Muigizaji maarufu nchini India, Salman Khan ahukumiwa jela miaka mitano kwa kosa la kuua swala

Muigizaji maarufu nchini India, Salman Khan ahukumiwa jela miaka mitano kwa kosa la kuua swala

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Muigizaji mkongwe nchini India, Salman Khan amehukumiwa kwenda jela miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuua wanyama jamii ya swala miaka 20 iliyopita.

4AD71FC000000578-5580785-Heading_to_jail_Bollywood_actor_Salman_Khan_52_has_been_found_gu-m-24_1522920054033.jpg

Salman Khan mwenye miwani akipelekwa gerezani.

Leo Aprili 05, 2018 Mahakama Kuu mjini Jodhpur katika jimbo la Rajasthan nchini India imetoa hukumu hiyo baada ya kumkuta na hatia, huku waigizaji wenzake Saif Ali Khan, Tabu, Sonali Bendre na Neelam Kothari wakiachiwa huru baada ya kukutwa hawana hatia.

Salman Khan (52) alishtakiwa kwa kosa la ujangili kwa kuua wanyama hao (BlackBuck Antelopes) ambao ni wachache nchini India mnamo mwaka 1998.

ANIMALS-OF-INDIA-BLACKBUCK-%E2%80%93-A-SPECIAL-ANTELOPE.png

Aina ya wanyama aliyowauwa Salman Khan.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail, Salman Khan alifanya tukio hilo katika kijiji cha Kankani wakati aki-shoot filamu yake ya Hum Saath Saath Hain akiwa na wasanii wenzake watano ambao wameachiwa leo.

Source: Bongo 5
 
Hawa nao wamezidisha dharau na ubaguzi hadi kwa wao kwa wao, acha akale mavi jela
 
Whaaat nooo!please who is going to run BBS season 12?!!##
 
Back
Top Bottom