Mume kizimbani kwa kutishia kumuua mke kisa kupeleka chakula kwa mchungaji

Ila hii nchi bana, wanawake wa nchi hii sijui wamepatwa na nini! Jamaa katishia kumuua mke wake kisa mama watoto anamplekea nyama mchungaji
[emoji23][emoji23]

“Mheshimiwa hakimu huyu mwanamke anakera sana, yaani tukichinja kuku, vipaja na vidari vyote anapelekewa mchungaji, alafu mimi ninayetafuta pesa kwa shida napewa vipapatio."

“Hii tabia imeota mizizi kiasi kwamba nahisi anatoka naye kimapenzi, kwanza mchungaji mwenyewe hana mke. Hivi hata ungekuwa wewe usingehisi vibaya?”

- Joseph Moses mkazi wa Mbeya anayedaiwa kutisha kumuua mkewe
 
Ila kuna wanawake sijuagi wana akili gani, kuna mwingine nae huku kaachika kisa hakai kabisa nyumbani anashinda kanisani.
 
Huyu ni wakutandika tu makofi ya masikioni na kumdurisha kwao, au unamkabidhi kwa "mchungaji"
 
Church woman wengii ni hatari kwa ustawi wa ndoa..na wengi wamevuruga mpk familia zao kisa huko kanisani na wachungaji wao
 
Hao ndiyo baadhi ya wanawake yaani, hapo usikute ameamua kwenda mahakamani kabisa ili jamaa afungwe yeye aendelee kula maisha na mchungaji, maana kama si dhamira yake kumfunga wangemalizana polisi then angeachana na jamaa maisha yaendelee

Kitendo cha mume kukesha akiitafuta pesa ya kulea familia, halafu mke naye anakuwa busy kulea mchungaji inaumiza sanaaaa
 
Hawa wanawake na wachungaji wao sijui wameumbwaje sijui akili zao zinawaza nini.. ukute huyo mchungaji ndiyo kamshauri aende mahakamani kumshtaki waachane
Hili lidini la kipumbavu sana. Na watu/wanawake wanavyopenda upumbavu, basi wanamiminika huko.
 
Tuna mahakama za hovyo sana,
Badala ya kusuhisha ndoa, wanataka kuivunja ndoa.

Hili suala lilitakiwa liishie huko serikali za mitaa au ustawi wa jamii.

Hivi wanategemea wakishamshughulikia uyo mume, kutakua na ndoa Tena hapo?

Vipi kuhusu hao watoto wa hiyo familia?
Mahakama itatoa malezi na matunzo?

Ujinga mtupu[emoji3525]
 
Mchungaji kajifanya ndege wa angani halimi, havuni wala kuweka ghalani lakini muumini wake anamlisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…