Habari zenu wapendwa,
Mwenzenu nina changamoto nipo kwenye ndoa miaka 13. Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana tulikuwa marafiki wazuri ila baada ya kuhamia Dar mwaka 2015 kuanza maisha mume wangu akapata Rafiki uyo Rafiki yake ni wale watu wenye uswahili mwingi maisha yakaendelea tukapata maisha biashara nzuri tuna mafanikio sasa hivi, ila yule Rafiki wa mume wangu Hana kazi kwa hiyo muda wote anafatana na mume wangu.
Muda mwingine mume wangu anaacha kazi kwenda kuzurura na rafiki yake nikawa namwambia mume wangu shughuli za kazi zetu ni mjini wewe unashinda Mbagala huku biashara nani anaendesha, basi anakuwa mkali.
Yaani nikitaka kumuongelea huyo rafiki yake vibaya anakuja juu. Mume hanywi pombe havuti sigara hapendi mpira ila siku akiwa na rafiki yake kurudi nyumbani ni saa 7 au saa 8 usiku msg za wanawake kama zote kwenye simu ila wakitengana na Rafiki yake kama miezi miwili au mitatu anawahi kurudi simu anaacha peupe anashinda mazingira ya kazini.
Mwanzo nikasema labda mimi namchukia huyu Rafiki yake ngoja nianze kuongea naye, ukikaa naye ni kama mtu Mwenye chuki na wanawake haoni thamani ya mwanamke anamwambia mume wangu
1) Mwanamke akikupenda anakuwa kama mzigo bora kuishi na mwanamke asiyekupenda
2) Hii alinambia mimi yaani wewe usipokuwa karibu na mimi nina uwezo kumharibu mumeo kumpeleka kwenye makundi mabaya na urafiki wangu na mumeo wakutenganisha Bado hajazaliwa
3) Mke kitu gani, wangapi tunasikia huyu alikua mke wa fulani kwa hiyo kuachana na mke sio ishu.
Mume wangu kila kitu cha ndani ya ndoa anamwambia hakuna kitu hajui nilimwambia mume wangu vitu vingine ni siri yetu haelewi.
Mume wangu nampenda ila nahisi ye anampenda zaidi rafiki yake kuliko Mimi. Imefikia hatua nawaza niondoke nimuache na Rafiki yake au niendelee kumvumilia huyo Rafiki yake maana hata akipiga simu huyo Rafiki yake anaenda kuongelea nje.
Nahisi ndoa imekuwa ya watu wa tatu sio wawili tena naomba mnisaidie ushauri.