Pole sana mpendwa kwa hilo unalopitia,hongera sana kwani umekubali hali na uko tayari kuishi muda mrefu ,nakushauri umshukuru sana Mungu hata kwa kujua hali yako na pia nakuomba uwe mwangalifu sana kuhusu mahusiano maana hata kama leo hii utampata wako ambaye anahali kama yako bado yapo mambo mengi sana ya kuzingatia katika kuishi na maambukizi ,changamoto zipo na wakati mngine unaweza ukawa huna maamuzi kuhusu mambo fulanifulani hasa ya kiafya.tiba..upendo..hisia..kujikubali..uchumi..tabia na mengine mengi hasa mkiwa wawili ...tumuombe Mungu kwakweli upate haja ya moyo wako na amani uishi maisha marefu ya furaha na uwaone watoto wa watoto wako...INAWEZEKANA MUNGU AKUTIE NGUVU.