RIP dada mzuri,
Huyu dada alikua ni make up artist na designer, na ni maarufu mwanza, pia ndoa yao ilikua ina migogoro tangu mda kisa ni Usaliti, mwanamke alikua na jamaa mwingne nje.
Siku ya tukio, Dada na mumewe walienda kwa match ya simba na yanga, baada ya hapo wakarudi home, baadae dada akaomba ruhusa ya kutaka kwenda kuangalia mpira wa UEFA, mumewe akagoma, ktk mabishano bidada akaamua kuondoka kwa kiburi chake.
Sasa kumbe huko kwa Mpira wa UEFA ndo alikua na mchepuko wake, kuna watu walimuona wakamtonya mumewe, machale ya bidada yakamcheza wakaondoka na jamaa ake pale eneo, mumewe alivyofika pale hakuwakuta, kila akimchek kwa cm kimyaa, bidada cm alizima, mumewe akarud home kumsubiri.
Bidada naye baada ya kutosheka huko alikokua na jamaa, akaamua kurudi home, kufika home ndo akakutana na mumewe ktk maulizano bidada akatoa maneno ya kashfa kwa mumewe, mume uvumivu ukamshinda akaamua awashe kitu cha moto, paah paah paaah paaaah paaah, nayeye kusepa hapo hapo.
Marafiki na watu karibu wa huyu dada wanasema alikua anawaambia ukweli kuwa hampendi kwa dhati mumewe, ila yupo nae kwa kuwa ana pesa, na amemsaidia vingi ktk maisha, ila upendo wa dhati kwake hana. Mwishoe ndo haya yaliyotokea.
Mtu km humpendi bora umuache hata km ana pesa, wee kuwa na unaempenda mtafute wote, huku kujidanganya kuwa unaweza fake, matokeo yake ni hataree. Mapenzi yana nguvu mnoo na hayafichiki.
RIP dada mzuri, Tamaa mbele, Mauti nyuma.