Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Kila mtu na aoe kama anaweza kuish na mtoto wa wato ila kama mtu unaona huwez bora uwe alone kuliko kutenda hayo madhambi mbele za mwenyez Mungu pia ukosea jamuhuri.
Pia napenda kutoa usia kwa wakuu wenzangu umiliki wa silaha n mzuri ila mtu unapaswa kujua umemiliki jin na lipo ndani yako, likichoka kula unga litataka damu
 
IMG-20220531-WA0101.jpg
 
Nyinyi kuzitafuta hamuwezi ila za kupewa na watu wanaovuja jasho lao mnapokea meno yote nje afu unaziita "hela gani".?

Wanawake wengi humu Jf hawana hata uhakika wa kuingiza 10k tu kwa siku, na hata wanaoweza wengi wao unakuta ni kwa shughuli za kijinga au unakuta wanategemea wanaume wao , ila ndo hawahawa eti hawataki watawaliwe na wanaume.

Mtakaangwa sana.
Duuuh
 
Samahanini kidogo, japo ni jambo la msiba na huzuni.

Nina swali moja, hivi mshawahi kusikia mtu mwenye mke zaidi ya mmoja kaua mkewe ?
Imetokea zanzibar tena miezi ya karibuni. Mume alimuua mke mdogo kwa visu.

Ila huyu ni suspect. Maana dada alikutwa keshakufa chumbani kwake asubuhi na mapema.

Mwanzoni akakamatwa msichana wa kazi kwa sababu ilijulikana wapo wao wawili tu, mke na huyo dada wa kazi. Pia kulikuwa na mtt mdogo wa kiume wa huyo mke mdogo.

Lkn baada ya uchunguzi polisi walijua kuwa ile kazi haiwezi kuwa imefanywa na msichana wa kazi mdogo asie na nguvu.

Msichana wa kazi kuhojiwa zaidi ndio akatoa story kuwa mume alikuja pale nyumbani mapema sana kutoka kwa mke mkubwa alipolala. Na akatekeleza azma hio. Maana alipofika alimtuma dada wa kazi dukani wakati anajua fika kuwa mida hizo ni mapema sana maduka kupata yapo wazi ni shida. So ilichkua muda dada wa kazi kurudi dukani. Na alipofika ndio akamkuta yule mume na kisu kilo kuwa na damu na kuamrishwa akisafishe na amkoshe na mtt pia maana nae alikuwa nguo zake zimeingia damu. Baada ya hapo akamwamrisha pia amsaidie kuweka maiti sawa pale kitandani. Then akasepa na kumwacha dada wa kazi na vitisho juu kuwa akisema kama ni yeye ndie alifika pale naye pia atamchinja.
 
Mbinu ninayofanya ni kumpa hela hela kila mwezi nje ya matumuzi yake kwa kigezo cha kwamba ana nitunzia na siku moja nitazitaka.... "Mama fulani kuna hela nakuwekea uitunze nitakuomba sikumoja". Mwezi huu unampa labda 300K next labda 500K au 450K sometimes hata 600K kabisa, kulingana na ninavyojisikia tu.

Hii inasaidia asiwe mfuja mali kwakua anajua nimempa anitunzie, kumbe me ndo nampa mazima hivyo.


Nafanya hivyo kwasababu nilishajaribu kumfungulia bakiashara kadhaa ila anashindwa kuziendeleza.

NB: Bora hivi kuliko nikose huduma zangu za kuume kwa mwanamke eti kisa yupo kazini anatumwa na wanaume wengine kwa mshahara wa 300K au 400K.

KINACHONIMALIZA MIMI NI BETTING (KAMARI)
Hapo sawa
 
Kama alijaribu hivi na binti akagoma angefanya namna ya kuachana nae,nacho mlaumu huyu mwamba ni kuoa mwanamke maarufu wakati ana wivu wa hatari hivi
Mkuu wanawake bahadhi wanachangamoto kwelikweli, yaani kama una hasira kama hizi za kwangu ni kutoka na kurudi baadaye ukute hali ya hewa imetulia. Vinginevyo unaweza fanya kosa kubwa sana la kujutia maisha yote.
 
Kwanza marehemu Said alikuwa kolo Sana,Hana exposure,yaani akajua hapa duniani huyo swala ndio mwisho hakuna wanawake wengine!..na Nyie wanaume wa humu wote mnajifanya kumsupport Said hamna exposure Kama marehemu...Maisha Ni zawadi nzuri tuliyopewa huwezi poteza uhai wako kisa mtu wakati Kuna mamilioni ya watu ulimwenguni,,eti alikuwa anampa hela kwa hela gani Bwana za kumtoa mtu uhai?kwa hiyo mitumbwi ya mbao?Sasa Kama issue Ni uchungu wa pesa Bill gate itabidi atumie Nukes

Hebu itazame hivi: Mwamba ameacha mamilioni ya wanawake huko ameamua kuinvest kwako halafu wewe unamkosea heshima unaenda kulewa na kujitombesha bure kwa wahuni, tena nahisi risasi ziliisha tu angekula hata ishirini huyo fala
 
Mmh, haiwezekani, yaani mtu ajiue halafu ajitupe kwenye ziwa? Alijibebaje? Hapo kuna mtu alitaka kumuua mkewe na kumframe yeye kama amekombia, kumbe na yeye kauwawa na kutupwa ziwani.

UCHUNGUZI UFANYIKE!!
Nafanya ila mpaka sasa nmefiki 80%
 
Mwanza. Mtoto mwenye umri wa miaka 15 (jina linahifadhiwa) amesimulia jinsi alivyobaini mwili wa dada yake, Swalha Salum (28) ukiwa kitandani ukivuja damu baada ya kupigwa risasi.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwao eneo la Kirumba jijini Mwanza, mtoto huyo amesema kabla ya kuingia chumbani na kuukuta mwili huo, yeye na mwenzake waliokuwepo nyumbani muda huo walisikia milio ya risasi kadhaa.

Anasema kabla ya tukio hilo lillilotokea usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022, marehemu dada yake na mume wake aliyemtaja kwa jina la Said Oswayo walikuwa na ugomvi huku sauti za majibizano zikisikika kutoka chumbani kwa wanandoa hao waliofunga pingu za maisha Desemba 31, 2021.

"Mimi na msaidizi wetu wa nyumbani tulikuwa tukiandaa chakula cha usiku. Tuliwasikia wakizozana kwa karibia nusu saa ndipo tikasikia milio ya kwanza ya risasi. Nilikimbilia chumbani kwao na kubisha hodi lakini hakukuwa na jibu nikaamua kuondoka," anasimulia mtoto huyo

Anasema muda mfupi baada ya milio ya kwanza ya risasi, kulisikika milio mingine na aliporejea tena kugonga mara ya pili mlango wa chumbani kwa wana ndoa hao, shemeji yake alitoka na kumtuliza kuwa hakuna tatizo na kumtaka kuendelea na shughuli zake.

"Shemeji aliniambia wana mkwaruzani kidogo kutokana na dada ambaye sasa ni marehemu kutopokea simu yake zaidi ya mara 37," anasema


Anasema baada ya maelezo hayo ya shemeji yake, aliamua kurejea jikoni lakini ghafla zikasikika milio zaidi ya risasi huku msaidizi wao wa ndani akimshauri waondoke eneo hilo, ushauri ambao aliupinga kwa kuhofia usalama wa dada yake aliyekuwa chumbani kunakosikika milio ya risasi.

"Niliporudi jikoni nikakaa kidogo tukasikia tena risasi nikatulia, nikasikia tena ya nne nikatulia jikoni ningetoka pale huenda shemeji angekuwa na hasira na mimi angenipiga, nikatulia kimya baada ya kusikia mtu anafungua mlango kuchungulia nikaona shemeji anafungua mlango akiwa ameshikilia Bastola mkononi," anasema na kuongeza

"Nilipoona hivyo niliingiwa na hofu ya usalama wa dada na kukimbilia chumbani ambako nilimkuta amelala kitandani akivuja damu nyingi,"

Anasema alikimbilia nyumba ya jirani kuomba msaada lakini walisita kufika wakidai shemeji yake ambaye ni mtuhumiwa na mauaji hayo aliwazuia majirani kuingilia migogoro kati yake na mkewe.

"Baada ya kukosa msaada kwa majirani, niliwakimblia madereva wa pikipiki ambao walitoa msaada wa kumkimbiza hospitali Bodaboda watusaidie kupiga simu polisi waliofika muda mchache na kumkimbiza hospitali.

Wakati ndugu wakielezea uwepo wa mgogoro wa muda mrefu kati ya wana ndoa hao, Chanagenge Kilosa, mmoja wa marafiki wa mtuhumiwa Oswayo ameiambia Mwananchi kuwa hajawahi kusikia taarifa zozote za ugomvi huo.

"Mimi na Oswayo tumekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 10 sasa; sijawahi kusikia taarifa zozote kuhusu mgogoro tangu walipofunda ndoa. Hili tukio limetuacha na maswali mengi," amesema Kilosa

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea ikiwemo kumsaka mtuhumiwa aliyetoweka baada ya kudaiwa kufanya mauaji hayo.

"Polisi tunaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo ikiwemo msako dhidi ya anahetuhumiwa kuhusika na mauaji hayo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa uchunguzi zaidi," amesema kaimu Kamanda huyo

Kuhusu idadi ya risasi, Kamanda Makori amesema Jeshi la Polisi litatoa taarifa za kina baada ya uchunguzi wa awali wa mwili wa marehemu kukamilika.
Kuna maisha baada ya kifo.
 
Wachache sana watakulewa ila nidyo hivyo, kuna wapumbavu humu wanajiona ni vidume kweli mikwala mingiii ila ni wajinga na wafyata mikia nje ya keyboard , ila hakuna jambo la kijasiri kama la mwanaume kufanya uamuzi wa kumuacha mwanamke anamtia stress hata kama umetumia hela nyingi kumtunza ni bora umuache kuliko kutoa uhai wa mwanamke na wewe kujiangamiza, kizazi dhaifu sana hichi
Hata kwenye dini tunaambiwa mbabe zaidi na mwenye nguvu ni yule mwenye kuweza kuzizuia hasira zake.

Na mara nyingi ukiwa mpole na mstaarabu baada ya kuudhiwa karma ndio inakuwa mlipaji wako wa kisasi. Muhimu subrah tu
 
Ni kama hoja yako imebeba ubaguzi fulani ndani yake kwani wanawake wazuri wana nini tatizo wanaume ukioa mke mzuri ukua unamchunga sana na wivu sana matokeo yake ndo kama hayo masuala ya kitabia hayatokani na uzuri ispokua malezi kabla hujaoa angalia kwanza miendo ya mtu unaetaka kumuoa.
Mkuu kuna wanawake ni wa kawaida sana, il nyumba inakuwa kama mko Ukraine, yaani ni moto kila siku. Wengine tuko nao kwenye ndoa zaidi ya miaka 15 ila unatamani sijui uhame tu umuachie hayo makazi.
 
Mtu anawezaje kujiua halafu aende kujitupa ziwani?
Maeneo hayo fukwe imezungukwa na mawe , tena mawe yamo mpak kwenye maji ni rahs mtu kusimama kwenye jiwe akajipiga risasi Kwa vyovyote vile akianguka anaangukia kwenye maji , maeneo haya ni karbu kabisa na mwili ulipokutwa , yawezekana alijongea mpak pande hzi akajilipua

FB_IMG_1653979246442.jpg
 
Mwanaume kuwa na wivu kuelekea mwanamke wako ni ujinga...stress zote hizi ni za kujitakia tuu. Wewe hapa duniani hamna mbususu yako peke yako. Kwani huyo mwanamke alimuoa akiwa bikra?
Tulia dogo unajua maana ya ndoa wewe???
 
Hivi sisi wanaume tumerogwa? hatujui hata mwanamke wa kuowa na mwanamke wa kupita tu? wako wanawake kama unawataka jitahidi uwapitie wanawake sio kila mwanamke wa kuowa na wala sio kila mwanamme wa kuowa ila kama ukiingia kichwa unataka kuowa kama huyo uliyomtaja basi ujuwe utegemee nini usifanye hasira. Jamani fanya makosa yote usifanye kosa kuchagua mke bora huyo sio mke tu atakuwa Mama ya watoto wako. Ndio maana huyo Irene kuna mtu anamchezea tu hakuna harusi hapo.
kuna watu wanahisi ukiwa na hela ndio unapata kila kitu hadi mpenzi wa kweli
 
Mwanaume Umerudi nyumbani mwanamke hayupo na ulimwambia Una njaa ukirudi ukute Amepikaaa... Unafikaa unapiga simu usiku mzima hapokeiiii missed call 42! Baadae mama ake anasema alikuwa amelala anarudi nyumbani unamuuliza anakujibu Shit.. Nasemaa kama wewe huyo ni mkeoo bhasi labda iwe ndo mara ya kwanza kafanya hivyo ila ukute ndio tabiaa yakee bhasi Hasiraa zake sio za kawaidaa.. Kuna jamaa alijua mke wake anachepuka na akapata Uhakikaa alirudi nyumbani akamshikia bastola nusuu amlipuee ila akaishia kupiga mbwa wakee risasi.. sio jambo dogoo hasa kwa mwanamke uliemjali na kumpa kila kitu
Hio sio poa aisee mambo ni moto!
 
Back
Top Bottom