Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,864
Reaction score
5,254
Mwanaume aliyetambulika kwa jina la Laurent Kweka anatuhumiwa kumuua Mkewe, aliyefahamika kwa jina la Jenipher, kwa kumpiga risasi nyumbani kwao Bunju A, Mtaa wa Mkoani, Zone ya Senzele, Dar es salaam.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Shina la Mtaa wa Mkoani, Lucia Shirima, amesema tukio hilo lilitokea alfajiri ya Oktoba 1, 2026, ambapo alipigiwa simu na Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo aliyemweleza kuwa, “Baba amemuua Mama.”

Shirima amesema baada ya kupokea taarifa hiyo alifika eneo la tukio na kuwasiliana na Viongozi pamoja na Polisi, ambao baadaye walifika katika nyumba hiyo.

Kwa mujibu wa Shirima, walipoingia ndani waliukuta mwili wa Jenipher ukiwa upande wa kushoto, pembeni ya kitanda, huku Mumewe akiwa hayupo eneo la tukio ambapo baadaye alipata taarifa kuwa Kweka alikuwa amekwenda kujisalimisha Polisi.

Jitihada za kupata taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo zinaendelea, na tulipowasiliana kwa simu, tulielezwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro, hakuwepo, huku simu ya Kaimu Kamanda ikiita bila kupokelewa.

Unahisi nini kinasababisha matukio ya ukatili na mauaji kuongezeka ndani ya ndoa na familia zetu siku hizi, na nini kifanyike kuzuia majanga haya?

Video: https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/share/v/189ju9sdmC/
 

Attachments

  • HTp12HFWMAAdJoX.jpg
    317.6 KB · Views: 45
Wanandoa mnapochokana, vyema kuachana kwa amani

Hata kama mna watoto pamoja, bora Mama awe hai na Baba awe hai, hao watoto watawatembelea kwa utaratibu utakaowekwa kisheria

Vinginevyo wanandoa wengi watauana kwa risasi ama sumu 🙌

Afya ya akili
 
Ila ndoa ni nyoko sana na picha za wapenzi mtandaoni tukiwaona wapo kwenye mitoko full tabasamu tunaona wanafaidi kumbe uozo mtupu

Nimefatilia account ya Facebook ya huyo mwanaume na mkewe kwakweli picha zao jinsi walivyo na furaha huwezi amini kama wamgefikia hapa aiseeee ndo maana tunaambiwa tusiyaamini maisha ya mtandaoni🥹🥹imenisikitisha hii
 
Ndugu yangu, tatizo ndoa za under 30 ni Mtihani kweli kweli siku hizi
 
Hizi silaha wakati mwingine inakosekana hata maana ya kumilikisha watu.

Hawajihami dhidi ya majambazi wala vibaka,ni kutishia walevi bar na barabarani,kujiua wenyewe ama kama hivi.
 
Wale waliokuwa wanawaambia " msiachane watoto watateseka" ikitokea tukio kama hili na wenyewe wanaanza kusema" bora mngeachana kwa amani kuliko sasahivi mama kaburini baba jela, watoto watalelewa na nani??"" Mwanandoa mwenzako akianza kukupiga matukio magumu jamani ni bora kukaa mbali nae hasira zipoe. Huyu baba inaonekana hakudhamiria kumuua mkewe ndo maana kaenda kujisalimisha polisi kabisa, hapa unakuta ni makwazo ya miaka mingi yamejaa moyoni, siku ukikasirishwa kidogo tu unalipuka unafanya tukio ambalo hukutegemea.
 
🥹🥹
 

Attachments

  • FB_IMG_1791017350556.jpg
    162.7 KB · Views: 37

Wanawake mnazingua sana,Hapo mwanamke alitaka kuchukua asicho stahili kwenye talaka ,Unaweza fikilia nn mbaya zaidi
 
Mimi sina chochote cha kuhisi kuhusu sababu ya mauaji ndani ya ndoa.Tutafika na jamaa zangu kuhani msiba hapo nyumbani kwa marehemu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…