Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Ila ndoa ni nyoko sana na picha za wapenzi mtandaoni tukiwaona wapo kwenye mitoko full tabasamu tunaona wanafaidi kumbe uozo mtupu

Nimefatilia account ya Facebook ya huyo mwanaume na mkewe kwakweli picha zao jinsi walivyo na furaha huwezi amini kama wamgefikia hapa aiseeee ndo maana tunaambiwa tusiyaamini maisha ya mtandaoni🥹🥹imenisikitisha hii
Hizi nyumba hizi acha tu nahisi malaika wa zamu kulinda duniani kila siku huwa wanajionea mengi sana ya ajabu na kutusikitikia tu.... Kuna vitu vinachemka kwenye mioyo na nyumba za watu hasa wana ndoa, usione tu nyumba zimeezekwa kwa mabati mazuri zimefunika mambo mazito mno ndani, usione watu wana vifua vikubwa (six pack) au nyonyo kubwa ukajua wanafanya mazoezi gym au wamenenepa, kumbe wamebeba mambo mazito vifuani mwao mpaka wanataka kupasuka..
 
Wanandoa mnapochokana, vyema kuachana kwa amani

Hata kama mna watoto pamoja, bora Mama awe hai na Baba awe hai, hao watoto watawatembelea kwa utaratibu utakaowekwa kisheria

Vinginevyo wanandoa wengi watauana kwa risasi ama sumu 🙌

Afya ya akili
Kweli kabisa,inabidi mtu uushinde moyo kubali matokeo,haya sasa jamaa ataishia gerezani
Mambo ya ndoa magumu sana

Ova
 
Wanandoa mnapochokana, vyema kuachana kwa amani

Hata kama mna watoto pamoja, bora Mama awe hai na Baba awe hai, hao watoto watawatembelea kwa utaratibu utakaowekwa kisheria

Vinginevyo wanandoa wengi watauana kwa risasi ama sumu 🙌

Afya ya akili
Tatizo watu wanawaza mali zote zinapigwa pasu halafu njemba nyingine inakuja kuinjoi hela zako
 
Mwanaume aliyetambulika kwa jina la Laurent Kweka anatuhumiwa kumuua Mkewe, aliyefahamika kwa jina la Jenipher, kwa kumpiga risasi nyumbani kwao Bunju A, Mtaa wa Mkoani, Zone ya Senzele, Dar es salaam.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Shina la Mtaa wa Mkoani, Lucia Shirima, amesema tukio hilo lilitokea alfajiri ya Oktoba 1, 2026, ambapo alipigiwa simu na Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo aliyemweleza kuwa, “Baba amemuua Mama.”

Shirima amesema baada ya kupokea taarifa hiyo alifika eneo la tukio na kuwasiliana na Viongozi pamoja na Polisi, ambao baadaye walifika katika nyumba hiyo.

Kwa mujibu wa Shirima, walipoingia ndani waliukuta mwili wa Jenipher ukiwa upande wa kushoto, pembeni ya kitanda, huku Mumewe akiwa hayupo eneo la tukio ambapo baadaye alipata taarifa kuwa Kweka alikuwa amekwenda kujisalimisha Polisi.

Jitihada za kupata taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo zinaendelea, na tulipowasiliana kwa simu, tulielezwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro, hakuwepo, huku simu ya Kaimu Kamanda ikiita bila kupokelewa.

Unahisi nini kinasababisha matukio ya ukatili na mauaji kuongezeka ndani ya ndoa na familia zetu siku hizi, na nini kifanyike kuzuia majanga haya?

Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/189ju9sdmC/

Wanawake muache kucheat.
 
Back
Top Bottom