Mimi niliwahi kumwuliza mume wa shangazi yangu mimi nimwiteje? Akaniambia mimi ni shemeji yako. Kwa hiyo ninavyofahamu mume wa shangazi ni shemeji yangu na tulikuwa tunaitana hivyo!!
Wanaomwita mume wa shangazi kuwa ni baba shangazi ni makosa!! Unaposema baba shangazi unamaanisha ni baba wa shangazi. Lakini baba wa shangazi ni babu mzaa baba yako na mzaa shangazi yako,
Karibuni tujadili mume wa shangazi tumwiteje? Vinginevyo tumbatize jina fulani na uwe ni mchango wa jamii forum kwenye kukuza msamiati wa kiswahili. Nawaza tumtize kumwita SHANGAMU. (kifupi cha shangazi mumewe!)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.