Mume kizimbani kwa kutishia kumuua mke kisa kupeleka chakula kwa mchungaji

Nobunaga

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Posts
1,205
Reaction score
5,121
Japo kutishia kuua ni kosa, ila alilofanya huyu dada ni ujinga na upumbavu kwa wakati mmoja. Hatukatai mtu kumtolea Bwana sadaka ila aina hizi za sadaka ni dhambi si sadaka tena.

---
Joseph Moses dereva wa ‘bodaboda’ mkazi wa Mbeya anayekabiliwa na shtaka la kutishia kumuua mkewe kwa maneno, Irene Mwaikana, ameiambia mahakama kuwa chanzo cha ugomvi huo ni tabia ya mkewe kupeleka chakula kwa mchungaji.

Moses ametoa madai hayo katika Mahakama ya Mwanzo mjini Mbeya chini ya Hakimu Upendo Moshi alipokuwa akitoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Ameiambia mahakama kuwa anafanya kazi kwa shida na kukutana changamoto nyingi hususani ajali za barabarani, lakini pindi anaporudi nyumbani anakuta mkewe amepika chakula na kukipeleka kwa mchungaji.

“Mheshimiwa Hakimu huyu mwanamke anakera sana, yaani tukichinja kuku, vipaja na vidari vyote anapelekewa mchungaji, alafu mimi ninayetafuta pesa kwa shida napewa vipapatio,” amedai.

“Hii tabia imeota mizizi kiasi kwamba nahisi anatoka naye kimapenzi, kwanza mchungaji mwenyewe hana mke, hivi hata ungekuwa wewe usingehisi vibaya?” amehoji.

Moses anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti Mosi mwaka huu usiku, na ndipo mkewe alipomfikisha mahakamani akidai kutishiwa kuuawa.

Chanzo: Swahili Times
 
Huyo mchungaji katoa wapi ujasiri wa kumgegeda mke wa mtua adi ana lishwa na gharama za mwenye mke?? kwa kweli anastahili kukatwa shingo na yeye na huyo mchepuko wake
 
Japo dada ana makossa lakini ni heri alivyojiwahi polisi, maana sikuhizi visa vya wapenzi au wanandoa kuuana vimekuwa vingi mno, yani ukisikia mtu amethubutu kukutamkia hivyo ujue iko siku atafanya
 
Japo dada ana makossa lakini ni heri alivyojiwahi polisi, maana sikuhizi visa vya wapenzi au wanandoa kuuana vimekuwa vingi mno, yani ukisikia mtu amethubutu kukutamkia hivyo ujue iko siku atafanya
 
Japo kutishia kuua ni kosa, ila alilofanya huyu dada ni ujinga na upumbavu kwa wakati mmoja. Hatukatai mtu kumtolea Bwana sadaka ila aina hizi za sadaka ni dhambi si sadaka tena.

---
Joseph Moses dereva wa ‘bodaboda’ mkazi wa Mbeya anayekabiliwa na shtaka la kutishia kumuua mkewe kwa maneno, Irene Mwaikana, ameiambia mahakama kuwa chanzo cha ugomvi huo ni tabia ya mkewe kupeleka chakula kwa mchungaji.

Moses ametoa madai hayo katika Mahakama ya Mwanzo mjini Mbeya chini ya Hakimu Upendo Moshi alipokuwa akitoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Ameiambia mahakama kuwa anafanya kazi kwa shida na kukutana changamoto nyingi hususani ajali za barabarani, lakini pindi anaporudi nyumbani anakuta mkewe amepika chakula na kukipeleka kwa mchungaji.

“Mheshimiwa Hakimu huyu mwanamke anakera sana, yaani tukichinja kuku, vipaja na vidari vyote anapelekewa mchungaji, alafu mimi ninayetafuta pesa kwa shida napewa vipapatio,” amedai.

“Hii tabia imeota mizizi kiasi kwamba nahisi anatoka naye kimapenzi, kwanza mchungaji mwenyewe hana mke, hivi hata ungekuwa wewe usingehisi vibaya?” amehoji.

Moses anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti Mosi mwaka huu usiku, na ndipo mkewe alipomfikisha mahakamani akidai kutishiwa kuuawa.

Chanzo: Swahili Times

Wanaume tuna Kazi sana
 
Wachungaji mnawatesa wanaume wenzenu jamani.....[emoji1787]ila angemuua kabisa, yaani anunue kuku aishie kula vipapatio!? Haikubaliki
 
Kuna shida ya uelewa kwa watu wetu wengi sana, matokeo yake wengi ni rahisi sana kurubuniwa, hili ni kwa wote anaweza kuwa wanamke au mwanaume.
 
Japo kutishia kuua ni kosa, ila alilofanya huyu dada ni ujinga na upumbavu kwa wakati mmoja. Hatukatai mtu kumtolea Bwana sadaka ila aina hizi za sadaka ni dhambi si sadaka tena.

---
Joseph Moses dereva wa ‘bodaboda’ mkazi wa Mbeya anayekabiliwa na shtaka la kutishia kumuua mkewe kwa maneno, Irene Mwaikana, ameiambia mahakama kuwa chanzo cha ugomvi huo ni tabia ya mkewe kupeleka chakula kwa mchungaji.

Moses ametoa madai hayo katika Mahakama ya Mwanzo mjini Mbeya chini ya Hakimu Upendo Moshi alipokuwa akitoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Ameiambia mahakama kuwa anafanya kazi kwa shida na kukutana changamoto nyingi hususani ajali za barabarani, lakini pindi anaporudi nyumbani anakuta mkewe amepika chakula na kukipeleka kwa mchungaji.

“Mheshimiwa Hakimu huyu mwanamke anakera sana, yaani tukichinja kuku, vipaja na vidari vyote anapelekewa mchungaji, alafu mimi ninayetafuta pesa kwa shida napewa vipapatio,” amedai.

“Hii tabia imeota mizizi kiasi kwamba nahisi anatoka naye kimapenzi, kwanza mchungaji mwenyewe hana mke, hivi hata ungekuwa wewe usingehisi vibaya?” amehoji.

Moses anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti Mosi mwaka huu usiku, na ndipo mkewe alipomfikisha mahakamani akidai kutishiwa kuuawa.

Chanzo: Swahili Times
Mwanamke na mchungaji wamepanga kijana afungwe ili wao wawe huru.
 
Back
Top Bottom