Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa alithibitisha mauaji hayo na kusema kuwa tukio hilo ni la Mei 5 mwaka huu saa nne usiku katika mtaa wa stoo Kata ya Igunga mjini.
Mwakalukwa alisema mtuhumiwa, Ezekiel Jonas alikuwa anaishi na binti huyo aliyekuwa mfanyakazi wa ndani. Alisema baada ya yeye kutengana na mke wake, alimwita ndani binti huyo na kumuuliza amwambie mwanaume anayetembea na mke wake.
Alisema binti huyo alipoulizwa na mtuhumiwa, alidai yeye hajui kitu chochote, ambapo mtuhumiwa hakuridhika na majibu ya binti huyo, hivyo alianza kumshanbulia kwa kumpiga kichwani na kitu chenye ncha kali hadi kusababisha kifo chake.
Alisema mtuhumiwa alipoona ameua, alichukua mfuko wa sandarusi na kuuweka mwili wa marehemu kwenye mfuko huo.
“Polisi tulipata taarifa kutoka kwa raia wema wakisema kuna binti anapigwa vibaya na tajiri yake.
Sisi tulifika eneo la tukio majira ya saa nne usiku, ambapo tulikuta mtuhumiwa ameshamuua binti huyo huku akiwa amemuweka kweye mfuko wa sandarusi” alisema.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote. Alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Merchades Magongo alithibitisha kupokea mwili wa Ester Mahona Mei 5 majira ya saa 4:30 usiku. Alisema baada ya kuufanyia uchunguzi, waliwakabidhi ndugu zake kwa ajili ya mazishi.
Chanzo: Mtanzania