Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,264
- 10,535
AmeeeeenMungu anipe kukinai kwa nafsi nisije nikafikie tamaa ya kiasi hicho.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AmeeeeenMungu anipe kukinai kwa nafsi nisije nikafikie tamaa ya kiasi hicho.
Ahsante sana ntakufanyia kaziSema watu wengi wanao hamia dar wakapata marafiki uku dar wanabadlika sana sijui ulimbukeni nishawai pata kesi kama yako
Yaani mwanaume anatumia muda mwingi na rafiki kuliko mkewe ambaye akiumwa ndio atamuogesha
Be patient mpotezee acha kumfwatilia fanya mambo yako usionyeshe kukelekwa na tabia zake
Sijajua kitu gani kinampa jeuri maana uyo Rafiki yake na mkewe Kuna kipindi mpaka wananitukana mume wangu hafanyi chochote na Mimi huwa siwajibuHuo urafiki, urafiki gani ? Dunia ya leo hii iliyojaa mapicha-picha. Kuna kinachompa jeuri huyo rafiki, simama imara huihitaji hata kwenda popote isipokuwa "Sala yashinda hofu" na Mungu atashughulika naye. Wala usipoteze muda wako kwa kumfaatilia mume wako au kumchunguza.
Kipindi tunaona huyu Rafiki yake hakuwepo mume wangu alikua na marafiki zake wengine na nilikuwa napatana nao wote baada ya kuja dar ndio kampata uyo Rafiki marafiki zake wa zamani mmoja wapo alikuja dar kututembelea mi nilikuwa nimesafiri nilivo rudi akaniambia shemu uyu Rafiki wa mumeo wa sasa hivi sio mtu mzuri mi sikutilia akilini sana kwanini ananiambia hivyo Wala sikujua kaona NiniHawa watu huwa wanapenda watuchagulie marafiki wa kuwa na nao
Ukimuoa tu anahakikisha marafiki zako wote anawaondoa
Nakumbuka kuna rafiki yetu alipooa siku za wkend tulikuwa tukienda kwake mke ananuna au anafagia ili mradi awatimulie vumbi tu,mwisho wa siku ilibid tuache kwenda kwa jamaa
Iyo chumvi ya mawe wanatumiaje naomba nielekezeMuombe sana Mungu lakini pia tumia chumvi ya mawe kumfukuza huyo shetani maana keshaiingilia ndoa yenu na hakuna mchawi anaweza kumtoa mpaka mfilisike kabisa.
Ameshapata pa kuponea kwahiyo usimuoneshe kabisa kwamba unamchukia, maana kwa jinsi alivyomkamata mumeo anaweza kumuamrisha chochote naye akafanya.
Sawa ahsante ntalifanyia kazi1. Muombee kwa Mungu sana huyo mume wako, afunguke macho na masikio yake atambue na kujali thamani na hisia zako kwake. Tumia meditation- unamwomba Mungu muda wote na kwa ukimya kabisa. Asijue mtu unachokiwaza.
2. Usimjali, usimwogope, usimnyenyekee hata kidogo wala usimwoneshe chuki directly huyo rafiki yake. Kuwa bold. Akijichekesha shem shem we kuwa serious usimkenulie meno au kumjibu..aone tofauti flani.
3. Badilika katika mambo yako na tabia zako flani flani positively, na yeyote asijue kwanini umebadilika ghafla. Kama ulizoea kuamka saa moja, amka saa 12 asbh. Kama ulizoea kulala na vyombo vichafu au jikoni rafu.. ongeza usafi zaidi. Hali kadhalika na usafi binafsi (in case haukuwa 100%)
- Acha kumwongelea huyo rafiki wa mumeo kwa mumeo, acha kabisa tena kwa ghafla. Endelea tu na meditation kwa Mungu wako kuwa waachane/ mumeo afunguliwe.
- Ikitokea siku mumeo akasema jambo flani baya alilokerwa na huyo jamaa, usikimbilie kuchangia moja kwa moja, kuwa "si nilikwambia!" au "ndio matokeo ya ubishi wako!" No, No! Usije kufanya jambo hilo. Badala yake toa jibu la general kama vile " uwe makini na marafiki" basi.
- Kila la kheri.
Hii hatari sana kumuamini mtu sana nayo sio nzuri, kuna watu wakiligundua hilo hulitumia vibaya.Siamini sana kwenye uchawi ila naamini kuna watu wamejaaliwa kipaji cha kulaghai watu, ana manipulate mind yako na hisia zaki unakua kama robot anakuendesha atakavyo, wapo watu wa hivyo wake kwa waume, wana maneno mazuri, yenye ushawishi wa hali ya juu na kama amekutarget huchomoki labda na wewe una na nguvu dhidi yake.
Habari zenu wapendwa,
Mwenzenu nina changamoto nipo kwenye ndoa miaka 13. Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana tulikuwa marafiki wazuri ila baada ya kuhamia Dar mwaka 2015 kuanza maisha mume wangu akapata Rafiki uyo Rafiki yake ni wale watu wenye uswahili mwingi maisha yakaendelea tukapata maisha biashara nzuri tuna mafanikio saiz ila yule Rafiki wa mume wangu Hana kazi kwaiyo mda wote anafatana na mume wangu.
Muda mwingine mume wangu anaacha kazi kwenda kuzurura na rafiki yake nikawa namwambia mume wangu shughuli za kazi zetu ni mjini we unashinda Mbagala uku biashara nani anaendesha, basi anakuwa mkali.
Yani nikitaka kumuongelea uyo rafiki yake vibaya anakuja juu. Mume hanywi pombe havuti sigara hapendi mpira ila siku akiwa na rafiki yake kurudi nyumbani ni saa 7 au saa 8 usiku msg za wanawake km zote kwenye simu ila wakitengana na Rafiki yake kama miezi miwili au mitatu anawahi kurudi simu anaacha peupo anashinda mazingira ya kazini.
Mwanzo nikasema labda mi namchukia huyu Rafiki yake ngoja nianze kuongea naye, ukikaa naye ni kama mtu Mwenye chuki na wanawake haoni thamani ya mwanamke anamwambia mume wangu
1) Mwanamke akikupenda anakuwa km mzigo bora kuishi na mwanamke asiyekupenda
2) Hii alinambia mimi yani wewe usipokuwa karibu na mimi nina uwezo kumharibu mumeo kumpeleka kwenye makundi mabaya na urafiki wangu na mumeo wakutenganisha Bado hajazaliwa
3) Mke kitu gani, wangapi tunasikia huyu alikua mke wa fulani kwaiyo kuachana na mke sio ishu.
Mume wangu kila kitu cha ndani ya ndoa anamwambia hakuna kitu hajui nilimwambia mume wangu vitu vingine ni siri yetu haelewi.
Mume wangu nampenda ila nahisi ye anampenda zaidi rafiki yake kuliko Mimi. Imefikia hatua nawaza niondoke nimuache na Rafiki yake au niendelee kumvumilia huyo Rafiki yake maana ata akipiga simu uyo Rafiki yake anaenda kuongelea nje.
Nahisi ndoa imekuwa ya watu wa tatu sio wawili tena naomba mnisaidie ushauri.
Piga moyo konde na kuwa jasiri. Utayashinda🤝Ahsante sana ntakufanyia kazi
Sijajua kitu gani kinampa jeuri maana uyo Rafiki yake na mkewe Kuna kipindi mpaka wananitukana mume wangu hafanyi chochote na Mimi huwa siwajibu
Upo sahihi, watu wengi hutumia madhaifu yetu ili kufanikisha jambo lao, muhimu ni kuacha kujielezea sana na kutompa mtu funguo ya maisha yako.Hii hatari sana kumuamini mtu sana nayo sio nzuri, kuna watu wakiligundua hilo hulitumia vibaya.
Nakazia hapa, chunguzaHuyo rafiki yake ni mke mwenzio, chunguza.
Madogo wa chuo hao hamna wanalolijua.Huu ni uandishi wa kijana ambaye bado yupo chuo au amemaliza hivi karibuni bado hajaanza kusota na vibahasha,
Kuna mada zingine zinakua kubwa unaachana nazo tu.
Hakika, na kuweka mipaka.Upo sahihi, watu wengi hutumia madhaifu yetu ili kufanikisha jambo lao, muhimu ni kuacha kujielezea sana na kutompa mtu funguo ya maisha yako.
Safi, alipata stahiki yake.Umemshauri vizuri kaka mkubwa.
Story ya huyo dada inafanana na ya Aunt yangu, ndoa yake ili vamiwa na kidudumtu akamshika Anko kichwa akawa anamtafutia wanawake, kila kitu anamshirikisha, nyumba ikawa haina amani, hajali tena familia yeye ni wa kupelekeshwa na huyo rafiki aliyemuamini kuliko nafsi yake, Aunt alikonda sana, alihangaika sana kuwatenganisha vikao na vikao viliwekwa lakini wapiiii.
Siku moja huyo kidudumtu akamtambulisha Anko kwa mwanamke akadai alikua anaishi Uingereza ameachana na mume wake amerudi Tz, basi wakaanza mahusiano penzi lilinoga akawa harudi nyumbani hata wiki, nguo akahamishia kwa huyo Muingereza, si akaanza kumjengea nyumba bhana, unaambiwa Anko alitumia pesa zake zote na mikopo juu kujenga nyumba ya kifahari, nyumba ilijengwa kwa shinikizo la huyo huyo rafiki mtu akamshawishi ajenge nyumba ya kifahari amuoe huyo mwanamke waishi wote.
Kufupisha story, siku moja anko, kidudumtu na yule mwanamke walikua hoteli moja maarufu kwenye live band, mmoja wa waimbaji wa ile Band anawafahamu wote watatu si ndio akaenda kuwasalimia bhana akawa anamuita yule mwanamke shemeji, kwa kuzuga ikawa hana namna ilibidi aitikie na kulazimisha uchangamfu, baada ya yule muimbaji kuondoka kidudumtu na Mwanamke wa UK hawakua na furaha baada ya muda wakaondoka, lakini Anko akabaki na alama nyekundu vipi yule muimbaji amuite yule Mwanamke Shemeji? Alijua ni Mwanamke wa nani wakati yeye mke wake anajulikana na yule hawara anamficha kama bangi sura yake haitambuliki isipokua kwa rafiki yake? na Rafiki yake hana Mke? Hakutaka kupuuzia hilo.
Weekend iliyofata akaenda peke yake akamuomba muimbaji wazungumze pembeni, alipomuuliza kama yule mwanamke anamjua muimbaji akashangaa sana akamjibu mbona yule ni mke wa rafiki yako? Ina maana pale kwenye meza nyie mlikaa bila kujuana au ina maana hujui kama rafiki yako ana mke na watoto na yule mwanamke! Anko alipoteza fahamu hapo hapo.
Anko aliwajengea Mume na Mke nyumba nzuri huku yeye akibakiwa na madeni na msongo wa mawazo alirudi kwa mke wake suruali imetepeta, zombie si zombie ilichukua miezi 6 kurecover, nyumba hakuipata na huo ndio ukawa mwanzo na mwisho wa urafiki wao.
Kuna tetesi zilisema alikua anaenda kuitizama nyumba yake kwa mbaaali huku analia ndio familia ikaazimia imuhamishe Mkoa.
Huyo wa Mbagala ni baby mwenzioHabari zenu wapendwa,
Mwenzenu nina changamoto nipo kwenye ndoa miaka 13. Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana tulikuwa marafiki wazuri ila baada ya kuhamia Dar mwaka 2015 kuanza maisha mume wangu akapata Rafiki uyo Rafiki yake ni wale watu wenye uswahili mwingi maisha yakaendelea tukapata maisha biashara nzuri tuna mafanikio sasa hivi, ila yule Rafiki wa mume wangu Hana kazi kwa hiyo muda wote anafatana na mume wangu.
Muda mwingine mume wangu anaacha kazi kwenda kuzurura na rafiki yake nikawa namwambia mume wangu shughuli za kazi zetu ni mjini wewe unashinda Mbagala huku biashara nani anaendesha, basi anakuwa mkali.
Yaani nikitaka kumuongelea huyo rafiki yake vibaya anakuja juu. Mume hanywi pombe havuti sigara hapendi mpira ila siku akiwa na rafiki yake kurudi nyumbani ni saa 7 au saa 8 usiku msg za wanawake kama zote kwenye simu ila wakitengana na Rafiki yake kama miezi miwili au mitatu anawahi kurudi simu anaacha peupe anashinda mazingira ya kazini.
Mwanzo nikasema labda mimi namchukia huyu Rafiki yake ngoja nianze kuongea naye, ukikaa naye ni kama mtu Mwenye chuki na wanawake haoni thamani ya mwanamke anamwambia mume wangu
1) Mwanamke akikupenda anakuwa kama mzigo bora kuishi na mwanamke asiyekupenda
2) Hii alinambia mimi yaani wewe usipokuwa karibu na mimi nina uwezo kumharibu mumeo kumpeleka kwenye makundi mabaya na urafiki wangu na mumeo wakutenganisha Bado hajazaliwa
3) Mke kitu gani, wangapi tunasikia huyu alikua mke wa fulani kwa hiyo kuachana na mke sio ishu.
Mume wangu kila kitu cha ndani ya ndoa anamwambia hakuna kitu hajui nilimwambia mume wangu vitu vingine ni siri yetu haelewi.
Mume wangu nampenda ila nahisi ye anampenda zaidi rafiki yake kuliko Mimi. Imefikia hatua nawaza niondoke nimuache na Rafiki yake au niendelee kumvumilia huyo Rafiki yake maana hata akipiga simu huyo Rafiki yake anaenda kuongelea nje.
Nahisi ndoa imekuwa ya watu wa tatu sio wawili tena naomba mnisaidie ushauri.
Duuuuh!!! Pole sana, hili suala la ndoa watu wawe serious kucommentHabari zenu wapendwa,

Huyo jamaa ni mshirikina....chukua hatua mapemaHii alinambia mimi yaani wewe usipokuwa karibu na mimi nina uwezo kumharibu mumeo kumpeleka kwenye makundi mabaya na urafiki wangu na mumeo wakutenganisha Bado hajazaliwa
Dahhh!!sio poaDunia imeshapinduka sasa hivi angalia na chunguza vizuri mambo yafuatao kati ya mme wako na huyo rafiki yake:-
1. Ushoga
2. Ushirikina
3. Dawa za kulevya
Kati ya hayo matatu hutokosa moja, haingii akilini mtu mpaka anaacha shughuli za uzalishaji na kwenda ku mfuata mwanaume mwenzie Mbagala!!!!!!