Muislamu anaweza kutibu nguruwe?

Muislamu anaweza kutibu nguruwe?

Nimesoma mifugo na waislam wanamshika nguruwe vizuri sana na wanamtibu na kumwosha kabisa,wengine walienda mbali zaid wakamla sio mara moja na si mmoja na walikiri huyu mdudu wanamsingizia hana makosa yoyote
Andiko halitabadilika ukisema waislamu umejumlisha wote na hili ni kosa ,kuna muislam ni mwizi ,jambazi ,malaya au mchawi ,hatuwezi tukasema wote wako vile ila ni wachache ,katika uislamu tumekatazwa kula nyama ya nguruwe na humo ndani kuna busara ya yake ,ukimuona muislam anafanya kinyume na Katazo,haimaanishi Katazo hilo litakuwa halali kwa kuwa yeye ni muislamu ,bali atakuwa amefanya makosa ,muulizaji wa swali unatakiwa ujue dhumuni la kumtibu nguruwe nini ?

Ni sawasawa na kukutana na mtu njiani anakuambia nisaidie kusukuma hili gari langu limeingia kwenye tope ,limeshindwa kutoka haliyakuwa limebeba kreti za pombe ,je utamsaidia ?

Mfano mwingine ni mzazi wako kukutuma dukani ukamletee sigara ,je utaenda?
Kwa hiyo atakayeshiriki kwa namna moja au nyingine kutendeka kwa Katazo katika uislamu naye atakuwa amelitenda,utamtibu nguruwe kuna watu watakula nyama yake hili nalo liangaliwe.

Cha kuzingatia ya kwamba usimjibu mtu masuala ya dini kutokana na hisia na maono yako ,ukiwa hujui unakaa kimya kusubiri wanaojua, upotoshaji katika masuala ya dini nayo ni makosa makubwa ,tuweni makini ndugu zangu(nami sio mkamilifu)
Screenshot_20221210-135813_1.jpg
 
Niliwahi pita na nguruwe kwenye pikipiki mbele ya msikiti ikawa nongwa! Nilizongwa sana, tulichapana sana mkono na madogo wa msikitini pale,walianza kama masikhara apigwe apigwe,nilipambana kiume wakataka kuchoma pikipiki. Ila nilichapika sana siku ile sitasahau. Akatokea mzee mtu mzima toka msikitini akawaamuru waniachie ndo tifu likaisha. Nguruwe wangu nilikuwa nimemfunga nyuma na mipira nikawasha chuma nikasepa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwani nguruwe sio kiumbe cha Allah
Anaweza kuwa kiumbe cha Allah, ila yeye akawa na msimamo wale wa kuto watibia.
Kumbuka Papa amewata viongozi wa dini, ndani kanisa lake, kuwabariki wapenzi wa jinsia moja, akitoa sababu kuwa, wapenzi wa jinsia moja nao, ni wa Mungu.

Ila kuna baadhi ya viongozi wa kanisa hilo, wameonyesha, msimamo wao wa kupinga kauli hiyo ya Papa.
 
Poleni na majukumu wakuu.

Niende kwenye mada,hivi dakitari wa wanyama (vet) Muislam ana ruhusiwa kutibu nguruwe?

Kama hapana, je pale vyuo vya kilimo huwa naona wakifuga wanyama tofauti tofauti akiwemo na nguruwe au taaluma haina dini?

Kama ndiyo basi daktari hatakiwi kuwa na itikadi ya dini yoyote kwa maana hakuna kitabu cha dini yotote kinachoruhusu kula nguruwe ila kama mimi sijaelewa basi naomba wajuvi wa mambo haya mnisaidie[emoji120]
Mchungaji hawezi kutibu Mwanaume mzinzi?[Mwanaume mwenye zaidi ya mke mmoja]
 
Ewaaaa swali zuri sana nakupa jibu alafu hilo jibu nataka ukawape na wengine .


SABABU GANI NA KUNA ATHARI GANI YA KIAFYA KWENYE ULAJI WA NYAMA YA NGURUWE


[KUWA NA] VITU VYENYE SUMU

Nyama ya nguruwe ina mafuta mengi sana. Ikiwa italiwa, mafuta huchanganyika na damu. Kwahiyo, damu huchanganyika na chembechembe za mafuta. Kiwango hiki kikubwa cha mafuta husababisha magonjwa yanayojulikana kama, arteriosclerosis, presha (hypertension) na magonjwa ya moyo (heart infarct). Zaidi ya hayo, vitu vyenye sumu vijulikanavyo kama sutoxines vinapatikana kwenye siagi (lard). Matezi ya limpathik (Lymphatic glands) hulazimika kufanya kazi ngumu ili kuondoa chembechembe hizo za sumu ambazo huingia mwilini. Husababisha maambukizi na kunyonya tezi zijulikanazo kama lymph nodes hasa kwa watoto. Koromeo la mtoto humeza na kuonekana kama la nguruwe. Hivyo basi, maradhi haya yanajulikana kama scrofulosis (maradhi ya nguruwe). Kama maradhi yataongezeka, tezi zote za lymph huathiriwa na kumezwa. Hali joto huongezeka; maumivu huanza na hali ya hatari sana hujitokeza.


KIWANGO KIKUBWA CHA SALFA


Tishu zijulikazo kama kolageni (collagen tissue) zilizopo katika mfumo wa majimaji kamasi (mucus) ambazo zinapatikana kwa wingi kwenye nyama ya nguruwe, zina kiwango kikubwa sana cha salfa (sulfur). Hivyo, kiwango kikubwa cha salfa huchukuliwa na kuingizwa mwilini. Kiwango hiki cha ziada cha salfa hubaki kwenye misuli (muscles) na mishipa ya neva (nerves), na kusababisha maambukizi kwenye viungio (joints), calcification na ngiri (hernia) kwenye viuno (loins). Ikiwa mtu atakuwa na mazoea ya kula nyama ya nguruwe, sehemu ngumu (hard cartilage) kwenye mwili itaondolewa na tishu za kolageni zenye mfumo wa majimaji (kamasi) kutoka kwa nguruwe. Hatimae, fuvu gumu linalainika; haliwezi sasa kuhimili uzito wa mwili na huvunjika. Hivyo basi, uharibifu kwenye viungo huanza kujitokeza. Miili ya wanaokula nyama ya nguruwe huwa legevu kama jeli; tabaka za mafuta hutengenezeka. Kwa mfano, mwanamichezo akila nguruwe, huwa mchovu, mvivu na kutokuwa madhubuti. Baadhi ya wachezaji wa mpira hufikia hatua ya kukata tamaa kwasababu ya matumizi ya nyama ya nguruwe.


UKUAJI KUPINDUKIA


Kiwango cha vichocheo vya makuzi (growth hormone) kwenye nguruwe ni vingi kupita kiasi. Kitoto cha nguruwe ambazo kina uzito wa gramu mia kadhaa anapozaliwa huwa na kilo mia kwa miezi sita tu. Kwa kiwango hicho cha makuzi ni kutokana na kiwango kikubwa cha vichocheo vya makuzi (growth hormone). Homoni ya makuzi inayobebwa na nyama ya nguruwe husababisha kumezwa kwa tishu na maambukizi kwenye mwili. Husababisha pua, kidevu, mkono na mifupa ya miguu kukuwa katika hali isiyo ya kawaida na mwili kuganda mafuta. Jambo la hatari zaidi kwenye homoni hii ya makuzi ni uwezekano wa kufungua njia ya kupata saratani (cancer). Kwakweli, wachinjaji wa nguruwe wanaeleza kwamba nguruwe dume hupata saratani baada ya umri fulani.


MARADHI YA NGOZI


Chembe chembe zinazojulikana kama histamine na imidazole kwenye nyama ya nguruwe husababisha maumivu kupita kiasi. Pia hurahisisha kutokea kwa maradhi ya kuambukiza ya ngozi kama vile ugonjwa unaojulikana kama eczema, damatiti (dermatitis) na nyurodamatitis (neurodermatitis). Chembechembe hizi huongeza hatari ya kutokea majipu (boils), kidole tumbe (appendicitis), magonjwa ya kibofu (gall bladder diseases), venali (venal) na maambukizi ya ateri (arterial infections). Kwa sababu hiyo, madaktari huwashauri wagonjwa wa moyo wasile nyama ya nguruwe.

NYAMA YA NGURUWE NA MNYOO UJULIKANAO KAMA TRICHINA


Moja ya maradhi hatari sana ambayo yanaaambukizwa kwa mwanadamu kupitia nyama ya nguruwe ni trichina. Ingawa, trichina hausababishi tatizo kubwa kwa nguruwe mwenyewe. Hata hivyo, mnyoo huu unasababisha maradhi hatari sana kwa wanadamu. Mnyoo wa trichina humezwa kupitia nyama ya nguruwe na kwenda kwenye damu kupitia utumbo mkubwa na utumbo mdogo. Hivyo basi, hutapakaa mwili mzima.


Minyoo ya trichina hukaa hasa kwenye tishu za misuli kwenye magego, ulimi, shingo, koo na maeneo ya kifuani. Husababisha kupooza kwenye kutafuna, kuzungumza na misuli ya kumezea. Pia husabisha vikwazo kwenye mishipa, tatizo la meningitis na athari kwenye ubongo. Na hatari zaidi zinaweza kusababisha kifo. Jambo la hatari katika maradhi haya ni kwamba hayana tiba sahihi. Ugonjwa wa trichina ni maarufu hasa kwenye nchi za Ulaya. Mripuko wa maradhi ya trichina umeshuhudiwa kwenye nchi kama vile Uswidi (Sweden), Uingereza, na Poland, licha ya udhibiti wa mifugo. Uturuki, mripuko wa ugonjwa wa trichina haujawahi kuonekana isipokuwa kwenye jamii za Wakristo wanaoishi Uturuki.


CHAKULA NA TABIA YA MWANADAMU


Wanadamu na wanyama huathiriwa na vyakula wanavyokula kwa kiasi fulani. Kwa mfano, inajulikana kwamba wanyama wanaokula nyama (carnivorous) kama paka, mbwa na simba ni wakali na wanyama wanaokula majani (herbivorous ) kama kondoo, mbuzi na ngamia ni watiifu na wapole. Na hivyo hivyo kwa wanadamu. Imeonekana kwamba watu wanaokula mboga kwa ujumla wao ni wapole, na wale wanaokula nyama na yatokanayo na nyama ni wakali. Nguruwe ni mnyama pekee ambae hana wivu kwa mwenza wake wa kike. Imegundulika kuwa hisia za wivu zinadhoofika au kuisha kabisa kwa wanaotumia nyama ya nguruwe. Katika kulipa umuhimu jambo la athari za chakula kwenye tabia, Savorin, mwanafalsafa wa Kifaransa amesema “Niambie unachokula, ntakuambia wewe ni nani.”


CHAKULA CHA HALALI KINATOSHA KWA MAHITAJI YA MWANADAMU


Mola wetu ametuumbia aina nyingi za vyakula kwa ajili yetu. Ingawa, Ametukataza tusile na tusinywe aina za vyakula vyenye madhara kwasababu Ana ukarimu na huruma isiyo na ukomo. Hamtwishi mja wake mzigo mzito ambao ni nje ya uwezo wake. Maamrisho na makatazo yake ni rahisi kutekelezwa. Kwani mtu atapoteza nini akiacha kunywa pombe na ikiwa hali nyama ya nguruwe?

Hilo jibu kama alijakutosha niambie mkuu nitakupa jibu jingine cha umuhimu nataka upate elimu tu
Cha kushangaza China na korea ndio zinaongoza kwa ulaji wa nyama ya nguruwe ila kiwango chao cha kuishi kipo juu kuliko cha watu wa mataifa ya mashariki ya kati ambao ulaji wao wa nguruwe upo chini.
 
Sio tuu kutibu hata kupandikiziwa figo ini la nguruwe anapewa hata kupika kasoro kuonja tuuu. Hata pua ya nguruwe anaweza pandikiziwa
 
Back
Top Bottom