Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Mume aliniacha nimefungua Biashara ila nina Mwanaume mwiangine naye kaniletea mtoto!
Hello, kaka Iddi. Habari ya kazi? Naomba ushauri nisiendelee kuharibu zaidi. Niliolewa ndoa ya Kikatoliki, nikazaa na mume wangu watoto watatu. Maisha hayakuwa mazuri sana kwa sababu ya changamoto za kimahusiano, na mume wangu alikuwa ni mwanaume mkorofi, ananipi*ga sana na kunizalia nje, kitu ambacho nilikivumilia kwa miaka 8.
Kuna kipindi mume wangu aliondoka tu na Kwenda kuishi na mwanamke mwingine. Basi nilimua kujiongeza ingawa hakunipa talaka lakini nilianza biashara nikawa nazunguka mikoani! Nilibahatika nikapata mtaji wangu hapa Tanga, na niko tu vizuri, japo watoto wakati nakuja kutafuta maisha, niliwaacha kwao, kwa maana nilitokea kwao, sababu ya matatizo. Nahudumia wanangu vizuri tu kwa mahitaji yao, namshukuru Mungu kwa hili.
Shida inakuja nilipokuja huku Tanga, katika harakati za kutafuta maisha, nilikutana na kijana mmoja, ndiye aliyenishika mkono, tukaanza kupambana wote hadi nilipofanikiwa na kuweza kujisimamia. Huyu kijana naye aliwahi kuzaa, japo hakuoa, alikuwa akihudumia tu mtoto. Sasa huku Tanga, ilibidi tuanze kuishi wote, kwa lengo la kusave kodi, japo kwa usiri, tu kama marafiki.
Changamoto ikaanza, yule mzazi mwenzie akamleta mtoto aje aishi na baba yake. Mtoto ni mdogo, ana umri wa miaka 7. Mimi sikuchukia, maana niliona ni mtoto tu na huko alikuwa akiishi kwa tabu. Shida inakuja, mimi kwa upande wangu, sikutaka familia yangu ijue kama ninaishi na mwanaume, na pia watoto wangu sipendi wajue kama nina mtu nje ya baba yao. Na huyu mwanaume, nikimuuliza kwa nini mtoto asikae kwa mama yake, naye anasema hata mama yake hana malezi mazuri.
Sasa nipo njia panda, natamani kumuacha huyu kaka, nitafute nyumba, nipange, nikae peke yangu, yeye nimuache na mwanae, au sijui nifanyeje, maana naona kama nakosa mwelekeo, ukizingatia tumekimbizana kupambana pamoja, japo hapa tulipopanga, mimi ndio mwenye vitu vyote. Sielewi, naomba unipe ushauri wa busara nisiendelee kuharibu. Nifanyeje?
JIBU LANGU; Kama bado hujapewa talaka na mume wako, wewe bado ni mke wa mtu, hivyo hata ukikaa na huyo mwanaume miaka 10 bado utatakiwa kurudi kwa mume wako. Jambo la pili ni kwamba, ulitakiwa kujifunza kutoka kwa ndoa yako kuwa si kila wakati unatakiwa kumtegemea mwanaume kwa asilimia mia. Mume wako alianza na wanawake wengine na akaamua kukuacha.
Sasa ulipoanzisha biashara, ulitakiwa kujifunza kusimama wewe kama wewe mwenyewe bila kuhangaika na wanaume. Ili uheshimike, usitok katika kumtegemea mwanaume mmoja kwenda mwingine. Usiamini kwamba mwanaume atakubeba kila wakati. Hata kama utaamua kuachana na mume wako, uwe umesimama kama wewe mwenyewe na si kukimbilia kwa mwanaume mwingine ambaye naye katelekeza mwanamke mwingine!
Ushauri wangu, ondoka hapo, pangisha nyumba yako mwenyewe, halafu simama wewe kama wewe kibiashara. Baada ya hapo, kama humhitaji mume wako, dai talaka mahakamani au kwake, kisha kama utataka kuendelea kwenye mahusiano na huyo mtu sawa. Lakini muhimu, sasa ujilinde na uwe na chako ili usije kurudi kuanza sifuri tena.
MWISHO