania wa kawaida ndio mumpe tuzo
 
Sio Mchezo,mtu anaitwa bobezi from nowhere...

Labda wanamaanisha yupo juu ya mwenye super speciality na sijui ya nini kwenye afya, coz kila ubingwa unasomewa hamnaga kupeana kwenye afya ndio ya kwanza hii, hata Nyerere hatujawahi kusikia kapewa, kama kumbukumbu zangu zipo sawa
 
Wanamcheza shere, kuna kitu wanakihitaji kwake, ndio wanamnanga bila yeye kujijua.
Ukipenda sifa, unaweza katika viuno ukweni
 
Taasisi zinazotoa tuzo hizo zinazingatia vigezo gani ili kumpa mtu tuzo? Ukweli nchi yetu inahitaji reforms katika kila eneo. Itoshe kusema tupate katiba mpya na bora.
 
Very stupid! Ni ngumu kuamini kuwa kitu kama hicho kinaweza kufanywa na madaktari wanaoitwa mafaktari bingwa! Ndiyo maana kuna wakati unakutana una tatizo la kiafya, unaambiwa ukutane na daktari bingwa, lakini anachokufanyia ni uharibifu badala ya kukutibu! Kila kitu tumegeuza ni siasa za uchawa.

Hao madaktari bingwa bandia, wangekuwa na hekima japo cha kiasi cha chini, wangeweza kumpa tuzo, lakini siyo kuiita tuzo ya udaktari bingwa. Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na uelewa, unatarajia kuwa tuzo ya ufaktari bingwa itatolewa kwa daktari bingwa aliyefanya kitu cha pekee kwenye udaktari bingwa wake. Sasa huyo aliyepewa amefanya nini katika tiba ya kibingwa ili tuitangazie Dunia kuwa huku kuna daktari bingwa amevumbua tiba ya tatizo gani? Wenzetu wanawekeza kwenye gunduzi mbalimbali, sisi tunawekeza kwenye uchawa!!
 
Back
Top Bottom