jouneGwalu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,687
- 1,782
Mwanaume siku zote hapendi kuoneka mwenye makosa au kuonekana yuko chini,hata kama kosa amefanya yeye hutaka kuligeuza na kuwa la mwanamke.
1.Jitahidi kumpenda mtu mnaye'fitiana'..kielimu, kiuchumi na kimtazamo.
Hapana, kumpenda mtu ni suala la hisia tu ambalo halihitaji maelezo ya zaidi kuwa huyu ni nani na anafanya nini...Mbaya sana (Ila ndio utamu wa mapenzi) ni kuwa mnapokuwa kwenye hizo hisia huwa huoni pungufu lolote...Hapa hujatoa suluhisho .... lol..Suluhisho ni moja tu........... "Penzi halihoji kitu..., we penda tu"
Ni kweli unachosema kabisa ila inachosha sana pale ambapo mwanamke ndo unakuwa kila siku wa kujaribu kurejesha furaha au amani ndani ya ndoa kama vile mwanamke ndo unaihitaji saaana hiyo ndoa yeye mwanaume siku zote anasubiri uanze ndo mambo yaende sawa inachosha na maudhi yakizidi huduma kwa mke inapungua na ndo hapo mwanaume anaanza kutoka nje au kuhesabu mapungufu ya mke bila kuhoji chanzo cha tatizo ni nn. Mara nyingi mwanaume anataka tatizo liishe hivihivi tu bila kulitatua na usamehe au uombe msamaha muendelee ila likiwa tatizo kwa mwanamke ni ishu hawana subira wala uvumilivu ni matusi vipigo na tatizo litaongelewa miezi sita lol its sooo tiresome aah!Yeah But the last time I checked a woman is also a human being capable of making intuitive deductions. Ana sehemu kubwa ya kuhakikisha ndoa yake inakuwa ya furaha pia sio kukimbilia uzinzi na kuto'earn' mistakes zake kisha kusingizia hakuwa anasifiwa na mmewe.
Mkuu nadhani sakapal hakumalizia vizuri utafiti wake, otherwise angegundua kuwa wanaume wengi wasiojiamini wanasababishiwa na wake/wapenzi wao. Usikute hata bro wake naye alisababishiwa na mkewe!
mwanaume siku zote hapendi kuoneka mwenye makosa au kuonekana yuko chini,hata kama kosa amefanya yeye hutaka kuligeuza na kuwa la mwanamke,lakini ,mengine huchagizwa zaidi na tabia ya mtu binafsi pamoja na mazingira aliyokulia nayo.
sakapal naomba kujifunza zaidi kuhusu umuhimu wa hapo kwa red. Manake sinaga mazoea ya kumsifia mwandani wangu. Si kwamba siwezi kufanya hivyo, ila ni kwamba sijuagi mashiko yake, hivyo huwa na-ignore tu!
sakapal ungefafanua kwa mfano halisi ingekuwa haki zaidi, ila kwa hivyo ulivoiacha imekaa kiujumla-jumla hivyo hivyo inapoteza uhalisia sababu sio wote wanaokunywa pombe wanafanya hizo tabia za kishamba...
Ila yote kwa yote huyo mwanaume unayemaanisha hajafaulu kwenye mtihani wa The Boss kwa huyo mtu kuitwa
Mwanaume.
Ndio maana nasema lazima tujifunze kitu hapa..nini kimepelekea bro wako kuwa hivyo???
Kwa sababu yote unayoeleza ni matokeo ya 'inferiority'..je nini tunaeza kufanya ili kuepuka?
Hili ndio nataka tujadili!!
Kwakweli hapo sijajua ila nilichokuwa nataka kusema hapa makosa kwenye ndoa yanafanyika kwani sie wote ni wanadamau na si malaika ila kosa akilifanya mwanamke ni kosa kubwa ila kosa akilifanya mwanaume limezewe na liishie hapo tu na lisikumbushiwe hata likirudiwa kwa trend hii mwanamke anakereka na anachoka haraka. Mfano hii ilijulikana hadi kwenye familia yote bro alikuwa anamtongoza na haousegirl na yule mschana hakukubali akaondoka bila kuaga nyumba kaiacha wazi kuja kumfatilia y umefanya hivo coz vitu vingeibiwa ndo akasema huo ukweli kuulizwa bro wakati huo familia yote ishajua akasema samahani familia sitarudia tena it was soo kwa wifi na alikuwa mjamzito that time na watoto wadogo just emagine two years later same scenario repeated wifi akasema nimechoka kuishi nawewe na mambo yako ila kama mwanamke anatatizo y wanaume hawaliongelei na kulitatua? ila wao wakiwa na tatizo lisamehewe fast loooh!
unachosema ni sawa ila wanawake na nyie muwafanyie vyema waume zenu.....kufanya kitu inabidi kitoke moyoni
huwezi kusikia raha ya kumsifia mke wako ikiwa yy ana kudharau au ana vidumu, kuna wanawake hawawezi kukubali kosa mpaka aone una ushahidi wa kutosha ndo anakubali na kuwa mpole maana utakuwa umemkamata...kwa mazingira haya unafikiri neno I LOVE YOU au UMEPENDEZA linaweza kutoka kirahisi....kwanza linakuwa gumu na zito ni bora uende kulima kuliko kuyatamka haya maneno bila furaha
ni eona kila mtu anaona ya mwenzie na hakuna anaeona yake ndo maana wazee wetu walisema nyani haoni kundule.
Mtazamo wangu kwanini wanandoa wasiamue once in every six months kureconcile ndoa na kuenjoy kuliko kukimbilia site na kukaa bar till late hrs? mimi naamini maongezi hujenga kukiwa na kusikilizana na kusamehe na kuahidi kutorudia na kumkumbusha mwenzio pale unapoona anaanza kuanguka before hajaanguka ili kuweka peace home na kulea watoto. Maana inafikia mahali kila mtu anafanya mambo yake akiishiwa ndo mnarudi kuongea ukipata pesa yako kibindoni lol
hapo kwenye kukaa chini mkaelewana ndo ilipo shughuli....tatizo ni kudharau matatizo madogo madogo na kudhani mwenzangu anatakiwa kuelewa na kuliacha kimya bila kulizungumzia kumbe mmoja wao hajaridhika....ni bora mkae mzungumze yaishe pindi tatizo linapotokea lakini ukilimbikiza lazima itakuwa msala na itakuwa ngumu sana kuweza kukaa chini mzungumze maana mtaanza kukumbushia yale ambayo hayakufikiwa muafaka na ugomvi kuanza upay
kuondoa stress hizi kunawakina mama wengi wanaamua kuhamishia mapenz kwa watoto kwa kuwatoa out every sunday after church 1st service hamna kurudi home hadi jioni kuoga na kulala ready kwa monday sasa baba nae anaona wife anafaidi so next weekend anawawah watoto nae kuzunguka nao outing na kurudi jioni kuoga kulala watoto wanenjoy ila mke au mume wakikutana chumbani usiku ndita kama kawa utasikia unanilalia na mguu wako sogea uko lol cjui nn kifanyike kuokoa haya maswaibu :help:
hii ni nature ya wanawake kama wanavyoeleweka kwamba ni ua au pambo la nyumba shurti kulisifia au kulitambua kama lipo
Je kutokana na uchunguzi wangu niko sawa juu ya hii? naombeni maoni yenu pia,
Mwanaume ambaye yuko insecure juu ya mke wake katika maeneo yote yaani kuanzia kitandani hadi kimaongezi na utashi atakuwa hivi,
-Anamtukana mke wake na kumtamkia maneno ya kumuudhi kwa kosa dogo tuu, kosa lake yeye mwenyewe mwanaume, kosa lililofanyika zamani na kuchukulia ndo ulivo wew mwanamke.
-Hajiamini kama amefanikiwa kuwa na mke mzuri na anammiliki hadi watu wa nje wamwambie, kitu kizuri akiambiwa na mkewe hakikubali hadi aambiwe na mtu wa nje.
-Akifanya kosa na likionekana live-kubambwa au kufumwa akifanya uovu huwa mpole kama choroko na huomba msamaha kama mtoto na kuahidi kutorudia tena na kesho akirudia hilo kosa usithubutu kumkumbusha kwasababu utakula makofi hadi usahau jina lako
-Anatumia kilevi kupata confidense ya kujieleza na anajihisi hasikilizwi na kuishia kutishia nikijua unamahusiano nje utakoma
-Hujibu dry au short kwa story anazopigiwa na mkewe hata za kuchekesha ili kuvunja ukimya na mwisho huyageuza maongezi kuwa ugomvi na mwisho hasira na kurushiana maneno machafu na mwisho kununiana
Wanaume hawa huwa kero kwa wake zao wazuri na mwisho wa yoote mke hutafuta stress release nje itakayo mchekesha, itakayomfanya akijirembe asifiwe umependeza, hata zawadi ya pipi tu hutosha kumteka mwanamke wa namna hii
mwnamke huyu huwa amejeruhiwa tayari na akipata mtu anayemjali kwa kumsikiliza na kuongea na e kwa upole hulala na kuwaza muda wote maongezi mapya na kukunja ndita kwa mume wake.
Angalizo mwanaume wa jinsi hii tunzamke wako akipata wanaomjali nje hatakusikiliza tena na hatakuwa anaogopa kuvunja ndoa.
-Wanawake wengi wa dhahama ya ndoa kama hii hujaribu kwa nguvu zao zote kujenga hiyo ndoa isibomoke pamoja na kero zote wanazopata ila ogopa A FED UP WOMEN!!
Then mwanamke huyo akifanya hivyo unavyosema, a fed up woman anafanyaga, je hufanikiwa kumgeuza huyu mwanaume kuwa mzuri kama anavyotaka yeye? Je huo wa kukimbilia nje nao si udhaifu mwingine unaofanya wanawake waitwe majina mabaya?