Mume wa Khadija Koppa ambaye ni diwani kata ya Magomeni - Bagamoyo amefariki dunia

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Mume wa Malkia wa Mipasho Khadija Kopa ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mogomeni Bagamoyo kupitia CCM Jaffar Ali Yusuf amefaiki dunia mapema asubuhi ya leo katika Hospitali ya Lugalo.

Kwa mujibu wa baadhi ya ndugu wa marehemu wamesema ndugu yao huyo alikuwa anaumwa kwa muda mrufu na alianza kuumwa siku chache baada ya kushinda kiti cha udiwa ni katika kata hiyo. Hata hivyo ndugu hao hawakuwa tayari kusema aina ya ugonjwa uliokuwa unamkabili ndugu yao huyo.


Ikumbuke kuwa Bwana Jaffar Ali Yusuf alichaguliwa kuwa diwani wa kata ya Magomeni miezi michache iliyopita baada ya diwani wa alikuwa anaogoza kata hiyo kupitia CCM Abdalah Mshindo kufariki dunia mwaka jana.


Habari kamili zitakuja kadri tutakapo zipokea

..........................................................UPDATE .................................................................

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.



More update
Msiba wake umetawaliwa sana na mambo ya ushirikina kwani, hata kwenye kaburi lake wamekuta chungu kilichofukiwa ambacho haikujulikana mapema nani alikiweka, Hata hivyo baada ya sala ilibidi mwili wa marehemu uzikwe.




Enzi za uhai wa Mrehmu hapa akiwa na Mkewe Bi Khadija Omar Kopa

 

Attachments

  • Khadijanamumewe.JPG
    37.2 KB · Views: 716
jamani mbona hicho kiti kimepata mkosi mara mbili au kuna mkono wa mtu mambo ya uchawi
 

Alikuwa diwani kitambooo, ama mpaka anakufa......ili iwe kufa kufaana
 
Aliekuwepo kabla nae alifariki,na pengo lake likazibwa na mme wa khadija koppa nae kafariki,who is next then?

"bagamoyo hii hatutaki upinzania kabisa hasa chadema haitakiwi hapa"by riz1 kupitia gazeti la jamhuri


RIP BROTHER
 
Nadhani andiko hili limetokana chama alichokuwa.......nadhani ni vema tukawa na siasa za ukomo......P.K.A Diwani....
Chuki hizi za kisiasa hazitusaidii kitu


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kama ni hivyo; Hicho kiti kuliko kugombea mara mia nikautangaze ukristo Somalia naweza nikasalimika duuuhh! R.I.P Mpendwa
 
Huyu mama omari kumbe anauguza mume halafu anapuyanga2. Jana alikuepo rukwa kwenye tamasha. R.I.P.
 
Aliekuwepo kabla nae alifariki,na pengo lake likazibwa na mme wa khadija koppa nae kafariki,who is next then?

"bagamoyo hii hatutaki upinzania kabisa hasa chadema haitakiwi hapa"by riz1 kupitia gazeti la jamhuri


RIP BROTHER
kama ni kweli wanasema CDM haitakiwi hivyo vifo ni laana ya kuikataa CDM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…