Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Wakuu story ni kwamba huyu jamaa kwenye picha amemuua huyo mkewe usiku wa kuamkia leo huko Mwanza ikidaiwa ni baada ya kumkataza mkewe asiende kwenye show ya Mondi.

Baada ya kumwambia asiende kwenye hiyo show ya Nasib Abdul, mke akakaidi akaenda.

Jamaa amempiga risasi saba za kichwa na inasemekana na yeye kajiua japo maiti yake haijaonekana.

Ila na nyie Wanawake mpunguze visirani. Inaonesha jinsi huyu Marehemu alikuwa mkaidi na hamsikilizi Mme wake.

Mme kakuambia sitaki uende pahala fulani then wewe unakaidi ni nini kama sio dharau na kiburi?

By the way anything else Happen for a reason.

RIP Binti Mzuri



==================================

Mama mzazi wa marehemu, Bi Tiba Mohamed anasimulia kilichotokea kuhusu ndoa ya mwanaye na mumewe ambao wamedumu katika ndoa kwa muda wa miezi mitano, kwani walifunga pingu za maisha Desemba 30, 2021.

Anasimulia: “Watoto wangu waliitwa na baba yao hapa nyumbani (Mei 28, 2022), walipofika baba yao akapata dharura hivyo hakuzungumza nao nikabaki nao tukawa tunataniana tu.

“Alikuwa akinitania kwa kufurahi kuwafunga Simba akawa anishawishi na mimi nihamie Yanga (Yanga iliifunga Simba bao 1-0 siku hiyo kwenye CCM Kirumba Mei 28, 2022).

“Baadaye baba yake akapiga simu na kusema mume wa Swalha amepiga simu kumjulisha kuwa amefika na hivyo Swalha aende akampokee Igombe.

“Swalha akasema gari yake haina mafuta, hivyo wakakubaliana wakutane nyumbani na mwanaume akasisitiza kuwa ana njaa sana, akamtaka mke wake aende akampikie.

“Nikawasindikiza hadi barabarani mida ya saa moja usiku, muda huohuo mume wake akapiga simu akiwa anafoka, nikamtaka awe na subira mkewe anakuja yupo njiani.

CHANZO CHA UGOMVI
“Kuhusu ugomvi kati yao labda ni kuhusu simu, Jumatano iliyopita alipata tenda ya kwenda kumpodoa bibi harusi Shinyanga. Alipofika huko wakati akiwa kwenye kazi mume akawa anapigapiga simu, Swalha akawa anamwambia asimpigie kwa kuwa yupo kwenye kazi.

“Ijumaa jioni akawa anamtafuta hivyohivyo na kumsisitiza arudi nyumbani, Ijumaa hiyohiyo jioni akarudi akafika nyumbani usiku, mume akawa anapiga simu, Swalha akapokea na kumwambia anaomba apumzike kwa kuwa amepodoa watu wengi na amesimama muda mrefu hivyo amechoka.

“Mwanaume akawa anaendelea kupiga simu usiku huohuo, Swalha akalala, alikuja kushtuka saa tisa usiku akakuta miss call 42. Akampigia alivyopokea wakaanza kukwaruzana tena, mwanaume akawa analalamika na kumfokea alikuwa wapi na anafanya nini mpaka hapokei simu.

“Swalha alivyoona wanazidi kugombana akaamua kuweka simu pembeni ili ugomvi usiwe mkubwa.

“Asubuhi yake mume wake akanipigia simu na kusema kuwa mke wake amemjibu vibaya. Kwa hiyo ndio akapanga kurudi Mwanza.

“Baba yake alivyomuita hapa nyumbani nadhani alitaka wazungumze kuhusu hilo, lakini ikatokea wamepishana na mume alivyofika nadhani ugomvi utakuwa uliendelea.

KUHUSU KUPIGWA RISASI
“Taarifa ni za kweli, pale ndani (wanapoishi Swalha na mumewe) kulikuwa na watoto watatu wametuambia risasi zilipigwa.

“Wanasema huyo baba alikuwa na kawaida ya kuijaribu silaha yake, mara nyingine anapiga hewani, hivyo walivyosikia mlio wa risasi wakawandelea kulala.

“Ni hadi waliposikia Swalha amepiga kelele mara moja tu lakini risasi zikawa zinaendelea kupigwa. Mtoto mmoja akaenda kusikiliza mlangoni kwa Swalha kisha akatoka mbio kwenda kwa kuwataarifu majirani.

“Wakaenda Polisi, kumbe yule mtoto alivyotoka tu yule baba naye (mume wa Swalha) akaondoka. Polisi walivyofika wakauchukua mwili wa Swalha.

“Taarifa za tukio sisi tulianza kuzipata kutoka Kisiwani huko anapofanyia kazi (mume wa Swalha), ndipo majirani wa Swalha na askari wakaja kutoa taarifa wakisema mwanangu ana hali mbaya ameshambuliwa kwa risasi.

“Baba Swalha akaondoka na ndugu zangu kwenda huko maana nilibaki nyumbani, niliishiwa nguvu baada ya taarifa hizo, nikashindwa kwenda, saa tisa usiku wakarejea na ndipo nikajulishwa kuwa Swalha ameshafariki dunia.

“Marehemu hakuwa na mtoto na sijajua nini kinaendelea mpaka sasa.

“Kuhusu huyo mume wake haijulikani yuko wapi, kwani Polisi mara ya mwisho walisema wameangalia simu yake ikaonekana yupo maeneo ya Tunza.”

JESHI LA POLISI LINAMSAKA MTUHUMIWA
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi ni kuwa ni kweli tukio hilo limetokea kutokana na mgogoro wa ndani wa kifamilia na mtuhumiwa ametoroka, anaendelea kusakwa kwa kuwa alitoroka baada ya tukio.

Kuhusu madai kuwa mtuhumiwa ni mtu wa usalama kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema sio kweli, ni mvuvi na anamiliki silaha yake kihalali. Jina lake halijatajwa kutokana na sababu maalum.

إِنّا للهِ وَإِنَا إِلَـيْهِ رَاجِعُـونَ
Inna Lillahi wa inna ilayhi raaji'uun
 
Wapi umesoma Swalha alikuwa Malaya ?
Huna habari aliachika kwa umalaya wake kwenye ndoa ya kwanza, badala ya kujifunza akaendeleza ushenzi wake na dharau juu.

Ngosha akasema liwalo na liwe amekipata alichokipata, halafu humu ndani mnajazana ujinga ndio maana % kubwa humu mmeachika wachache sana wanajitambua na hutoona wakiunga tabia chafu kama za huyo marehemu.
 
Unaleta ukaid utapigwa tu HV nae jama anakuwaje. Na shamaba lenye migogoro hyo kitu tuachane nayo
 
Ukisikiliza maelezo ya mama mkwe inaonyesha Binti hakuwa tayari kuolewa bali jamaa labda sababu ya uzuri wa binti akaforce ndoa na influence ya pesa ikamvutia mwanadada...

tayari hapo utaona ilikuwa ndoa ya bahati mbaya sio watu wawili waliolidhiana....mmoja alipenda kuoa pambo kwa ajili ya show off, mwingine alipenda kuolewa kwa sababu ya pesa...
Umeandika vitu ambavyo nilikuwa nawaza pia
 
Huna habari aliachika kwa umalaya wake kwenye ndoa ya kwanza, badala ya kujifunza akaendeleza ushenzi wake na dharau juu.

Ngosha akasema liwalo na liwe amekipata alichokipata, halafu humu ndani mnajazana ujinga ndio maana % kubwa humu mmeachika wachache sana wanajitambua na hutoona wakiunga tabia chafu kama za huyo marehemu.
Jamaa kazingua kuua, inagharimu mambo yake, vyombo vya usalama havijui habari za umalaya. Mwamba kazingua naamini alimchomoa huyo manzi kwenye mazingira tata najua alikuwa anajua demu wake ni namna gani .. ali fail, mahala pa kupiga na kusepa yeye kaweka kambi kosa hilo mwamba alifanya, sasa ina gharimu mambo yake
 
Hawa viumbe kila siku hawasikii..kuna yule mwingine alichomwa na magunia mawili ya mkaa
 
Mmmmmhhhhhhh mjadala inaonekana wanaume mnavutia upande wenu....


Hakuna JUSTIFICATION WHATEVER ya kukufanya utoe uhai wa mwenzako...


Mrudishe ulikomtoa mtoto wa watu maana uliupende Uzuri wake hukuangalia TABIA wala majibu yake na ulikubaliana Naye wakati wa uchumba LEO kaingia kwenye NDOA UNALETA WIVU NA KUMWEKEA MIPAKA!!!!! Utakuwa na akili sawasawa????

Ukimkuta binti wa watu anapenda kwenda NIGHT CLUBS na ukamwoa katika mazingira hayo hayo BASI JUA UKIINGIA KWENYE NDOA NA UKATAKA ABADILIKE BASI NI MKATABA MWINGINE NA MNATAKIWA KUKAA MEZANI......


Yaani kuna watu wakati wanatafuta wachumba wanaongozwa na tamaa na hasa kile kitu katikati ya mapaja yao, wakishaoa ndiyo wanaanza kuweka masharti......

Kwakweli kama atanusurika ANYONGWE HADI KUFA na kutuulia mdada mwenzetu...
Maelezo ya mama yanatia shaka... Inaonekana clearly huyo mwanamke ana shida.

Mambo ya kuolewa halafu unaenda enda kwenu huagi ni ujinga.

Mtaendelea kumiminiwa za kichwa msipotia akili.
 
Huyu mwanaume nalog of kwa kumuita jina nililolitohoa kwenye "simba wa tsavo" anaitwa "nyamaume"
 
Asubuhi yake mume wake akanipigia simu na kusema kuwa mke wake amemjibu vibaya.

Nafikiri shida yote ilianzia hapa,, K I B U R I na lingine ni U J E U R I.

Japo hatua aliyochukua jamaa ni mbaya lakini kwa wengine mliokimbilia kuolewa mjifunze kitu kupitia mwenzenu huyu...

Hakuna Mwanaume anaweza vumilia Kiburi au Ujeuri..,,,nakazia tena HAKUNA...

Maua hunyauka, stori huisha, kumbukumbu husahaulika, hii inamaanisha Duniani sote tunapita, Maneno mkuki ila Heshima ni ngao,, na Upendo ndio nguzo Kuu...Mwanamke usiidharau Nazi,,Embe ni tunda tu la msimu.

R. I. P Dada yetu..
 
Back
Top Bottom