Habari wadau.
Nimeona watu wengi wanabadili dini zama hizi. hasa wakiwa na migogoro ya ndoa zao.
Reference case ben pol. alifunga ndoa ya kanisani.. then mwaka mmoja mbele akabadili dini kutoka ukristo na kuhamia uislamu. ikasemekana ndoa yake ya awali ya kikristo ilikuwa na mgogoro na imevunjika haraka haraka baada yeye kubadili dini, je ni sahihi?
Inasemekana wanawake wengi wa kikristo huwa hawasapoti ndoa ivunjike kisheria hata kama ndoa imekufa hasa mume akiwa na mali, mahakamani hawatoi ushirikiano wa divorce kabisa na kupelekea divorce kushindikana mfano hai master jay imemchukua zaidi ya miaka 10 kufanya divorce.. ama yule bwana wa mbunge magige aliyeleta seke seke kwenye mazishi., je mbinu ya kubadili dini inavunja ndoa kisheria?
Wanasheria ni vizuri mkatoa majibu, ili wakristo ambao bado hatujafunga ndoa na maskini, tujue mpema siku tukipata mali ama utajiri tuwe makini kujua tunafunga ndoa zenye sheria gani

1. Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania ya mwaka 1970 (kama ilivyofanyiwa marekebisho hadi 2019) moja ya vipengere vinavyoonyesha kuwa ndoa imevunjika na haiwezi kurekebika ni pale ushahidi unapoonyesha kuwa mlalamikaji amebadili dini wakati ilipofungwa wanandoa walikuwa dini moja na kwa mujibu wa dini yao kubadilisha dini kunafanya ndoa yao isiwepo tena au ni moja ya sababu zinazofanya ndoa yao isiwepo. Soma sura ya 107(2)(i).
2. Kwa sheria za kidini, mfano kwa upande wa Kanisa Katoliki, ndoa (iliyofungwa kanisani), ambayo imevunjwa kiserikali (mahakamani) itaendelea kuwa ndoa halali machoni pa kanisa hadi hapo utakapotikana ushahidi mbele ya mahakama ya Kanisa kwamba kabla ya kufunga ndoa, wanandoa au mmojawapo hakuwa na uhuru (hakuridhia) kufunga ndoa, mmojawapo au wanandoa wote wawili walidanganya ili ndoa ifungwe wakati wakijua kwamba kama wasingedanganya isingefungwa kanisani, kama wanandoa ni ndugu wa damu (are within prohibited relationship) au kama wakati wa kufunga ndoa mmoja au wanandoa wote wawili walikuwa na ndoa ingine halali au walikuwa wanafungwa na maagano mengine (kwa mfano mmojawapo alikuwa padri hata kama ameecha, lakini hajafuata utaratibu wa kuvuliwa upadri).
Nje ya sababu hizo, ndoa iliyofungwa kanisani (Kanisa Katoliki) itaendelea kuwa ndoa halali kwa sababu kwa mujibu wa Kanisa Katoliki 'alichounganisha Mungu (ndoa iliyo halali) mwanadamu hawezi kutenganisha/kuitengua isipokuwa kifo'. Kanisa linaamini wanaofunga ndoa halali si wawili tena bali Mungu huwafanya kuwa mwili mmoja na ndoa yao si tu ndoa, bali ni sakramenti (alama wazi inayoonekana inayoonyesha neema ya Mungu isiyoonekana).
Dini zingine nadhani hazina msimamo kama huu na kutokana na matatizo waliyonayo wanandoa, huenda ndoa inaweza kutenguliwa. Kwa Kanisa Katoliki wanandoa wanapofunga ndoa wanaahidi kuishi pamoja kwa upendo na uvumilivu "wakati wa neema na matatizo hadi kufa". Kwa mantiki hii, matatizo yanayojitokeza baadaye kama ndoa waliyofunga ilikuwa halali hayahalalishi ndoa halali kutenguliwa (hayabatilishi) hata kama wanandoa wataamua wao wenyewe kuachana na kila mmoja kuamua kufunga ndoa ingine na mtu mwingine (kwa mfano wale ambao ndoa yao imetenguliwa mahakamani). Hivi ndivyo ninavyoweza kujibu swali lako.