Umemshauri vizuri kaka mkubwa.
Story ya huyo dada inafanana na ya Aunt yangu, ndoa yake ili vamiwa na kidudumtu akamshika Anko kichwa akawa anamtafutia wanawake, kila kitu anamshirikisha, nyumba ikawa haina amani, hajali tena familia yeye ni wa kupelekeshwa na huyo rafiki aliyemuamini kuliko nafsi yake, Aunt alikonda sana, alihangaika sana kuwatenganisha vikao na vikao viliwekwa lakini wapiiii.
Siku moja huyo kidudumtu akamtambulisha Anko kwa mwanamke akadai alikua anaishi Uingereza ameachana na mume wake amerudi Tz, basi wakaanza mahusiano penzi lilinoga akawa harudi nyumbani hata wiki, nguo akahamishia kwa huyo Muingereza, si akaanza kumjengea nyumba bhana, unaambiwa Anko alitumia pesa zake zote na mikopo juu kujenga nyumba ya kifahari, nyumba ilijengwa kwa shinikizo la huyo huyo rafiki mtu akamshawishi ajenge nyumba ya kifahari amuoe huyo mwanamke waishi wote.
Kufupisha story, siku moja anko, kidudumtu na yule mwanamke walikua hoteli moja maarufu kwenye live band, mmoja wa waimbaji wa ile Band anawafahamu wote watatu si ndio akaenda kuwasalimia bhana akawa anamuita yule mwanamke shemeji, kwa kuzuga ikawa hana namna ilibidi aitikie na kulazimisha uchangamfu, baada ya yule muimbaji kuondoka kidudumtu na Mwanamke wa UK hawakua na furaha baada ya muda wakaondoka, lakini Anko akabaki na alama nyekundu vipi yule muimbaji amuite yule Mwanamke Shemeji? Alijua ni Mwanamke wa nani wakati yeye mke wake anajulikana na yule hawara anamficha kama bangi sura yake haitambuliki isipokua kwa rafiki yake? na Rafiki yake hana Mke? Hakutaka kupuuzia hilo.
Weekend iliyofata akaenda peke yake akamuomba muimbaji wazungumze pembeni, alipomuuliza kama yule mwanamke anamjua muimbaji akashangaa sana akamjibu mbona yule ni mke wa rafiki yako? Ina maana pale kwenye meza nyie mlikaa bila kujuana au ina maana hujui kama rafiki yako ana mke na watoto na yule mwanamke! Anko alipoteza fahamu hapo hapo.
Anko aliwajengea Mume na Mke nyumba nzuri huku yeye akibakiwa na madeni na msongo wa mawazo alirudi kwa mke wake suruali imetepeta, zombie si zombie ilichukua miezi 6 kurecover, nyumba hakuipata na huo ndio ukawa mwanzo na mwisho wa urafiki wao.
Kuna tetesi zilisema alikua anaenda kuitizama nyumba yake kwa mbaaali huku analia ndio familia ikaazimia imuhamishe Mkoa.