Mume kumgeuza rafiki ndio kila kitu kwake

Mume kumgeuza rafiki ndio kila kitu kwake

Umemshauri vizuri kaka mkubwa.

Story ya huyo dada inafanana na ya Aunt yangu, ndoa yake ili vamiwa na kidudumtu akamshika Anko kichwa akawa anamtafutia wanawake, kila kitu anamshirikisha, nyumba ikawa haina amani, hajali tena familia yeye ni wa kupelekeshwa na huyo rafiki aliyemuamini kuliko nafsi yake, Aunt alikonda sana, alihangaika sana kuwatenganisha vikao na vikao viliwekwa lakini wapiiii.

Siku moja huyo kidudumtu akamtambulisha Anko kwa mwanamke akadai alikua anaishi Uingereza ameachana na mume wake amerudi Tz, basi wakaanza mahusiano penzi lilinoga akawa harudi nyumbani hata wiki, nguo akahamishia kwa huyo Muingereza, si akaanza kumjengea nyumba bhana, unaambiwa Anko alitumia pesa zake zote na mikopo juu kujenga nyumba ya kifahari, nyumba ilijengwa kwa shinikizo la huyo huyo rafiki mtu akamshawishi ajenge nyumba ya kifahari amuoe huyo mwanamke waishi wote.

Kufupisha story, siku moja anko, kidudumtu na yule mwanamke walikua hoteli moja maarufu kwenye live band, mmoja wa waimbaji wa ile Band anawafahamu wote watatu si ndio akaenda kuwasalimia bhana akawa anamuita yule mwanamke shemeji, kwa kuzuga ikawa hana namna ilibidi aitikie na kulazimisha uchangamfu, baada ya yule muimbaji kuondoka kidudumtu na Mwanamke wa UK hawakua na furaha baada ya muda wakaondoka, lakini Anko akabaki na alama nyekundu vipi yule muimbaji amuite yule Mwanamke Shemeji? Alijua ni Mwanamke wa nani wakati yeye mke wake anajulikana na yule hawara anamficha kama bangi sura yake haitambuliki isipokua kwa rafiki yake? na Rafiki yake hana Mke? Hakutaka kupuuzia hilo.

Weekend iliyofata akaenda peke yake akamuomba muimbaji wazungumze pembeni, alipomuuliza kama yule mwanamke anamjua muimbaji akashangaa sana akamjibu mbona yule ni mke wa rafiki yako? Ina maana pale kwenye meza nyie mlikaa bila kujuana au ina maana hujui kama rafiki yako ana mke na watoto na yule mwanamke! Anko alipoteza fahamu hapo hapo.

Anko aliwajengea Mume na Mke nyumba nzuri huku yeye akibakiwa na madeni na msongo wa mawazo alirudi kwa mke wake suruali imetepeta, zombie si zombie ilichukua miezi 6 kurecover, nyumba hakuipata na huo ndio ukawa mwanzo na mwisho wa urafiki wao.

Kuna tetesi zilisema alikua anaenda kuitizama nyumba yake kwa mbaaali huku analia ndio familia ikaazimia imuhamishe Mkoa.
So sad!!!
 
Kuna mawili, huyo jamaa kama sio mshirikina basi atakuwa kamfundisha michezo ya hatari sana mumeo.

Aidha anamvutisha bange wakiwa uswahilini na anamtaftia mademu na kumtembeza viwanja pia kashamfundisha kufira. Mumeo kashapagawa na michezo ya town inaonesha alikuwa mshamba ndo analimbuka na mji.

In expense of all that huyo mswahili ananufaika na uchawa anaofanya kwa mumeo ana access na gari na hela za jamaa yako wanakostarehe huko. Kuhusu kukusagia kunguni lazma afanye hivyo ili mume akuone huna maana.
 
Hawa watu huwa wanapenda watuchagulie marafiki wa kuwa na nao

Ukimuoa tu anahakikisha marafiki zako wote anawaondoa

Nakumbuka kuna rafiki yetu alipooa siku za wkend tulikuwa tukienda kwake mke ananuna au anafagia ili mradi awatimulie vumbi tu,mwisho wa siku ilibid tuache kwenda kwa jamaa
Ni kero mwanawane yaani ni mwendo wa kuwakomedha tu wasije wakakupanda kichwani Hawa viumbe maana ni ubavu wetu hivyo mwambie jamaa akae chonjo
 
Huu ni uandishi wa kijana ambaye bado yupo chuo au amemaliza hivi karibuni bado hajaanza kusota na vibahasha,
Kuna mada zingine zinakua kubwa unaachana nazo tu.
Wacha tudandie mkuu time is an illusion
 
Dunia imeshapinduka sasa hivi angalia na chunguza vizuri mambo yafuatao kati ya mme wako na huyo rafiki yake:-
1. Ushoga
2. Ushirikina
3. Dawa za kulevya
Kati ya hayo matatu hutokosa moja, haingii akilini mtu mpaka anaacha shughuli za uzalishaji na kwenda ku mfuata mwanaume mwenzie Mbagala!!!!!!
Usiforce mkuuu kila kitu 🤮🤮🤮🤮
 
Ombea ndoa yako ,ombea Mumeo usiondoke hapo ,mmevamiwa tayari .Huyo rafiki mpaka anathubutu kukuongelea kwa kujiamini hivyo ni kutokana na nguvu iliyo ndani yake ...we pia una nguvu yako funguo ya hiyo nguvu ni maombi tu ,na usisahau kumtolea sadaka huyo mumeo
 
Kuna mawili, huyo jamaa kama sio mshirikina basi atakuwa kamfundisha michezo ya hatari sana mumeo.

Aidha anamvutisha bange wakiwa uswahilini na anamtaftia mademu na kumtembeza viwanja pia kashamfundisha kufira. Mumeo kashapagawa na michezo ya town inaonesha alikuwa mshamba ndo analimbuka na mji.

In expense of all that huyo mswahili ananufaika na uchawa anaofanya kwa mumeo ana access na gari na hela za jamaa yako wanakostarehe huko. Kuhusu kukusagia kunguni lazma afanye hivyo ili mume akuone huna maana.
pia yawezekana si rafiki wa mumewe bali mke mwenzake.
 
Siamini sana kwenye uchawi ila naamini kuna watu wamejaaliwa kipaji cha kulaghai watu, ana manipulate mind yako na hisia zaki unakua kama robot anakuendesha atakavyo, wapo watu wa hivyo wake kwa waume, wana maneno mazuri, yenye ushawishi wa hali ya juu na kama amekutarget huchomoki labda na wewe uwe na nguvu dhidi yake.

Urafiki mkubwa wa wanaume huwa ni wa mademu kutafutiana mademu tena ukikuta mmoja ana pesa mwingine hela weeeeee ambae hana kitu anakuwa chawa na anahakikisha anafanya vitu ambavyo vinamfurahisha mwenye pesq kama kumtafutia mademu nna ushuhuda na hilo
 
Acha ujinga mume huwa hachunguzwi utajiumiza kichwa bure.

Mume huwa haulizwi umetoka wapi,utarudi saa ngapi? au ulikuwa wapi na ilikuwa na nani?

Mume hachaguliwi marafiki!

Mume anahitaji nafasi (space) muache afanye mambo yake as long as anakutimizia mahitaji yako na wanao ( chakula,mavazi,malazi na tendo la ndoa)

Mume hafatiliwi/kuulizwa/kuchunguzwa mipango yake ya utafutaji.!!

Weka hili akilini.

Unachotakiwa kumpatia mumeo ni Heshima, uskivu na utii ,Space (nafasi) na tendo la ndoa.
Kwanini Mme wa dizaini hii asiishi tu na house girl na house boy afanyiwe usafi apikiwe nk mbunye atapiga piga za kila aina.....kwa maisha ya hivi yani anaoa ili iweje labda?
 
1. Muombee kwa Mungu sana huyo mume wako, afunguke macho na masikio yake atambue na kujali thamani na hisia zako kwake. Tumia meditation- unamwomba Mungu muda wote na kwa ukimya kabisa. Asijue mtu unachokiwaza.

2. Usimjali, usimwogope, usimnyenyekee hata kidogo wala usimwoneshe chuki directly huyo rafiki yake. Kuwa bold. Akijichekesha shem shem we kuwa serious usimkenulie meno au kumjibu..aone tofauti flani.

3. Badilika katika mambo yako na tabia zako flani flani positively, na yeyote asijue kwanini umebadilika ghafla. Kama ulizoea kuamka saa moja, amka saa 12 asbh. Kama ulizoea kulala na vyombo vichafu au jikoni rafu.. ongeza usafi zaidi. Hali kadhalika na usafi binafsi (in case haukuwa 100%)

  • Acha kumwongelea huyo rafiki wa mumeo kwa mumeo, acha kabisa tena kwa ghafla. Endelea tu na meditation kwa Mungu wako kuwa waachane/ mumeo afunguliwe.
  • Ikitokea siku mumeo akasema jambo flani baya alilokerwa na huyo jamaa, usikimbilie kuchangia moja kwa moja, kuwa "si nilikwambia!" au "ndio matokeo ya ubishi wako!" No, No! Usije kufanya jambo hilo. Badala yake toa jibu la general kama vile " uwe makini na marafiki" basi.
  • Kila la kheri.
You are a very intelligent person. I really appreciate this comment of yours. You have summarized perfectly on how to handle a negative situation and use it to improve yourself positively and grow positively. Kudos. I really hope mtoa thread will see and follow this advice.
 
Huu ni ushauri mbovu kuuona tangu mwaka huu uanze ukiachana na nyuzi za kisiasa za wana-CCM.Umeambiwa uishi na mke kwa akili na siyo umpe jirani au rafiki akili akushikie.Simama kama mwanaume.Kwani lazima utumie akili za rafiki uliyekutana naye tu mjini kuiendesha familia yako?Huo ni udhaifu daraja la juu sana.Badilika!
Ndo akili za wengi zilivyo. Si unaona wanavyojazanaga ujinga humu wa kuchukia wanawake.
 
Pole sana, huyo ni mke mwenzio. Au ndio anakula mumeo kinyeo... watu wengi walioishia kuuchunguza urafik wa namna hyo kiundani hawakutoka na majibu mazuri zaidi ndoa ziliishia kufa. Pole sana muombe Mungu akuondolee huyo pepo kwenye ndoa yako
 
Habari zenu wapendwa,

Mwenzenu nina changamoto nipo kwenye ndoa miaka 13. Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana tulikuwa marafiki wazuri ila baada ya kuhamia Dar mwaka 2015 kuanza maisha mume wangu akapata Rafiki uyo Rafiki yake ni wale watu wenye uswahili mwingi maisha yakaendelea tukapata maisha biashara nzuri tuna mafanikio sasa hivi, ila yule Rafiki wa mume wangu Hana kazi kwa hiyo muda wote anafatana na mume wangu.

Muda mwingine mume wangu anaacha kazi kwenda kuzurura na rafiki yake nikawa namwambia mume wangu shughuli za kazi zetu ni mjini wewe unashinda Mbagala huku biashara nani anaendesha, basi anakuwa mkali.

Yaani nikitaka kumuongelea huyo rafiki yake vibaya anakuja juu. Mume hanywi pombe havuti sigara hapendi mpira ila siku akiwa na rafiki yake kurudi nyumbani ni saa 7 au saa 8 usiku msg za wanawake kama zote kwenye simu ila wakitengana na Rafiki yake kama miezi miwili au mitatu anawahi kurudi simu anaacha peupe anashinda mazingira ya kazini.

Mwanzo nikasema labda mimi namchukia huyu Rafiki yake ngoja nianze kuongea naye, ukikaa naye ni kama mtu Mwenye chuki na wanawake haoni thamani ya mwanamke anamwambia mume wangu

1) Mwanamke akikupenda anakuwa kama mzigo bora kuishi na mwanamke asiyekupenda

2) Hii alinambia mimi yaani wewe usipokuwa karibu na mimi nina uwezo kumharibu mumeo kumpeleka kwenye makundi mabaya na urafiki wangu na mumeo wakutenganisha Bado hajazaliwa

3) Mke kitu gani, wangapi tunasikia huyu alikua mke wa fulani kwa hiyo kuachana na mke sio ishu.

Mume wangu kila kitu cha ndani ya ndoa anamwambia hakuna kitu hajui nilimwambia mume wangu vitu vingine ni siri yetu haelewi.

Mume wangu nampenda ila nahisi ye anampenda zaidi rafiki yake kuliko Mimi. Imefikia hatua nawaza niondoke nimuache na Rafiki yake au niendelee kumvumilia huyo Rafiki yake maana hata akipiga simu huyo Rafiki yake anaenda kuongelea nje.

Nahisi ndoa imekuwa ya watu wa tatu sio wawili tena naomba mnisaidie ushauri.
Hapo ndoa hamna tena, jiandae kutengana nae ili baadae yeye aje kujutia maamuzi yake.
 
Kama ana uswahili basi tayari kashamfanyia huo uswahili. Hakuna ukawaida hapo. Mkabidhi mumeo mikononi mwa Yesu Kwa MAOMBI kabla hajaharibikiwa zaidi

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom