Muislamu anaweza kutibu nguruwe?

Nimesoma mifugo na waislam wanamshika nguruwe vizuri sana na wanamtibu na kumwosha kabisa,wengine walienda mbali zaid wakamla sio mara moja na si mmoja na walikiri huyu mdudu wanamsingizia hana makosa yoyote
Andiko halitabadilika ukisema waislamu umejumlisha wote na hili ni kosa ,kuna muislam ni mwizi ,jambazi ,malaya au mchawi ,hatuwezi tukasema wote wako vile ila ni wachache ,katika uislamu tumekatazwa kula nyama ya nguruwe na humo ndani kuna busara ya yake ,ukimuona muislam anafanya kinyume na Katazo,haimaanishi Katazo hilo litakuwa halali kwa kuwa yeye ni muislamu ,bali atakuwa amefanya makosa ,muulizaji wa swali unatakiwa ujue dhumuni la kumtibu nguruwe nini ?

Ni sawasawa na kukutana na mtu njiani anakuambia nisaidie kusukuma hili gari langu limeingia kwenye tope ,limeshindwa kutoka haliyakuwa limebeba kreti za pombe ,je utamsaidia ?

Mfano mwingine ni mzazi wako kukutuma dukani ukamletee sigara ,je utaenda?
Kwa hiyo atakayeshiriki kwa namna moja au nyingine kutendeka kwa Katazo katika uislamu naye atakuwa amelitenda,utamtibu nguruwe kuna watu watakula nyama yake hili nalo liangaliwe.

Cha kuzingatia ya kwamba usimjibu mtu masuala ya dini kutokana na hisia na maono yako ,ukiwa hujui unakaa kimya kusubiri wanaojua, upotoshaji katika masuala ya dini nayo ni makosa makubwa ,tuweni makini ndugu zangu(nami sio mkamilifu)
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwani nguruwe sio kiumbe cha Allah
 
Kwani nguruwe sio kiumbe cha Allah
Anaweza kuwa kiumbe cha Allah, ila yeye akawa na msimamo wale wa kuto watibia.
Kumbuka Papa amewata viongozi wa dini, ndani kanisa lake, kuwabariki wapenzi wa jinsia moja, akitoa sababu kuwa, wapenzi wa jinsia moja nao, ni wa Mungu.

Ila kuna baadhi ya viongozi wa kanisa hilo, wameonyesha, msimamo wao wa kupinga kauli hiyo ya Papa.
 
Mchungaji hawezi kutibu Mwanaume mzinzi?[Mwanaume mwenye zaidi ya mke mmoja]
 
Cha kushangaza China na korea ndio zinaongoza kwa ulaji wa nyama ya nguruwe ila kiwango chao cha kuishi kipo juu kuliko cha watu wa mataifa ya mashariki ya kati ambao ulaji wao wa nguruwe upo chini.
 
Sio tuu kutibu hata kupandikiziwa figo ini la nguruwe anapewa hata kupika kasoro kuonja tuuu. Hata pua ya nguruwe anaweza pandikiziwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…