Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Kweli kabisa,inabidi mtu uushinde moyo kubali matokeo,haya sasa jamaa ataishia gerezani
Mambo ya ndoa magumu sana

Ova
Wanasema majuto mjukuu, labda itumike hela kuizima hiyo kesi

Otherwise jamaa atafungwa.

Usipokuwa na moyo wa uvumilivu na kuachilia mambo, Kila siku watu watauana, hasa wanapohisi wake/waume zao ni malaika.

Kwamba hawawezi kukoseana
 
Kuachqna sio issu÷. Issue ni hao viumbe kungangania majasho yetu.
Kama umezaa naye, sio mbaya ukampa percentage kubwa ya ulichonacho

Sisi Wanaume ni wapambanaji, hatuwezi kushindwa kutafuta

Kuna jamaa alimwachia mkewe lodge 2 hapo Arusha, nyumba 3 za kuishi...huku yeye akibaki na nyumba 1 tu bila biashara isipokuwa mshahara wake

Baada ya miaka 5, jamaa aliweza kuanzisha kampuni iliyokuwa na returns nzuri kuliko mwanzo

Mkewe alikamatwa na kibenten, akauza nyumba na lodge zote huku akiishia kupanga hapo Ubungo Makuburi 🙌
 
Nipige kama wewe Mwanaume.

Hapo muhanga ni mtoto.
Tena hawa watu wanakuaga na ujinga mwingne, unakuta wanaongea kama kamezeshwa flash, tena ukimgusa ndo kabsa anaboyoka had majiran wanasikia!

Tena kuna wanawake, akikosea hakubali kosa, katakata utapga uue lakn hakubali kosa, tena wakat huo anaongea sana atahakikisha wakat mnaonge, saut yako aipoteze kwa saut yake, hapo mixer ashapga cm kwao kabadr kosa, ukwen uonekane unamuonea wew ndo mbaya!

MUNGU tu atusimamie maana ukifata hasira wanaume wengi tutaenda jera!
 
Sasa mwanaume si ataishia
Kukaa kwenye majengo ya serikali
Huo uamuzi aliyouchukua ni wa kipuz kabisa

Ova
Kuna baadhi ya watu hawawezi kuvumilia dharau mkuu yaani ni bora akae jela kuliko kumletea dharau yaani kwa mfano anakuonyeshea mchepuko wake waziwazi na ukimuuliza anakwambia amua la kufanya na ukicheki mmeshazaa watoto na mnamiliki mijengo na mali zingine na unawaza ukimuacha mtagawana mijengo halafu amlete mchepuko wake amzagamue humohumo ndani hapo ndipo akili hugeuka na kuwa ya kinyama
 
Mwanaume aliyetambulika kwa jina la Laurent Kweka anatuhumiwa kumuua Mkewe, aliyefahamika kwa jina la Jenipher, kwa kumpiga risasi nyumbani kwao Bunju A, Mtaa wa Mkoani, Zone ya Senzele, Dar es salaam.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Shina la Mtaa wa Mkoani, Lucia Shirima, amesema tukio hilo lilitokea alfajiri ya Oktoba 1, 2026, ambapo alipigiwa simu na Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo aliyemweleza kuwa, “Baba amemuua Mama.”

Shirima amesema baada ya kupokea taarifa hiyo alifika eneo la tukio na kuwasiliana na Viongozi pamoja na Polisi, ambao baadaye walifika katika nyumba hiyo.

Kwa mujibu wa Shirima, walipoingia ndani waliukuta mwili wa Jenipher ukiwa upande wa kushoto, pembeni ya kitanda, huku Mumewe akiwa hayupo eneo la tukio ambapo baadaye alipata taarifa kuwa Kweka alikuwa amekwenda kujisalimisha Polisi.

Jitihada za kupata taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo zinaendelea, na tulipowasiliana kwa simu, tulielezwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro, hakuwepo, huku simu ya Kaimu Kamanda ikiita bila kupokelewa.

Unahisi nini kinasababisha matukio ya ukatili na mauaji kuongezeka ndani ya ndoa na familia zetu siku hizi, na nini kifanyike kuzuia majanga haya?

Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/189ju9sdmC/

Wasiojulikana
 
Tena hawa watu wanakuaga na ujinga mwingne, unakuta wanaongea kama kamezeshwa flash, tena ukimgusa ndo kabsa anaboyoka had majiran wanasikia!

Tena kuna wanawake, akikosea hakubali kosa, katakata utapga uue lakn hakubali kosa, tena wakat huo anaongea sana atahakikisha wakat mnaonge, saut yako aipoteze kwa saut yake, hapo mixer ashapga cm kwao kabadr kosa, ukwen uonekane unamuonea wew ndo mbaya!

MUNGU tu atusimamie maana ukifata hasira wanaume wengi tutaenda jera!
Mwanamke akianza hizo mbanga, RUUUN, RUUUN. Hiyo ndo salama yako. Ukibaki yatakukuta yaliyomkuta huyu bwana
 
Back
Top Bottom