
Salaam sana wajasiria Kilimo,
Kujiunga katika masomo hayo tafadhali jaza fomu hii
https://goo.gl/forms/wg3afYbHrEDwbGNJ2 kwa mtandao ama tuma sms ama email yenye ujumbe wenye 1.
jina Lako kamili 2.
Namba ya simu 3.
zao unalotaka kulima ama kuzalisha 4.
eneo la mradi ama jina la kijiji unataka kuweka kilimo hicho 5.
Msimu wa mradi huo ama lini unaanza/ ulianza 6.
Mahitaji mengine mf mbegu na ushauri wa masoko kwenda namba 0753843321 ama 0718664645 ama 0789856246 email
kilimobiznet@gmail.com cc
info@graduatefaemers.co.tz (KUMBUKA KUWA NA HABARI ZA KUTOSHA KUHUSU MAHITAJI YA SOKO UNALOTEGEMEA).
Ni wakati mwingine tena tukijiandaa kuanza msimu wa Kilimo cha nafaka na Mikunde pamoja na mazao mengine. Tunashukuru sana kwa wale ambao wameshanunua mbegu bora za mazao hayo kupitia Umoja wa Wakulima wahitimu (Graduate Farmers) na kutumiwa ama kuchukua mbegu hizo sehemu husika.
Kutokana na maombi ya wadau wengi wa Kilimo cha mazao ya mikunde wakiwa wanahitaji kufaham namna bora ya Kuzalisha na kusimamia miradi ya Kilimo cha mazao ya DENGU, CHOROKO, KUNDE, MBAAZI NA DENGU kampuni yetu kwa kushiriana na GRADUATE FARMERS tutakuwa na madarasa huru na ushauri elekezi wa BURE kupitia mitandao ya kijamii hasa WHATSAPP na GOOGLE GROUPS kuanzia tar 12 mwezi wa 10/2016.
Ushauri elekezi utaendana na majadiliano, maelekezo ya Sauti picha kwa Kilimo bora cha Mbaazi, dengu, kunde na choroko, mpangilio wa miradi ya uzalishaji wa mbaazi, uhifadhi na mbinu sahihi za masoko.
Karibuni sana muda wa kuomba kuwekwa kwenye kundi ni kesho saa 11 jioni.