Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Mwanaume aliyetambulika kwa jina la Laurent Kweka anatuhumiwa kumuua Mkewe, aliyefahamika kwa jina la Jenipher, kwa kumpiga risasi nyumbani kwao Bunju A, Mtaa wa Mkoani, Zone ya Senzele, Dar es salaam.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Shina la Mtaa wa Mkoani, Lucia Shirima, amesema tukio hilo lilitokea alfajiri ya Oktoba 1, 2026, ambapo alipigiwa simu na Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo aliyemweleza kuwa, “Baba amemuua Mama.”

Shirima amesema baada ya kupokea taarifa hiyo alifika eneo la tukio na kuwasiliana na Viongozi pamoja na Polisi, ambao baadaye walifika katika nyumba hiyo.

Kwa mujibu wa Shirima, walipoingia ndani waliukuta mwili wa Jenipher ukiwa upande wa kushoto, pembeni ya kitanda, huku Mumewe akiwa hayupo eneo la tukio ambapo baadaye alipata taarifa kuwa Kweka alikuwa amekwenda kujisalimisha Polisi.

Jitihada za kupata taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo zinaendelea, na tulipowasiliana kwa simu, tulielezwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro, hakuwepo, huku simu ya Kaimu Kamanda ikiita bila kupokelewa.

Unahisi nini kinasababisha matukio ya ukatili na mauaji kuongezeka ndani ya ndoa na familia zetu siku hizi, na nini kifanyike kuzuia majanga haya?

Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/189ju9sdmC/

IMG_5319.jpeg

IMG_5320.jpeg
IMG_5321.jpeg
IMG_5322.jpeg
 
Hizi silaha wakati mwingine inakosekana hata maana ya kumilikisha watu.

Hawajihami dhidi ya majambazi wala vibaka,ni kutishia walevi bar na barabarani,kujiua wenyewe ama kama hivi.
Mara 1000 uishi na Ke kuliko silaha, hekima za kuishi na silaha ni hatari sana kuliko hekima za kuishi na Ke.

Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 
Ndoa kudumu inahitaji mwanamke kuwa submissive. Ndoa za zamani zilidumu kutokana na mama zetu walikua submissive kwa waume zao.

Wanawake wote inabidi waambiwe,
Waulizwe kabla ya ndoa. Ndoa ni ya mwanaume (anapoamua kutafuta mwenza wa kuishi nae) , mwanamke yeye anaolewa ( ana kabidhi mamlaka yake yote kwa mume na anakuwa Mali ya mume).
Waulizwe je wapo tayari kuolewa? Zingatia definition ya kuolewa hapo juu.

Sasa unakuta kwenye ndoa mwanamke nae anagombania Mali wakati anasahau kuwa na yeye ni sehemu ya mali ya mwanaume.
 
Bwana Kweka ameshindwa kudhibiti hasira zake hadi kufikia hatua ya kumuua mkewe, that's too bad.

Tusifike huko wanandoa, mambo yakiwa magumu tupeane nafasi, tutengane na yakishindikana tuachane kaa amani.

Lengo ni kulea hawa watoto pamoja, ila mambo yakiwa magumu hata remotely watalelewa tu.
Ndoa za wakristo huwa hazina talaka mkishaungana ni milele hiyo
 
Namshukuru Mungu sana kwa kunilinda na kuidhibiti hasira yangu muda wote wa ndoa yangu!
... maana, kwakweli wakati mwingine hisia mbaya za kumuumiza mke wangu zilinijaa kichwani kwa sababu ya hasira zilizosababishwa na maudhi ya mke wangu, lakini kwa msaada wa Mungu nilipita!
NAOMBA MUNGU TUMALIZE SALAMA!
 
Ndoa kudumu inahitaji mwanamke kuwa submissive. Ndoa za zamani zilidumu kutokana na mama zetu walikua submissive kwa waume zao.

Wanawake wote inabidi waambiwe,
Waulizwe kabla ya ndoa. Ndoa ni ya mwanaume (anapoamua kutafuta mwenza wa kuishi nae) , mwanamke yeye anaolewa ( ana kabidhi mamlaka yake yote kwa mume na anakuwa Mali ya mume).
Waulizwe je wapo tayari kuolewa? Zingatia definition ya kuolewa hapo juu.

Sasa unakuta kwenye ndoa mwanamke nae anagombania Mali wakati anasahau kuwa na yeye ni sehemu ya mali ya mwanaume.
Ke wa 2000 wana kaupumbavu kao kasemacho "kuoana" kama vile Ke naye ni muoaji, ni ujinga ujinga tu.

Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 
Bwana Kweka ameshindwa kudhibiti hasira zake hadi kufikia hatua ya kumuua mkewe, that's too bad.

Tusifike huko wanandoa, mambo yakiwa magumu tupeane nafasi, tutengane na yakishindikana tuachane kaa amani.

Lengo ni kulea hawa watoto pamoja, ila mambo yakiwa magumu hata remotely watalelewa tu.
Ndoa za wakristo huwa hazina talaka mkishaungana ni milele hiyo
 
Tatizo watu wanawaza mali zote zinapigwa pasu halafu njemba nyingine inakuja kuinjoi hela zako
Sasa hapo alivyomuua hizo mali hawaendi kuzifaidi watu wengine?. Bado na watoto ndo wamekuwa yatima. Si bora hata wangeokoa watoto maana mali zinatafutwa. Mali zimeondoka na watoto wataenda kubaki na majeraha ya milele mioyoni.
 
Back
Top Bottom