Hajafa yupo sana mama Ashirafu ila ni makubwa, mke mkubwa ndo kazaa naye mtoto wakiwa kwenye nyumba za kupanga huku wanajenga hiyo nyumba baada ya nyumba kuisha akapigwa stop kukanyaga huko akanyang'anywa na mtoto huyo Ashirafu akaenda kuishi naye huko kwenye nyumba waliyojenga na akawa anachukuwa wanawake anaishi nao bila ndoa wanamlea huyo mtoto wanashindwana wanaondoka ila Sasa Swalha katika wanawake wake wote ndo alifunga naye ndoa hivyo kuondoka kwake ilihitajika talaka kitu kilicholeta ugomvi, hata bi mkubwa hakuwa na ndoa naye ila alimuzalisha tena mtoto kabla ya kufunga ndoa na Swalha hivyo bi mkubwa akawa na watoto naye wawili bila ndoa.