Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Kwa wivu wa kijinga wa yule jamaa alitakiwa afanye hivyo na kama mwanamke angekataa angeachana nae,kuliko hivyo alivyofanya
Mwanaume kuwa na wivu kuelekea mwanamke wako ni ujinga...stress zote hizi ni za kujitakia tuu. Wewe hapa duniani hamna mbususu yako peke yako. Kwani huyo mwanamke alimuoa akiwa bikra?
 
Kwa wivu wa kijinga wa yule jamaa alitakiwa afanye hivyo na kama mwanamke angekataa angeachana nae,kuliko hivyo alivyofanya
Mimi nilimuachisha kazi mapema kabisa, maana unakuta mtu yupo busy kutwa maofsini na kupewa oder mbalimbali na mabosi wake afu unakuta mshahara wenyewe labda ni 300K hela ambayo wewe unaiiingiza mara 15 ( 4.5M), ya nini sasa?

Nilimfanya akawa mama wa nyumbani mwaka wa 9 huu na kila kitu kinaenda sawa.
 
Kama alijaribu hivi na binti akagoma angefanya namna ya kuachana nae,nacho mlaumu huyu mwamba ni kuoa mwanamke maarufu wakati ana wivu wa hatari hivi
Jamaa alizingua mno.

Ila wale watu wa visiwani huwa na ushirikina mno unaweza kuta waliona wampoteze jamaa kupitia wanawake. Mengine ya visiwani hayawezi kusemwa huku. Ila tambua huko ziwani kuna ushirikina mno.
 
Hiyo clip iko wp!
Mwanza. Mtoto mwenye umri wa miaka 15 (jina linahifadhiwa) amesimulia jinsi alivyobaini mwili wa dada yake, Swalha Salum (28) ukiwa kitandani ukivuja damu baada ya kupigwa risasi.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwao eneo la Kirumba jijini Mwanza, mtoto huyo amesema kabla ya kuingia chumbani na kuukuta mwili huo, yeye na mwenzake waliokuwepo nyumbani muda huo walisikia milio ya risasi kadhaa.

Anasema kabla ya tukio hilo lillilotokea usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022, marehemu dada yake na mume wake aliyemtaja kwa jina la Said Oswayo walikuwa na ugomvi huku sauti za majibizano zikisikika kutoka chumbani kwa wanandoa hao waliofunga pingu za maisha Desemba 31, 2021.

"Mimi na msaidizi wetu wa nyumbani tulikuwa tukiandaa chakula cha usiku. Tuliwasikia wakizozana kwa karibia nusu saa ndipo tikasikia milio ya kwanza ya risasi. Nilikimbilia chumbani kwao na kubisha hodi lakini hakukuwa na jibu nikaamua kuondoka," anasimulia mtoto huyo

Anasema muda mfupi baada ya milio ya kwanza ya risasi, kulisikika milio mingine na aliporejea tena kugonga mara ya pili mlango wa chumbani kwa wana ndoa hao, shemeji yake alitoka na kumtuliza kuwa hakuna tatizo na kumtaka kuendelea na shughuli zake.

"Shemeji aliniambia wana mkwaruzani kidogo kutokana na dada ambaye sasa ni marehemu kutopokea simu yake zaidi ya mara 37," anasema


Anasema baada ya maelezo hayo ya shemeji yake, aliamua kurejea jikoni lakini ghafla zikasikika milio zaidi ya risasi huku msaidizi wao wa ndani akimshauri waondoke eneo hilo, ushauri ambao aliupinga kwa kuhofia usalama wa dada yake aliyekuwa chumbani kunakosikika milio ya risasi.

"Niliporudi jikoni nikakaa kidogo tukasikia tena risasi nikatulia, nikasikia tena ya nne nikatulia jikoni ningetoka pale huenda shemeji angekuwa na hasira na mimi angenipiga, nikatulia kimya baada ya kusikia mtu anafungua mlango kuchungulia nikaona shemeji anafungua mlango akiwa ameshikilia Bastola mkononi," anasema na kuongeza

"Nilipoona hivyo niliingiwa na hofu ya usalama wa dada na kukimbilia chumbani ambako nilimkuta amelala kitandani akivuja damu nyingi,"

Anasema alikimbilia nyumba ya jirani kuomba msaada lakini walisita kufika wakidai shemeji yake ambaye ni mtuhumiwa na mauaji hayo aliwazuia majirani kuingilia migogoro kati yake na mkewe.

"Baada ya kukosa msaada kwa majirani, niliwakimblia madereva wa pikipiki ambao walitoa msaada wa kumkimbiza hospitali Bodaboda watusaidie kupiga simu polisi waliofika muda mchache na kumkimbiza hospitali.

Wakati ndugu wakielezea uwepo wa mgogoro wa muda mrefu kati ya wana ndoa hao, Chanagenge Kilosa, mmoja wa marafiki wa mtuhumiwa Oswayo ameiambia Mwananchi kuwa hajawahi kusikia taarifa zozote za ugomvi huo.

"Mimi na Oswayo tumekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 10 sasa; sijawahi kusikia taarifa zozote kuhusu mgogoro tangu walipofunda ndoa. Hili tukio limetuacha na maswali mengi," amesema Kilosa

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea ikiwemo kumsaka mtuhumiwa aliyetoweka baada ya kudaiwa kufanya mauaji hayo.

"Polisi tunaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo ikiwemo msako dhidi ya anahetuhumiwa kuhusika na mauaji hayo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa uchunguzi zaidi," amesema kaimu Kamanda huyo

Kuhusu idadi ya risasi, Kamanda Makori amesema Jeshi la Polisi litatoa taarifa za kina baada ya uchunguzi wa awali wa mwili wa marehemu kukamilika.
 
Ilipaswa amuachishe,na amtengenezee biashara za kuwa eneo moja kila siku
Kwa vyovyote vile jamaa alitia mpunga mzito kwenye biashara za huyo mdada ..!! Nigga penzi lili-mdrive crazy Sana , Kwa wajanja wa mjini demu wa hvyo huoi , kila mtu na mishe zake mnakutana unapiga mzigo unachora , sku mmezaa na mtoto mmeshibana sasa ndo unasogeza ..demu hajatotoa unamwingiza ndani wa nini , af miez Mitano yote hajavimba tumbo , mtu mwenyewe kutwa Photoshop lazima wenye verosa wapite nae tuu, we kutwa nzima upo ziwani unakimbizana na samaki
 
Sipendi mwanaume anayependa kupitiliza!wanakuwa weak sana
Kikubwa usile hela zake tu, we kama humpendi muweke wazi, sio kumtumia kama ngazi ilhali unajua humpendi au kama unataka hela zake mwambie akununue tu ili mkimaliza kila mtu apite na zake (mnakuwa https://jamii.app/JFUserGuide mates)

Mkuwa hivyo mambo yatakuwa marahisi sana.
 
Sasa waoaji ndio waweke ndani ng'ong'ozo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mbona hii kama kampeni ya wale sura personal kupata ndoa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sio kampeni huu ndio ukweli. Alafu sijataja sura personal hayo ni yako [emoji23]
 
Slay queen kuvimba tumbo sio swala rahisi maana huwa wanaona kama inawashusha hadhi kwenye tasnia yao ya udangaji.
 
Ni kama hoja yako imebeba ubaguzi fulani ndani yake kwani wanawake wazuri wana nini tatizo wanaume ukioa mke mzuri ukua unamchunga sana na wivu sana matokeo yake ndo kama hayo masuala ya kitabia hayatokani na uzuri ispokua malezi kabla hujaoa angalia kwanza miendo ya mtu unaetaka kumuoa.
 
Duhh!! Hujampa hata kabiashara tu hapo hapo nyumbani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…