Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Hii ni kama sadaka kwa walio kwenye mahusiano na wanaotaka kuingia kujipanga na kufanya uamuzi sahihi kwa watu wanaotaka kua nao
 
Kupata mwanamke anaekusikiliza na kukuheshimu kama baba yake ni baraka kubwa sana ambayo wengi wanaikosa katika kizazi hiki, Asante Mungu.

Muda mwingine sisi wanaume tunashindwa kusimamia uanaume wetu, hivi Mungu kakujalia Pesa na afya ya nini kung'ang'ania mwanamke anaekuumiza akili?? Najua mapenzi yanauma na pengine labda kuna watu wapo humu jf muda huu wanapitia fukuto la mahusiano, nawashauri mfanye maamzi ya kiume kabla hamjachelewa.


"Every woman in any given reletionship, is taken as the man's project".

Project imekushinda, achia wengine wahangaike nayo kwanini uumie?
Umesema vizuri sana mkuu,kosa tayari ni la mwanaume kaua,lakini ukifuatilia unaweza kukuta mwanamke ndio alikuwa pasua kichwa,ikamfikisha jamaa kuchukua hayo maamuzi,hawa watu tunatakiwa tuishi nao kwa akili sana na kumshirikisha Mungu,kinyume cha hapo usije kumcheka mwanaume mwenzio kwa maamuzi ya majuto aliyoyafanya,kwani hapo shetani na mawakala wake wanahusika kwa asilimia 100......
 
IMG_7255.jpg

huyu mtoto we acha tu.tulio mwanza
 
Hiyo ni akili?!!!
Yaani ulazimike kwenda kukesha kwenye shoo ya kipuuzi kisa mke analazimisha?
Na wao wameambiwa watii waume..
Na pia, tumeambiwa '..mume ni kichwa cha mkewe', meaning maamuzi ya mume ndo yanasimama!
Siungi mkono mauaji, lakini sikubaliani na mke kukaidi maelekezo ya mume.
Sawasawa
 
Kumbuka kila binadamu ana level yake ya ukichaa, kuna point ukimfikisha mtu anakubadilikia na kuwa zaidi ya mnyama. Unadhani wakipewa hizo silaha hawawaangalii mkuu?
Dah....ndiyo maana kwenye mafunzo ya kutumia silaha dhidi ya mwanadamu....mafunzo ya awali huwa ni kutiwa ukichaa....wanaoshindwa huwa na akili timamu...hutemwa 🤣🤣🤣🤣
 
wanaume....muwe makini mtakapo kuoa......wanawake chunguzeni vema hao mnaoamini future husband..........msipende pesa bila kutafakari maisha utayaratibu vipi kwa heshima na upendo......dunia ni uwanja wa fujo......utakavyo cheza ndivyo utachezwa.....RIP SWALHA.....
 
Wakuu story ni kwamba huyu jamaa kwenye picha amemuua huyo mkewe usiku wa kuamkia leo huko Mwanza ikidaiwa ni baada ya kumkataza mkewe asiende kwenye show ya Mondi.

Baada ya kumwambia asiende kwenye hiyo show ya Nasib Abdul, mke akakaidi akaenda.

Jamaa amempiga risasi saba za kichwa na inasemekana na yeye kajiua japo maiti yake haijaonekana.

Ila na nyie Wanawake mpunguze visirani. Inaonesha jinsi huyu Marehemu alikuwa mkaidi na hamsikilizi Mme wake.

Mme kakuambia sitaki uende pahala fulani then wewe unakaidi ni nini kama sio dharau na kiburi?

By the way anything else Happen for a reason.

RIP Binti Mzuri



==================================

Mama mzazi wa marehemu, Bi Tiba Mohamed anasimulia kilichotokea kuhusu ndoa ya mwanaye na mumewe ambao wamedumu katika ndoa kwa muda wa miezi mitano, kwani walifunga pingu za maisha Desemba 30, 2021.

Anasimulia: “Watoto wangu waliitwa na baba yao hapa nyumbani (Mei 28, 2022), walipofika baba yao akapata dharura hivyo hakuzungumza nao nikabaki nao tukawa tunataniana tu.

“Alikuwa akinitania kwa kufurahi kuwafunga Simba akawa anishawishi na mimi nihamie Yanga (Yanga iliifunga Simba bao 1-0 siku hiyo kwenye CCM Kirumba Mei 28, 2022).

“Baadaye baba yake akapiga simu na kusema mume wa Swalha amepiga simu kumjulisha kuwa amefika na hivyo Swalha aende akampokee Igombe.

“Swalha akasema gari yake haina mafuta, hivyo wakakubaliana wakutane nyumbani na mwanaume akasisitiza kuwa ana njaa sana, akamtaka mke wake aende akampikie.

“Nikawasindikiza hadi barabarani mida ya saa moja usiku, muda huohuo mume wake akapiga simu akiwa anafoka, nikamtaka awe na subira mkewe anakuja yupo njiani.

CHANZO CHA UGOMVI
“Kuhusu ugomvi kati yao labda ni kuhusu simu, Jumatano iliyopita alipata tenda ya kwenda kumpodoa bibi harusi Shinyanga. Alipofika huko wakati akiwa kwenye kazi mume akawa anapigapiga simu, Swalha akawa anamwambia asimpigie kwa kuwa yupo kwenye kazi.

“Ijumaa jioni akawa anamtafuta hivyohivyo na kumsisitiza arudi nyumbani, Ijumaa hiyohiyo jioni akarudi akafika nyumbani usiku, mume akawa anapiga simu, Swalha akapokea na kumwambia anaomba apumzike kwa kuwa amepodoa watu wengi na amesimama muda mrefu hivyo amechoka.

“Mwanaume akawa anaendelea kupiga simu usiku huohuo, Swalha akalala, alikuja kushtuka saa tisa usiku akakuta miss call 42. Akampigia alivyopokea wakaanza kukwaruzana tena, mwanaume akawa analalamika na kumfokea alikuwa wapi na anafanya nini mpaka hapokei simu.

“Swalha alivyoona wanazidi kugombana akaamua kuweka simu pembeni ili ugomvi usiwe mkubwa.

“Asubuhi yake mume wake akanipigia simu na kusema kuwa mke wake amemjibu vibaya. Kwa hiyo ndio akapanga kurudi Mwanza.

“Baba yake alivyomuita hapa nyumbani nadhani alitaka wazungumze kuhusu hilo, lakini ikatokea wamepishana na mume alivyofika nadhani ugomvi utakuwa uliendelea.

KUHUSU KUPIGWA RISASI
“Taarifa ni za kweli, pale ndani (wanapoishi Swalha na mumewe) kulikuwa na watoto watatu wametuambia risasi zilipigwa.

“Wanasema huyo baba alikuwa na kawaida ya kuijaribu silaha yake, mara nyingine anapiga hewani, hivyo walivyosikia mlio wa risasi wakawandelea kulala.

“Ni hadi waliposikia Swalha amepiga kelele mara moja tu lakini risasi zikawa zinaendelea kupigwa. Mtoto mmoja akaenda kusikiliza mlangoni kwa Swalha kisha akatoka mbio kwenda kwa kuwataarifu majirani.

“Wakaenda Polisi, kumbe yule mtoto alivyotoka tu yule baba naye (mume wa Swalha) akaondoka. Polisi walivyofika wakauchukua mwili wa Swalha.

“Taarifa za tukio sisi tulianza kuzipata kutoka Kisiwani huko anapofanyia kazi (mume wa Swalha), ndipo majirani wa Swalha na askari wakaja kutoa taarifa wakisema mwanangu ana hali mbaya ameshambuliwa kwa risasi.

“Baba Swalha akaondoka na ndugu zangu kwenda huko maana nilibaki nyumbani, niliishiwa nguvu baada ya taarifa hizo, nikashindwa kwenda, saa tisa usiku wakarejea na ndipo nikajulishwa kuwa Swalha ameshafariki dunia.

“Marehemu hakuwa na mtoto na sijajua nini kinaendelea mpaka sasa.

“Kuhusu huyo mume wake haijulikani yuko wapi, kwani Polisi mara ya mwisho walisema wameangalia simu yake ikaonekana yupo maeneo ya Tunza.”

JESHI LA POLISI LINAMSAKA MTUHUMIWA
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi ni kuwa ni kweli tukio hilo limetokea kutokana na mgogoro wa ndani wa kifamilia na mtuhumiwa ametoroka, anaendelea kusakwa kwa kuwa alitoroka baada ya tukio.

Kuhusu madai kuwa mtuhumiwa ni mtu wa usalama kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema sio kweli, ni mvuvi na anamiliki silaha yake kihalali. Jina lake halijatajwa kutokana na sababu maalum.

View attachment 2243941
Hii pisi mbona kama nilishiaionaga badoo enzi hizo🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom