Zinedine
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 1,187
- 694
Tofauti ya mwanzo na kubwa iliyopo baina ya ughaibuni na nchini kwetu sio hatua ya maendeleo ya majengo na miundombinu mingineyo, bali ni utofauti wa usalama wa raia. Polisi wa ughaibuni hana taim na asiye mhalifu, na hawana taim na watu, polisi wetu hawana taim na wahalifu ila na wasio wahalifu. Unatembea usiku kucha hakuna mtu wala polisi atakayekuuliza kama huna shida. Tembea saa tano nchini kwetu na mkeo uone polisi watakavyoona dili. Hili ni jambo la kushangaza sana na linatutoa akili watu weusi, why? why polisi wanakosa maadili kiasi hiki why?. Likitokea tukio la kihalifu litakuwa gumzo na vyombo vyote vya habari, ukisahau japo simu klabuni jua utaikuta au itapelekwa kituo cha polisi. Wakikuona usiku wa maneno unatatizika na jambo, polisi wako tayari kukusaidia si kukutisha,