Mume au mke kubadili dini kutoka ukristo kwenda dini nyingine, je, Kunaifanya ndoa yake ya kanisani kuvunjika kidini na kisheria baada ya kubadili?

Mume au mke kubadili dini kutoka ukristo kwenda dini nyingine, je, Kunaifanya ndoa yake ya kanisani kuvunjika kidini na kisheria baada ya kubadili?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau.

Nimeona watu wengi wanabadili dini zama hizi. hasa wakiwa na migogoro ya ndoa zao.

Reference case ben pol. alifunga ndoa ya kanisani.. then mwaka mmoja mbele akabadili dini kutoka ukristo na kuhamia uislamu. ikasemekana ndoa yake ya awali ya kikristo ilikuwa na mgogoro na imevunjika haraka haraka baada yeye kubadili dini, je ni sahihi?

Inasemekana wanawake wengi wa kikristo huwa hawasapoti ndoa ivunjike kisheria hata kama ndoa imekufa hasa mume akiwa na mali, mahakamani hawatoi ushirikiano wa divorce kabisa na kupelekea divorce kushindikana mfano hai master jay imemchukua zaidi ya miaka 10 kufanya divorce.. ama yule bwana wa mbunge magige aliyeleta seke seke kwenye mazishi., je mbinu ya kubadili dini inavunja ndoa kisheria?

Wanasheria ni vizuri mkatoa majibu, ili wakristo ambao bado hatujafunga ndoa na maskini, tujue mpema siku tukipata mali ama utajiri tuwe makini kujua tunafunga ndoa zenye sheria gani

1. Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania ya mwaka 1970 (kama ilivyofanyiwa marekebisho hadi 2019) moja ya vipengere vinavyoonyesha kuwa ndoa imevunjika na haiwezi kurekebika ni pale ushahidi unapoonyesha kuwa mlalamikaji amebadili dini wakati ilipofungwa wanandoa walikuwa dini moja na kwa mujibu wa dini yao kubadilisha dini kunafanya ndoa yao isiwepo tena au ni moja ya sababu zinazofanya ndoa yao isiwepo. Soma sura ya 107(2)(i).

2. Kwa sheria za kidini, mfano kwa upande wa Kanisa Katoliki, ndoa (iliyofungwa kanisani), ambayo imevunjwa kiserikali (mahakamani) itaendelea kuwa ndoa halali machoni pa kanisa hadi hapo utakapotikana ushahidi mbele ya mahakama ya Kanisa kwamba kabla ya kufunga ndoa, wanandoa au mmojawapo hakuwa na uhuru (hakuridhia) kufunga ndoa, mmojawapo au wanandoa wote wawili walidanganya ili ndoa ifungwe wakati wakijua kwamba kama wasingedanganya isingefungwa kanisani, kama wanandoa ni ndugu wa damu (are within prohibited relationship) au kama wakati wa kufunga ndoa mmoja au wanandoa wote wawili walikuwa na ndoa ingine halali au walikuwa wanafungwa na maagano mengine (kwa mfano mmojawapo alikuwa padri hata kama ameecha, lakini hajafuata utaratibu wa kuvuliwa upadri).

Nje ya sababu hizo, ndoa iliyofungwa kanisani (Kanisa Katoliki) itaendelea kuwa ndoa halali kwa sababu kwa mujibu wa Kanisa Katoliki 'alichounganisha Mungu (ndoa iliyo halali) mwanadamu hawezi kutenganisha/kuitengua isipokuwa kifo'. Kanisa linaamini wanaofunga ndoa halali si wawili tena bali Mungu huwafanya kuwa mwili mmoja na ndoa yao si tu ndoa, bali ni sakramenti (alama wazi inayoonekana inayoonyesha neema ya Mungu isiyoonekana).

Dini zingine nadhani hazina msimamo kama huu na kutokana na matatizo waliyonayo wanandoa, huenda ndoa inaweza kutenguliwa. Kwa Kanisa Katoliki wanandoa wanapofunga ndoa wanaahidi kuishi pamoja kwa upendo na uvumilivu "wakati wa neema na matatizo hadi kufa". Kwa mantiki hii, matatizo yanayojitokeza baadaye kama ndoa waliyofunga ilikuwa halali hayahalalishi ndoa halali kutenguliwa (hayabatilishi) hata kama wanandoa wataamua wao wenyewe kuachana na kila mmoja kuamua kufunga ndoa ingine na mtu mwingine (kwa mfano wale ambao ndoa yao imetenguliwa mahakamani). Hivi ndivyo ninavyoweza kujibu swali lako.
 
Ukiwa na ndoa ya halali ya dini nyingine ikitokea mmoja wenu kahamia kwenye uislamu hasa mwanaume ndoa inaendelea kutambulika, isipokuwa kwa wakristu ile ndoa inakuwa batili ,mwanamke moja kwa moja anakuwa hana ndoa.

Mwanaume anakuwa na ndoa halali ila mwanamke inakuwa ndoa batili kivipi?
 
Ninavyoelewa ndoa ikishafungwa iwe katika dini yeyote,hapo tayari hutambulika kisheria.Mmoja kuhama dini haiathiri ndoa hiyo kwa kuifanya batili,ndoa huvunjwa mahakamani tu.
 
1. Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania ya mwaka 1970 (kama ilivyofanyiwa marekebisho hadi 2019) moja ya vipengele vinavyoonyesha kuwa ndoa imevunjika na haiwezi kurekebika ni pale ushahidi unapoonyesha kuwa mlalamikaji amebadili dini wakati ilipofungwa wanandoa walikuwa dini moja na kwa mujibu wa dini yao kubadilisha dini kunafanya ndoa yao isiwepo tena au ni moja ya sababu zinazofanya ndoa yao isiwepo. Soma kifungu 107(2)(i).

2. Kwa sheria za kidini, mfano kwa upande wa Kanisa Katoliki, ndoa (iliyofungwa kanisani), ambayo imevunjwa kiserikali (mahakamani) itaendelea kuwa ndoa halali machoni pa kanisa hadi hapo utakapotikana ushahidi mbele ya mahakama ya Kanisa kwamba kabla ya kufunga ndoa, wanandoa au mmojawapo hakuwa na uhuru (hakuridhia) kufunga ndoa, mmojawapo au wanandoa wote wawili walidanganya ili ndoa ifungwe wakati wakijua kwamba kama wasingedanganya isingefungwa kanisani, kama wanandoa ni ndugu wa damu (are within prohibited relationships) au kama wakati wa kufunga ndoa mmoja au wanandoa wote wawili walikuwa na ndoa nyingine halali au walikuwa wanafungwa na maagano mengine (kwa mfano mmojawapo alikuwa padri hata kama ameacha, lakini hajafuata utaratibu wa kuvuliwa upadri).

Nje ya sababu hizo, ndoa iliyofungwa kanisani (Kanisa Katoliki) itaendelea kuwa ndoa halali kwa sababu kwa mujibu wa Kanisa Katoliki 'alichounganisha Mungu (ndoa iliyo halali) mwanadamu hawezi kuitenganisha/kuitengua isipokuwa kifo'. Kanisa linaamini wanaofunga ndoa halali si wawili tena bali Mungu huwafanya kuwa mwili mmoja na ndoa yao si tu ndoa, bali ni sakramenti (alama wazi inayoonekana inayoonyesha neema ya Mungu isiyoonekana).

Dini zingine nadhani hazina msimamo kama huu na kutokana na matatizo waliyonayo wanandoa, huenda ndoa inaweza kutenguliwa. Kwa Kanisa Katoliki wanandoa wanapofunga ndoa wanaahidi kuishi pamoja kwa upendo na uvumilivu "wakati wa neema na matatizo hadi kufa". Kwa mantiki hii, matatizo yanayojitokeza baadaye kama ndoa waliyofunga ilikuwa halali hayahalalishi ndoa halali kutenguliwa (hayabatilishi) hata kama wanandoa wataamua wao wenyewe kuachana na kila mmoja kuamua kufunga ndoa nyingine na mtu mwingine (kwa mfano wale ambao ndoa yao imetenguliwa mahakamani). Hivi ndivyo ninavyoweza kujibu swali lako.
 
Ninavyoelewa ndoa ikishafungwa iwe katika dini yeyote,hapo tayari hutambulika kisheria.Mmoja kuhama dini haiathiri ndoa hiyo kwa kuifanya batili,ndoa huvunjwa mahakamani tu.

Kwa case kama ya ben pol mfano. Amefunga ndoa ya kikristo kisha akabadili dini na kuhamia uislamu, then akafunga ndoa ya kiislam na binti mwingine wa kiislam kabla ya mahakama kutoa talaka ndoa yake ya dini ya awali ya ukristo. Je ndoa zote zinakuwa na uhalali kisheria? Wake wote wawili wanakuwa wake halali?
 
Nadhani kisheria ndoa ya pili sio halali(watu wa sheria watupe uhakika) kama ndoa ya kwanza haikuvunjwa kisheria au kama hakukuwa na sababu ya ndoa ya kwanza ionekane haipo au sababu ya kisheria kumruhusu afunge ndoa ya pili.Lakini pia labda hatufahamu undani wa ndoa yake ya kwanza na hata hiyo ya pili.
 
Ukiwa na ndoa ya halali ya dini nyingine ikitokea mmoja wenu kahamia kwenye uislamu hasa mwanaume ndoa inaendelea kutambulika, isipokuwa kwa wakristu ile ndoa inakuwa batili ,mwanamke moja kwa moja anakuwa hana ndoa.
Ungetaja dhehebu. Si wakristo wote wana mtazamo kama wako.
Serikali (Sura ya 29 ya katiba) inatambua ndoa (1)Kiislamu (2)Kikristo (3)Kimila.
 
Kwa case kama ya ben pol mfano. Amefunga ndoa ya kikristo kisha akabadili dini na kuhamia uislamu, then akafunga ndoa ya kiislam na binti mwingine wa kiislam kabla ya mahakama kutoa talaka ndoa yake ya dini ya awali ya ukristo. Je ndoa zote zinakuwa na uhalali kisheria? Wake wote wawili wanakuwa wake halali?
Hapa watu wanachanganya kati ya dini na sheria mfano hata ukifunga ndoa kanisani mahakama inatoa talaka lakini kanisa halitambui talaka inatambua ndoa moja tu, kwa swala la benpol kama hajaachana na mke wa awali basi uislamu unamtambua mke wake wa kwanza kama mke wake wa halali na kama hawajaachana. Lakini kwa upande wa mke wa benpol kwenye ukristo ndoa yao inabatilishwa.
Ila kimahakama kama hajampa mke wake wa awali talaka ndoa zake zote zinatambulika.
 
Je mke wa pili ambaye amemuoa kwa ndoa ya kiislam baada ya ben pol kubadili dini? Nae anatambulika kama mke halali? Ama ndoa yake inakuwa haitambuliki kisheria sababu mwanaume ana ndoa ya kwanza ya kikristo ambayo haijavunjwa na mahakama? Je ndoa ya pili ya ben pol ya kiislam mke anakuwa na haki kisheria?
 
Ndoa ya pili itatambulika kidini na kisheria , kwenye cheti benpol kitajazwa ndoa ya mke zaid ya mmoja .
 
Swali lako liko so complex..

Kuna sheria za ndoa zaidi ya moja..

Mfano mkioana Bomani kiserikali ndoa hazivunjiki kwa sahani ya dini..
Ndoa inavunjwa kwa mmoja kudai talaka mahakamani
 
Ndoa ya pili itatambulika kidini na kisheria , kwenye cheti benpol kitajazwa ndoa ya mke zaid ya mmoja .
Nadhani kisheria ndoa ya pili sio halali(watu wa sheria watupe uhakika) kama ndoa ya kwanza haikuvunjwa kisheria au kama hakukuwa na sababu ya ndoa ya kwanza ionekane haipo au sababu ya kisheria kumruhusu afunge ndoa ya pili.Lakini pia labda hatufahamu undani wa ndoa yake ya kwanza na hata hiyo ya pili.

Why ndoa ya pili inakuwa sio halali. Huku dini mpya aliyohamia ben pol inaruhusu ndoa mpaka 4.

Ama sheria hairuhusu watu wabadili dini?

Ama hata ukibadili dini sheria hairuhusu kufata taratibu za dini mpya ya muhusika ?
 
Swali lako liko so complex..

Kuna sheria za ndoa zaidi ya moja..

Mfano mkioana Bomani kiserikali ndoa hazivunjiki kwa sahani ya dini..
Ndoa inavunjwa kwa mmoja kudai talaka mahakamani

Swali langu haliongelei bomani wala kimila wala ndoa ya kiserikali. Soma vizuri. Linaongelea ukristo na uislamu kwenye sheria za mahakama. Na ben pol ametumika kama case study. Hakuna sehemu kwenye swali nimeongelea ndoa za bomani wala za kimila
 
Hapana, kwa waislamu ndoa ambazo zimefungwa katika ukristo kihalali na wakaamua kubadili dini wote wawili wanendelea na ndoa yao. Inatambulika kiislamu.

Je kama amebadili dini mmoja tu wa wanandoa. Ndoa inakuwa bado halali?
 
Swali langu haliongelei bomani wala kimila wala ndoa ya kiserikali. Soma vizuri. Linaongelea ukristo na uislamu kwenye sheria za mahakama. Na ben pol ametumika kama case study. Hakuna sehemu kwenye swali nimeongelea ndoa za bomani wala za kimila

Kwanza Kenya na Tz Wana sheria tofauti za ndoa...
 
Back
Top Bottom