Mume wa ndoa akikujibu hivi utajisikiaje?

...uhudumiwe kwani wewe mtoto ?!..jihudumie mwenyewe
Sent using Jamii Forums mobile app
 
....constructive advice,..MTU mzima unalalamika kuhudumiwa kweli ?!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bidada anamaduka yake ya dawa 2 jamaa anahakikisha anasimamia

Kama alikutwa na duka lake kwa nini asibaki kulisimamia Hilo ili apate mahitaji yake asiboreke na majibu ya jamaa?

Kuna mama mmoja ni mke wa Doctor wa chuo kikuu kimoja maarufu , huyo Doctor Ana mashule pia Tena yanajaza kweli kweli so pesa iko ndefu. Yule mama amepewa kumsimamia ishu za makusanyo ya Ada kwa kuwa wafanyakazi wakiwekwa wanaiba mno kwa kushirikiana na management iliyopo. Cha kushangaza Yule Doctor huwa hamhudumii mkewe kwa chochote zaid sana Mara moja kwa week atampatia elf 2 ya nauli jioni ambayo haitoshi mafuta ya Corolla anayotumia (ambayo alinunua mwenyewe kwa kuwa ni mfanyakazi pia). Yule mama anachofanya anaiba mbayaaaa kwenye makusanyo ya mumewe. Hapo anafanya yake na anapata mahitaji . Yule Doctor ni Malaya mbaya na anahonga hatari. So bi dada ajiongeze kikubwa asikamatwe tu maana ukute michepuko inafaidi Kama kawaida Ila yeye ndo anateseka
 
Kiwango Cha chini ambacho anaweza pata ni 2m icho nikiwango Cha chini
Hiyo 2m ni hela anayoingiza kwa mwezi?Kama ni hivyo anajimudu vizur.
Lakini pia inategemea tena mwanzoni ulianza naye kwa staili gani,Kama ulianza kwa kumbughuzi kwa kuomba misaada ya kila siku isiyokuwa na mwisho wanaume huwa tunachoka na kuzira.
Jitahidi kuwaseti ndugu zako kwamba inapotokea shida ya msingi tu ndio waombe msaada.
Kwa mfano Kama Kuna mgonjwa amelazwa na inahitajika pesa ya matibabu hii ni shida ya msingi.
Au imetokea mzazi ameishiwa kodi ya nyumba na vyombo vinataka kutolewa nje,hii ni shida ya msingi.
Au imetokea mdogo wako anasoma na anadaiwa ada hadi inapelekea anataka kufukuzwa shule hii ni shida ya msingi.
Ila usipende mme wako aombwe pesa kila siku hadi za kwenda kufanyia starehe,itakuwa fedheha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Duh, muda mrefu sana ulipumzika kuleta thread za namna hii.
 
Tatizo ninaloliona hapo ni majibu yake machafu hilo la kutokutoa mahitaji lipo ndani ya ndoa nyingi.Wanaume wengi hawajui majukumu yao,yeye anataka wewe utimize yake lakini yeye hapana.Na ukimkumbusha majukumu yake ugomvi unaanzia hapo.Kuna haja ya vijana kupewa semina na kuelezwa majukumu yao kwenye ndoa na sio kupenda papuchi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ni simango kubwa mno. Hivi wanaume wenzetu wa hivi mlilazimishwa kuoa au? Ningekuwa huyo mwanamke naondoka mchana jua likiwa katikati ya dunia na sitageuka nyuma. Nitaapa nikigeuka nibadilike kuwa mnara wa chumvi.

Dada jipange huyo mwanaume labda ulilazimisha kuelewa naye au ana mwanamke pembeni hivyo hana haja na wewe. Chapa lapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…